Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam leo limefanikiwa kumkamata
askari bandia akiwa amevaa Sare za Jeshi la Polisi kitengo cha usalama
barabarani.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, DCP Suleiman Kova amesema leo majira ya saa
moja na nusu asubuhi wamefanikiwa kumkamata James Hussen mwenye umri wa
miaka 45 mkazi wa Kimara Tangi Bovu akiwa amevaa sare hizo huku
akiendelea na utapeli wa kujifanya askari wa kitengo cha usalama
barabarani.
Aidha Kamanda Kova ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la
polisi mara wanapomtilia mashaka askari yeyote na pia kuwaomba wananchi
wasikubali kupigwa bao bali kuwataka askari kwenda nao kituo cha polisi
pindi wanapokamatwa na makosa.
No comments:
Post a Comment