Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la MATRIDA ERICK mwenye umri wa
miaka ishirini mkazi wa magamba ,wilaya ya chunya ,amejifungua mtoto
jinsi ya kiume na wakati huohuo na chura.
Mkunga aliyemzalisha bi AGGRIPINA SIKANYIKA mkazi wa MBUYUNI wilaya ya
chunya amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa alasiri agosti 13
mwaka huu,mara mwanamke huyo kufikishwa kwa mkunga huyo na mumewe
aitwaye BUNDALA JOSEPHAT ISANDU mwenye umri wa miaka thelathini na tano
MATRIDA amesema huo ni uzao wake wanne na kwamba alishangazwa na kiumbe
hicho ingawa wakati anajifungua hakupata tatizo lolote na pia
alifurahia kupata mtoto wa kiume mwenye afya na alisikitishwa kupata
hicho kiumbe ambacho kilikuwa na miguu ya mbele yenye vidole vinne na
miguu ya nyuma vidole vitano vya binadamu.
Kwa upande wake AGGRIPINA amesema mtoto alikuwa katika kondo lake na
chura alikuwa katika kondo lake la nyuma la uzazi wa mwanamke huyo na
pia ameeleza kuwa hilo ni tukio la tatu ambapo la kwanza mwanamke
alijifungua kichwa cha ng’ombe mwaka jana na la pili mwaka huu mwezi wa
tano ambapo mwanamke alijifungua chura badala ya binadamu kwa hiyo hili
ni tukio la tatu hivyo hakushangazwa na tukio hilo.
Hata hivyo mume wa Matrida amesema katika familia yao hilo ni tukio la kwanza na kwamba limewashangaza.
Baada ya tukio hilo mkunga alimtafuta mwenyekiti wa kijiji cha MBUYUNI
bwana CONRAD WAMBOKA ambaye alimtaarifu mtendaji wa kijiji MICHAEL
SANZIMWA ambao walishuhudia tukio hilo na walimwamuru mkunga huyo
kuondoa kiumbe hicho ‘’CHURA’’ kwenye kondo la uzazi.
Aidha chura hicho kilikufa na ndugu siku moja baadae ambapo ndugu walikabidhiwa na taratibu za mila zilifuatwa.
Baadhi ya ndugu wamehusisha kitendo hicho na imani za kishirikina zilizokithiri huko wilayani chunya.
Mkunga akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na
Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.
\\
Kushoto ni Matrida Erick (20) aliyejifungua mtoto pamoja na kiumbe hicho
cha ajabu akiwa na mkunga Agripina Sikanyika aliyembeba mtoto wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kujifungua kwa mkunga huyo
Mtoto aliyezaliwa pamoja na kiumbe cha ajabu kinachofanana na chura
No comments:
Post a Comment