Waingereza washambuliwa Zanzibar
 
 
Polisi katika kisiwa cha Zanzibar wamesema wanawake 
wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao baada ya 
kuvamiwa mwendo wa usiku.
                     
Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume 
wawili waliwatendea wanawake hao Katie Gee na  Kirstie Trup, wote wenye 
umri wa miaka 18 kutoka  London,kitendo hicho walipokuwa wakitembea 
katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.
                     
Wanawake hao ni walimu wa kujitolea wakifanya kazi kisiwani humo
                     
Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi ya wanaume hao. 
                     
Katika taarifa yake shirika la usafiri la i-to-i nchini Uingereza lilisema kuwa wanawake hao wameondoka hospitalini.
                     
Kwa upande wake wizara ya mambo ya ndani 
Uingereza ililezea wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wake na 
kuwa tayari imetoa msaada kwao kupitia kwa ubalozi wake.
                     
Wanawake hao, wanasemekana kufanyia kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi hilo haijulikani.
                     
Polisi wanasema kuwa wanawake hao wenye umri wa 
miaka 18 walikuwa wakitembea katika mji wa Mawe kisiwani Zanzibar ambao 
ni kivutio kikuu cha utalii kisiwani humo, wakati wanaume wawili 
waliokuwa wamepanda piki piki walipowamwagia Acid kwenye mikono , vifua 
na nyuso zao.
                     
Wanawake hao walipelekwa kwa ndege hadi Dar es 
Salaam ambako walipokea matibabu . Afisa wa wizara ya afya amesema kuwa 
majeraha yao si ya kutishia maisha .
                     
Polisi wa Zanzibar wamesema ni mara ya kwanza kwa raia wa kigeni kushambuliwa kwa namna hiyo na kwamba wanawasaka wahusika.
                     
Zanzibar ni kisiwa kinachokaliwa na idadi kubwa 
ya waislam na shambulio hilo linakuja katika kipindi cha mwisho wa mwezi
 mtukufu wa Ramadhan , wakati watu wakisherehekea sherehe za Eid
SOURCE:BBC 
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment