ANC kususia ibada ya Marikana
Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wamekusanyika katika
mgodi mkubwa wa dhahabu nyeupe kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa
wachimba migozi 34. Chama tawala cha ANC kimesema hakitahudhuria
makumbusho ya leo kikisenya yanatumiwa kukejeli utawala wa nchi.
Katika maadhimisho hayo Afisa mtendaji wa
kampuni ya, Lonmin, Ben Magara amwaomba mshamaha familia za wachimba
migodi 34 waliouawa.
Tofauti kati ya makundi mawili ya
vyama vya wafanyikazi zililaumiwa kwa kuzuka vurugu zilizotokea mwaka
jana.Chama kilicho na uhusiano wa karibu na ANC- National Union Of
Mineworkers kimepingwa na wachimba migodi wengi na kuanzisha chama
kipya. Mauaji hayo yalisababisha gathabu ya umma na kupelekea lalama
nyingi dhidi ya sekta ya madini.
Afrika Kusini ina asili mia 80 ya madini ya
dhahabu na dhahabu nyeupe.Mauaji ya wafanyikazi hao yalitajwa kuwa
mabaya zaidi tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini mwaka
1994. Sherehe za leo zimepangwa na chama kipya cha kutetea maslahi ya
wachimba migodi Mineworkers and Construction Union (Amcu) ambacho
kinashinikiza nyongeza zaidi ya marupurupu ya wafanyikazi.
AMCU ndicho kikubwa zaidi katika mgodi wa
dhahabu nyeupe inayomilikiwa na kampuni ya Lonmin.Baadhi katika chama
tawala cha ANC wameelezea hofu huenda chama hicho kikaungana na aliyekua
kiongozi wa vijana Julius Malema ambaye alifukuzwa chamani kwa makosa
ya nidhamu.
Malema ameunda chama chake cha kisiasa. Rais
Jacob Zuma aliunda tume ya kuchuguza matukio yaliyopelekea mauaji ya
wachimba migodi hio. Mwandishi wa BBC Afrika Kusini anasema kumekuwa na
ghathabu ya umma kwani hadi sasa hakuna polisi hata mmoja
aliyewajibishwa na mauaji hayo.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment