Jeshi Nigeria "lamua" kamanda wa Boko Haram
Jeshi nchini Nigeria limetangaza kuwa limemua kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi la Boko Haram.
Taarifa hizo za kijeshi zemesema kuwa kiongozi
huyo aliyeuwawa ni Momodu Bama,ambaye ni wa pili katika uongozi wa kundi
hilo la wapiganaji.
Mapema mwezi huu wafuasi wengine wa
kundi hilo la Boko Haram ambao walikuwa wamekamatwa walifichua kwamba
huyo kamanda wao alikuwa ameuawawa.
Msemaji wa Jeshi Brig Jenerali Chris Olukolade
amesema Momodu Bama, ambaye pia anafahamika kama "Abu Saad", alikuwa na
ujuzi wa kufyatua makombora ya kutungua ndege.
Mapema mwezi wa Mei, Nigeria ilitangaza hali ya
hatari katika maeneo ya kaskazini Mashariki mwa nchi ili kupambana na
wapiganaji wa Boko Haram.
Hata hivyo hadi sasa hakuna taarifa huru
kuthibitisha kuuwawa kwa Bwana Momodu Bama nao Boko Haram wenyewe hawaja
thibitisha kifo cha kiongozi huyo.
Jenerali Olukolade, alisema Momodu Bama alikuwa
ni mmoja ya viongozi wa Boko Haram waliokuwa wakitafutwa zaidi na
kulikuwa kuna zawadi ya dola $155,000, £100,000 kwa yeyote atakaye toa
habari zitakazosaidia kukamatwa au kuuwawa kwake.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment