
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, 
limetangaza dau la Sh100 milioni kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa 
taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia 
maji baadhi ya watu yanayodhaniwa ni tindikali.
 
                
              
Hatua hiyo inatokana na vitendo hivyo kushamiri maeneo mbalimbali nchini.
                
              
Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova, 
alisema vitendo hivyo havipaswi kuvumiliwa na kuwaomba wananchi kutoa 
ushirikiano kwa kuwafichua watu hao.
                
              
“Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe 
mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha 
vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa,” alisema Kova.
                
              
Hivi karibuni Mkurungezi wa Maduka ya Home 
Shopping Center, Mfanyabiashara wa Lebonon na raia wawili wa Uingereza 
walimwagiwa maji yanayodhaniwa ni tindikali.
                
              
                
              
 
 
No comments:
Post a Comment