Clinton ampongeza Rais Paul Kagame
Aliyekuwa rais wa marekani Bill Clinton amempongeza
rais wa Rwanda Paul Kagame licha ya madai kwamba amekuwa akiunga mkono
makundi ya waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo
yanakiuka haki za kibinadamu.
Bwana Clinton amesema katika mahojiano na BBC kwamba madai hayo ambayo Rwanda inayakataa hayajathibitishwa mahakamani.
Pia alisema kuwa kuna changamoto kubwa katika
mpaka wa Rwanda na Congo, kwani una watu chungu nzima ambao walihusika
na mauaji ya halaiki miaka ya tisini.
Lakini bwana Clinton amesema kuwa anathamini
serikali ya Rwanda kutokana na mafanikio ya kiuchumi yalioafikiwa chini
ya rais Kagame.
Kiongozi huyo amekuwa akizuru mataifa ya Afrika pamoja na mwanawe Chelsea ili kujionea miradi ya wakfu wake.
SOURCE:BBC
No comments:
Post a Comment