Friday, 2 August 2013

Duru ya pili ya uchaguzi Mali

 

Uchaguzi wa Mali ambao umekuja kufuatia mapinduzi ya kijeshi pamoja na waasi kuteka sehemu ya Kaskazini mwa nchi, utakuwa na duru ya pili, kwa mujibu wa tangazo la serikali.

Hakuna mgombea aliyepata zaidi ya silimia hamsini ya kura zilizopigwa kudai ushindi.

Waziri mkuu wa zamani, Ibrahim Boubacar Keita na aliyekuwa waziri wa fedha, Soumaila Cisse watatoana kijasho katika duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika tarehe 11 Agosti.

Uchaguzi unanuia kurejesha demokrasia baada ya zaidi ya mwaka mmoja ya mgogoro wa kisiasa

No comments:

Post a Comment