Tanzania imekalia hazina. Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ina akiba ya
madini ya dhahabu wakia milioni 36. Katika orodha ya wazalishaji wakubwa
wa dhahabu Tanzania inashika nafasi ya tatu nyuma ya Ghana na Afrika
Kusini.
Lakini hadi sasa utajiri wa madini hayo haukuwanufaisha wananchi
kutokana na kwamba migodi hiyo iko kwenye mikono ya makampuni ya
kimataifa. Mwishoni mwa miaka ya 1990 serikali ya nchi hiyo imezivutia
kampuni hizo za migodi kwa kupunguza kodi na leseni zake kuwa rahisi.
Hata hivyo kunakuwepo na mizozo kwenye sehemu nyingi za migodi kati ya
kampuni hizo na wananchi wenyeji. Hususan hali hiyo imejitokeza kwenye
mkoa wa Mara Kaskazini ulioko magharibi kabisa ya eneo la kaskazini
magharibi mwa Tanzania kwenye mpaka na Kenya.Hapo kila kitu kinahusiana
na dhahabu na kwamba kwa gramu chache tu za dhahabu watu wanakuwa tayari
kuhatarisha maisha yao.
Wafanyakazi wavamizi
Wanasema wakati ni dhahabu ni masafa ya kama nusu saa kwa mwendo wa gari
kutoka kijiji cha Kewanja hadi mpaka wa Kenya. Jumanne anauparamia
mlima mkubwa wa kifusi cha migodi akiwa kama mita chache tu kufika juu.
Kijana huyu ni mvamizi kwa sababu mlima wa vifusi aliokuwa ameuparamia
unamilikiwa na kampuni ya dhahabu ya African Barrick Gold (ABG) tawi la
kampuni kubwa kabisa ya kuzalisha dhahabu duniani ya Barrick Gold kutoka
Canada. Mawe yalioko katika mlima huo ni taka kutoka kwenye mgodi ulio
karibu ambapo hata hivyo huwa chini ya ulinzi wa kampuni hiyo.
Hazina chini ya ulinzi mkali: Mgodi wa dhahabu Mara Kaskazini
Kwa wananchi wengi wanaoishi katika kijiji cha Kewanja katika
mkoa wa Mara Kaskazini masalia hayo ni pato pekee kwao. Kila siku
huuvamia mlima huo wa kifusi mara kwa mara kwa matarajio ya kupata
mabaki kidogo ya dhahabu.
Kwa mujibu wa Jumanne mtu mmoja kati ya kila watu watatu ni mvamizi
mahala hapo. Wengi kati yao ni vijana wa kiume na kuna na hata watoto.
Jumanne ana umri wa takriban miaka 20 na huuza dhahabu anayoipata katika
soko la kijiji ambapo hujipatia laki mbili za Tanzania kwa mwezi sawa
na euro mia moja, kwa hiyo Jumanne ni miongoni mwa watu wanaojipatia
kipato kikubwa katika mkoa huo.
Kuhatarisha maisha
Hata hivyo Jumanne anasema mzungu akimaanisha wamiliki wa mgodi huo
amekuwa akiwabana sana wasichukue mawe yalioko kwenye mlima wa kifusi
cha mgodi na kwamba watu wengine hupoteza maisha yao lakini maisha ni
magumu na hawana njia nyengine ya kujipatia kipato.
Kuhatarisha maisha: Mwanamigodi katika kijiji cha Kewanja
Eneo la kampuni hiyo ya dhahabu huwa liko chini ya ulinzi mkali
ambapo hata polisi wa taifa hushiriki katika kutowa ulinzi huo. Walinzi
hao huwa na mabomu ya kutowa machozi, risasi za mpira na na silaha
nyengine kali. Kila mara watu huuwawa na wengine kujeruhiwa. Mwaka 2012
pekee kutokana na vyombo vya habari vya ndani ya nchi takriban watu
wanane wameuwawa karibu na mgodi huo au kwenye mgodi wenyewe. Kwa
wavamizi hasira inazidi kupanda ambapo mvamizi mmoja aliekataa kutaja
jina lake amesema hakuna mtu anayejali juu ya watu walioko hapo na dio
maana hupigwa risasi kama mbwa kwamba polisi hutekeleza kila
wanachoagizwa na kampuni na wanakuwa kama vile ni vibaraka wao.
Donge nono
Kwa upande mwengine fedha nyingi hupatikana kutoka kwenye milima hiyo ya
vifusi vya migodi. Mgodi huo wa Mara Kaskazini umekuwa na wamiliki
mbali mbali hapo mwaka 2006 ulikuwa nchini ya mikono ya AGB. Kampuni
hiyo zaidi ya muongo mmoja uliopita imekuwa ikijishughulisha nchini
Tanzania na kwa hivi sasa pia inashughulikia migodi mengine minne ya
dhahabu nchini humo.
Huko Mara Kaskazini kwa mujibu wa taarifa za kampuni hiyo wafanyakazi wa
migodi 360 moja kwa moja wanatoka katika maeneo hayo na wengine zaidi
ya 1,500 wakaazi wa hapo wanafanya kazi kwa njia ya mikataba na kampuni
hiyo. Haata hivyo hiyo haiwezi kuitwa miujiza ya kazi. Mgodi huo hutowa
ajira chache tu kwa wanakijiji 70,000 waliokuwepo kwenye vijiji vilio
karibu na mgodi huo. Ingawa kampuni za migodi hupata fedha nyingi lakini
hutowa ajira chache hili ni tatizo halisi katika sekta ya malighafi.
Kwa mwaka 2001 pekee kampuni hiyo ya ABG imejipatia zaidi ya euro
milioni 200 kutoka mgodi wake huo wa Mara Kaskazini.
Miradi ya kijamii
Gary Chapman meneja wa mgodi anasema bila ya shaka kampuni hiyo
inatakiwa kuwajibika kwa jamii na kwamba wanachukua hatua kujenga
uaminifu baina yao na jamii ili kuheshimiwa na kuthaminiwa na jamii kwa
nia ya kushirikiana na kuleta maendeleo. Kutimiza lengo hilo kampuni
hiyo ina kitengo cha kushughulikia uhusiano na umma huko Mara Kaskazini
ambacho kinaundwa na wafanyakazi 17 wa kiume na wa kike. Wafanyakazi hao
wa masuala ya jamii hufanya ziara vijijini na kuwasiliana na wakuu wa
vijiji na watu wenye kushughulikia jamii. Kitengo hicho kinasimamia
miradi ya jamii ya kampuni hiyo. Kitu kimoja ambacho kampuni ya African
Barrick Gold inajivunia sana ni shule ya sekondari ya Ingwe ambayo iko
dakika chache kwa mwendo wa gari kutoka mgodi wao.
Anajivunia shule mpya: Mwalimu Mkuu Mageka
Kwa madarasa ambayo yamechakaa kampuni hiyo ya ABG imeyafanyia
ukarabati hapo mwaka 2012 na hivi sasa wanashughulikia ujenzi wa ukumbi
wa chakula na majengo zaidi ya shule kwa kutumia kampuni za kijenyeji
kwa lengo la kuzalisha ajira zaidi. Hili ni jambo linalolitiliwa mkazo
na kampuni hiyo ya AGB. Joash Mageka mkuu wa shule hiyo anafurahia
mabadiliko mazuri kwana shule hiyo sasa inapendeza na kwamba pia idadi
ya wanafunzi wanaokwenda kufanya kazi kama wavamizi imepunguwa. Anasema
ingawa bado kuna wengine wanaoendelea kwenda wanajaribu kuwaelimisha juu
ya umuhimu wa elimu na vipi inaweza kuwasaidia katika maisha yao ya
baadae. Shule hiyo ni mradi wa kupigiwa mfano na kwa kampuni hiyo huo ni
mfano wa maendeleo ya mkoa huo.
Mkoa unaendelea
Kwa mujibu wa taarifa za kampuni hiyo mwaka 2010 kampuni ya AGB imetowa
dola milioni 20. 6 kwa ajili ya miradi ya jamii nchini kote Tanzania.
Kiwango hiki ni chini ya aslimia moja ya faida inayopata kampuni hiyo.
Idara ya uhusiano na umma ya kampuni hiyo inasema sehemu kubwa ya fedha
hizo zimepelekwa Mara Kaskazini. Lakini hilo limetokea miaka miwili tu
iliopita.Kwa nini halikufayika mapema zaidi hakuna mtu anayetaka
kufafanuwa hilo.
Kwa mujibu wa Zakayo Kalebo meneja wa uhusiano wa jamii wa kampuni hiyo
idadi ya nyumba imeongezeka na pikipiki zimejaa na kimsingi watu
wanauona mgodi huo kuwa na manufaa kwa sababu maendeleo makubwa yameweza
kufikia hali ambayo haikuwa hivyo kabla ya kuwepo kwa mgodi huo.
David amehamia Mara Kaskazini kutoka Kenya
Kusema kwamba hali hiyo imesaidia kukuza uchumi au kusema ni
neema ya mali ghafi itakuwa kama ni kutia chumvi kwa Mara Kaskazini.
Biashara ya dhahabu huwavutia watu wengi kutoka nje. Kwa mfano David
Arumba aliigia hapo mwaka uliopita kutoka nchi iirani ya Kenya ana umri
wa miaka 25 ni mtu pekee katika familia yake aliekwenda shule. Lakini
haafiki kufanya kazi za uvamizi na ameamuwa kuwa na kazi tafauti.
Anasema watu wengi wanaokwenda hapo huishia kupigwa risasi na wengine
kujeruhuiwa.
Yeye hakutaka kuwa kwenye matatizo ya kufukuzana na polisi na kuwepo
mahala ambapo hakustahiki.Ameamua kuwa na biashara ya kuosha magari kwa
kuwa inampa uhuru.
Kijana huyo ana sehemu ndogo ya kuosha magari katika kijiji cha Kewanja
na mke wake humsaidia kwa kuuza ndizi na mafuta ya petroli katika chupa
za plastiki.Wengi ya wanavijiji hao wanaishi kwa kutegemea pungufu ya
dola moja kwa siku na kuweza kuwa na maji na umeme ni vitu vya anasa.
Nini tatizo Mara Kaskazini ?
Sospeter Muhongo ni waziri wa madini wa Tanzania mwenyewe anatoka Mara
Kaskazini ni mwanaeleojia na amekuwa katika wadhifa huo kwa miezi
kadhaa. Ameongeza kodi kwa kampuni hizo na amekuwa akitaka zijihusishe
zaidi na miradi ya kusaidia jamii.Muhongo anasema wamejaribu na
hawatosita watafanya juhudi zote kuhakikisha kwamba kuna amani na
usalama katika eneo hilo. Anaona njia moja ya kulitatua tatizo hilo ni
kuwekeza katika elimu ambapo watu watakapokuwa wamejifunza na kuelimika
vizuri watakuja kuwa na fikra tafauti.
"Elimu ni ufumbuzi" Waziri Sospeter Muhongo
Lakini hadi sasa hakuna ishara ya kuwa na fikra tafauti katika
kijiji cha Kewanja mkoa wa Mara Kaskazini. Biashara hiyo haramu ya
dhahabu hufanyika kwa vificho na mawe kuvunjwa vipande vipande kuichuja
dhahabu huko vijijini. Juu ya kwamba utaratibu wa kuisafisha dhahabu
hiyo huhusisha matumizi ya zebaki ambayo ni hatari kwa afya lakini hivyo
ndivyo anavyofanya Jumanne ambaye anasema binaadamu lazima atambuwe
wapi anaweza kupata riziki yake kwani fedha anazoweza kupata kwa siku
moja inabidi asubiri kwa mwaka mzima kuweza kuzipata akijishughulisha na
kilimo.
Kidonge cha dhahabu kinachong'ara kwenye mkono wake pengine hakizidi
hata gramu moja. Huuzwa kwa Euro 20 kwenye soko la magendo. Ni sehemu
ndogo ya utajiri wa mali ghafi lakini ni fedha nyingi kwa maskini
walioko kaskaziini mwa Tanzania.
No comments:
Post a Comment