Rais mpya wa Iran ashika madaraka
Rais mteule wa Iran Hassan Rouhani anaapishwa katika sherehe mjini
Tehran ambapo atapewa idhini ya kiongozi wa kidini nchini humo,
Ayatollah Ali Khamenei.
Rouhani ambaye alikuwa mpatanishi kwenye mazungumzo ya mradi wa
nuklia wa Iran, alishinda uchaguzi wa urais nchini Iran katika duru ya
kwanza.
Wakati wa kampeni zake rais huyo mteule aliahidi
kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, na alisema ataimarisha
uhusiano kati ya taifa hilo na jamii ya kimataifa ambao uliharibika
zaidi wakati wa utawala wa Rais Mahmoud Ahmedinejad.
SOURCE:BBC
No comments:
Post a Comment