Saturday, 17 August 2013
Mwakyembe aagiza wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wakamatwe!
Ni Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed.
Aidha, amesema wafukuzwe mara moja ni baada ya kupitia CCTV na kuona namna walivyohusika siku hiyo kwani walionekana wakipiga simu mara watoke nje kinyume na sheria za chumba cha ukaguzi (vifaa hivi ni kama vilivyotumika na CHADEMA kuwanasa polisi waliorusha bomu na baadae kuwashambulia kwa risasi).
Hao waliotajwa hapo juu ni waliofanikisha kupitisha kilo 180 zilizokuwa zimebebwa na wasichana wawili (Masogange na mwenzake) waliokamatwa huko Afrika kusini..
Aidha, amesema wafukuzwe mara moja ni baada ya kupitia CCTV na kuona namna walivyohusika siku hiyo kwani walionekana wakipiga simu mara watoke nje kinyume na sheria za chumba cha ukaguzi (vifaa hivi ni kama vilivyotumika na CHADEMA kuwanasa polisi waliorusha bomu na baadae kuwashambulia kwa risasi).
Hao waliotajwa hapo juu ni waliofanikisha kupitisha kilo 180 zilizokuwa zimebebwa na wasichana wawili (Masogange na mwenzake) waliokamatwa huko Afrika kusini..
ANC kususia ibada ya Marikana
Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wamekusanyika katika mgodi mkubwa wa dhahabu nyeupe kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa wachimba migozi 34. Chama tawala cha ANC kimesema hakitahudhuria makumbusho ya leo kikisenya yanatumiwa kukejeli utawala wa nchi.
Katika maadhimisho hayo Afisa mtendaji wa kampuni ya, Lonmin, Ben Magara amwaomba mshamaha familia za wachimba migodi 34 waliouawa.
Tofauti kati ya makundi mawili ya vyama vya wafanyikazi zililaumiwa kwa kuzuka vurugu zilizotokea mwaka jana.Chama kilicho na uhusiano wa karibu na ANC- National Union Of Mineworkers kimepingwa na wachimba migodi wengi na kuanzisha chama kipya. Mauaji hayo yalisababisha gathabu ya umma na kupelekea lalama nyingi dhidi ya sekta ya madini.
Afrika Kusini ina asili mia 80 ya madini ya dhahabu na dhahabu nyeupe.Mauaji ya wafanyikazi hao yalitajwa kuwa mabaya zaidi tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini mwaka 1994. Sherehe za leo zimepangwa na chama kipya cha kutetea maslahi ya wachimba migodi Mineworkers and Construction Union (Amcu) ambacho kinashinikiza nyongeza zaidi ya marupurupu ya wafanyikazi.
AMCU ndicho kikubwa zaidi katika mgodi wa dhahabu nyeupe inayomilikiwa na kampuni ya Lonmin.Baadhi katika chama tawala cha ANC wameelezea hofu huenda chama hicho kikaungana na aliyekua kiongozi wa vijana Julius Malema ambaye alifukuzwa chamani kwa makosa ya nidhamu.
Malema ameunda chama chake cha kisiasa. Rais Jacob Zuma aliunda tume ya kuchuguza matukio yaliyopelekea mauaji ya wachimba migodi hio. Mwandishi wa BBC Afrika Kusini anasema kumekuwa na ghathabu ya umma kwani hadi sasa hakuna polisi hata mmoja aliyewajibishwa na mauaji hayo.
CHANZO:BBC
Maelfu wajitokeza kuandamana tena Misri
Maelfu ya wafuasi wa Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi wameanza maandamano mengine mjini Cairo, huku kukiwa na hofu ya kuzuka makabiliano zaidi. Maafisa wa usalama wamezingira barabara kuelekea medani ya Ramses ambapo maandamano hayo yalipangwa kufanyika. Maandamano ya sasa yanajiri siku mbili baada ya jeshi kuvunja kambi ambapo wafuasi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood walikua wamesalia kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Makabiliano yalizuka na zaidi ya watu 600 wakauawa, maelfu walijeruhiwa.Maandamano zaidi yanaendelea nje ya mji mkuu Cairo na taarifa zinasema watu wanne wameuawa kwenye makabiliano eneo la Ismailia. Polisi wa Misri wameamrishwa kutumia risasi za moto kulijinda na kulinda majengo ya serikali dhidi ya kushambuliwa.
Huku utawala wa mpito ukitangaza hali ya
hatari, mwandishi wa BBC aliyeko Cairo amesema taharuki imetanda mji
mzima.Maelfu walikusanyika nje ya msikiti mmoja baada ya Muslim
Brotherhood kuwaomba wafuasi wao kuandamana baada ya sala ya ijumaa
wakiitaja kama siku ya hasira.
Magari ya kijeshi yanashika doria mjini Cairo, na njia ya kuingia medani ya Tahir kitovu cha maandamano ya mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani Hosni Mubarak imefungwa. Huku haya yakiarifiwa wapinzani wa Mohammed Mosri pia wamepanga kuandamana dhidi ya mahasimu wao. Wakati huo huo watu wameombwa kulinda makaazi yao, makanisa na biashara. Wakristo nchini Misri wamekuwa wakilengwa katika siku za karibuni na makundi ya kiisilamu yenye misimamo mikali. Jumla ya makanisa 25, makaazi na biashara yalishambuliwa hapo Jumatano na Alhamisi.
chanzo;BBC
Friday, 16 August 2013
Daktari aliyemtibu sheikh Ponda Morogoro atiwa mbaroni.. chama cha madaktari chapinga
- DAKTARI ALIYEMTIBU SHEIKH PONDA MOROGORO ATIWA MBARONI..
- CHAMA CHA MADAKTARI CHAPINGA NA KUDAI HANA KOSA
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa (Moi), jana aliondolewa na kupelekwa katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam.
Kitendo hicho kimelaaniwa vikali na familia yake na wafuasi wake, ambao wamepanga kufanya maandamano makubwa leo ...
Sheikh Ponda, ambaye alisomewa shtaka la uchochezi akiwa kitandani na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka ilidaiwa kuwa alitenda kosa hilo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Juni 2 mpaka Agosti 11, mwaka huu. Alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Liwa.
Jana, Polisi waliimarisha doria kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia saa 1:30 asubuhi. Magari matatu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU) yaliyobeba askari wenye silaha yalionekana yakiranda katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
Sheikh Ponda alitolewa wodini saa 4:20 asubuhi chini ya ulinzi mkali wa askari baadhi yao wakiwa wamebeba silaha.
Alionekana akiwa ameshikiliwa na polisi kutokana na kukosa nguvu ya kutembea.
Akiwa amevalia shati lenye rangi ya udongo, kikoi cheupe na kandambili, Sheikh Ponda alipakiwa kwenye gari ndogo aina ya Landcruiser nyeupe lililokuwa na vioo vya giza.
Baada ya kupakiwa, safari ya kuelekea Segerea ilianza saa 4:45. Gari lililombeba lilitanguliwa na gari la FFU lililokuwa na askari wenye silaha likifuatiwa na magari mengine mawili ya FFU yaliyokuwa na polisi wenye sare na magari mengine mawili ambayo yalikuwa na askari kanzu.
Wakili ashangaa, familia yaja juu
Akizungumza baada ya tukio hilo jana, Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro alisema hakuwa na taarifa za kuondolewa hospitali kwa mteja wake na kueleza kushangazwa na kitendo hicho akisema mteja wake alikuwa mgonjwa akiwa anahisi maumivu makali ya kidonda tangu juzi.
“Nimepigiwa simu mchana huu na mmoja wa wanafamilia, nimeshangaa sana kwa sababu nakumbuka jana (juzi Jumatano) Sheikh alishindwa kufanyiwa mahojiano na polisi kutokana na kuhisi maumivu na kizunguzungu,” alisema Nassoro.
Msemaji wa familia, Isihaka Rashid alisema hawakuwa na taarifa ya Sheikh Ponda kupata ruhusa ya kutoka hospitali na kwamba wakati anaondolewa alikuwapo mkewe na kijana mmoja kwani muda huo wanafamilia wengine walikuwa kwenye kikao.
“Nilifika hospitali asubuhi, hatukupewa nakala yoyote ambayo inaonyesha Sheikh Ponda karuhusiwa. Lakini baada ya tukio tulipokwenda kuhoji tukaambiwa wamemruhusu tukapewa na karatasi ya kuthibitisha kuwa ameruhusiwa,” alisema Isihaka.
Sheikh Ponda alifikishwa hospitalini hapo Jumapili iliyopita, akiwa na jeraha ambalo linadaiwa kuwa ni la risasi aliyopigwa na polisi katika mkutano wa Kongamano Mjini Morogoro. Rashid alisema familia imepatwa hofu juu ya usalama wa maisha yake kwa kuwa hali yake bado haijatengamaa kwani alikuwa amevimba mkono.
“Wamemchukua katika hali inayotia shaka kwa sababu hata dawa zake hawakumchukulia, cheti cha ruhusa ya daktari pia kimeachwa, gharama zake za matibabu yake ni Sh1.1 milioni. Tumeambiwa tuchague kama tunataka kulipia au vipi, kwetu tunaona kama wamemteka,” alisema Rashid.
Alisema kutokana na hali hiyo familia imeamua kulirejesha suala la kufuatilia usalama wa maisha ya Ponda mikononi mwa viongozi wa Jumuiya anayoiongoza ili walishughulikie na kwamba tayari wamewajulisha kwamba watatoa tamko leo kwenye Msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni.
Daktari matatani
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amesema watamhoji daktari aliyemtibu Sheikh Ponda Mjini Morogoro. Hata hivyo, Kamanda Shilogile hakutaka kutaja jina la daktari huyo akisema atakuwa anaingilia kazi ya Kamati ya Haki Jinai ambayo ndiyo inayochunguza suala hilo.
Jeraha la Sheikh Ponda limezua utata baada ya mwenyewe kusema kuwa limetokana na risasi aliyopigwa na askari wa jeshi hilo huku polisi wakikana.
Daktari huyo anaaminika kuwa ni miongoni mwa mashahidi muhimu kwani anafahamu chanzo cha kidonda cha Sheikh Ponda.
Inaaminika kuwa alitibiwa katika zahanati ya Al Jamih iliyoko Msamvu baada ya tukio hilo, Ijumaa iliyopita.
Hata hivyo, Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Rodrick Kabangira alipinga kitendo cha daktari kuhojiwa akisema Baraza la Madaktari Tanzania ndilo lilipaswa kumhoji.
“Tayari kuna utata wa jeraha lenyewe na ukweli ni kwamba ripoti ya huyo daktari ni muhimu kwa umma kwani ndiyo itathibitisha chanzo cha jeraha,” alisema.
Alisema hakuna kosa lolote kwa daktari huyo kumhudumia Sheikh Ponda isipokuwa kama atakuwa ameandika taarifa tofauti za jeraha hilo.
“Tatizo kubwa ni kwamba Serikali imekuwa ikiruhusu uchunguzi kwa tume ambazo hazitoi majibu halisi kwa wananchi. Ingetumika tume ya kimahakama au baraza ambalo lina mamlaka hata ya kumfutia usajili wake kama atakuwa amedanganya,” alisema.
Msajili wa Baraza la Madaktari Tanzania, Parot Luwena alisema madaktari hutakiwa kufanya kazi kwa misingi ya taaluma zao wala siyo kwa shinikizo, hivyo kama kuna masuala mengine ambayo polisi wanahitaji, wanapaswa kuzingatia sheria za nchi.
Polisi waonya waandamanaji
Polisi imesema kwamba itadhibiti maandamano yanayotarajiwa kufanyika leo kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Ponda.
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema jana kuwa maandamano yoyote hayatavumiliwa na jeshi hilo.
“Tunapiga marufuku maandamano yoyote, watakaoyafanya wafahamu kuwa jeshi litayadhibiti,” alisema.
Ubao wa matangazo ya Makao Makuu ya Polisi limebandikwa tangazo la kuwataka polisi kuwa tayari kukabiliana na vurugu zozote zitakazotokea.
Tangazo hilo limesema hali ya usalama siyo nzuri na kwamba askari polisi wanatakiwa kujiandaa kukabiliana na vurugu.
-Mwananchi.
HK Customs seizes heroin concealed in metal gear
Hong Kong Customs smashed two heroin smuggling cases at the Hong
Kong International Airport in two weeks and seized a total of 1.5
kilograms of heroin with a value of about $1.3 million.
In
the first case, Customs officers of the Airport Command selected an air
consignment parcel declared as a metal gear from Tanzania, East Africa,
for examination on August 2, and seized 0.7kg of heroin. The drug was
found concealed in a metal gear and could only be detected until the
metal gear was cut apart by a saw.
Customs officers of the
Airport Command continued to closely monitor this smuggling method and
routing. This morning (August 15), another air consignment parcel
declared as a metal gear from Tanzania was selected for examination and
0.8kg of heroin with the same concealment method was unveiled. The
seized dangerous drugs are believed to belong to the same syndicate.
Investigation is ongoing.
Under the Dangerous Drugs
Ordinance, drug trafficking is a serious offence. The maximum penalty is
life imprisonment and a fine of $5 million.
Ends/Thursday, August 15, 2013
Issued at HKT 19:52
NNNN
HUYU NDO KIJANA ALIYEKAMATWA NA MWAKYEMBE AKISAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JN-DAR
Habari ambayo imeripotiwa na ITV inadai kwamba baada ya siku moja ya ziara ya kushtukiza ya Waziri wa uchukuzi Dk. Harison Mwakyembe kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-Salaam, kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kimekamatwa uwanjani hapo katika harakati za kusafirishwa kwenda nchi za nje.
Aliekamatwa ni kijana ambae alikua anazisafirisha hizo dawa zikiwemo bangi pia akielekea nchini Italia.
PICHA ZA MADIWANI WALIOFUKUZWA CCM BUKOBA LAKINI WARUDISHIWA UANACHAMA WAO NA KAMATI KUU
Diwani Alexander Ngalina wa Kata Buhembe na Naibu Meya
Diwani Murungi Kichwabuta wa viti maalum na mjumbe baraza kuu la Taifa la wanawake
Diwani Yusuf Ngaiza wa kata ya Kashai na mwenyekiti wa CCM Bukoba mjini
Diwani Deusdedith Mutakyawa kata Nyanga
Diwani Robert Katunzi wa kata ya Hamugembe
Diwani Richard Gaspar wa Kata ya Miembeni na mjumbe mkutano mkuu wa Taifa wa CCM
Diwani Dauda Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo
Diwani Samweli Ruangisa wa kata ya Kitendaguro
Mama ajifungu mtoto na CHURA huko Mbeya
Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la MATRIDA ERICK mwenye umri wa miaka ishirini mkazi wa magamba ,wilaya ya chunya ,amejifungua mtoto jinsi ya kiume na wakati huohuo na chura.
Mkunga aliyemzalisha bi AGGRIPINA SIKANYIKA mkazi wa MBUYUNI wilaya ya chunya amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa alasiri agosti 13 mwaka huu,mara mwanamke huyo kufikishwa kwa mkunga huyo na mumewe aitwaye BUNDALA JOSEPHAT ISANDU mwenye umri wa miaka thelathini na tano
MATRIDA amesema huo ni uzao wake wanne na kwamba alishangazwa na kiumbe hicho ingawa wakati anajifungua hakupata tatizo lolote na pia alifurahia kupata mtoto wa kiume mwenye afya na alisikitishwa kupata hicho kiumbe ambacho kilikuwa na miguu ya mbele yenye vidole vinne na miguu ya nyuma vidole vitano vya binadamu.
Kwa upande wake AGGRIPINA amesema mtoto alikuwa katika kondo lake na chura alikuwa katika kondo lake la nyuma la uzazi wa mwanamke huyo na pia ameeleza kuwa hilo ni tukio la tatu ambapo la kwanza mwanamke alijifungua kichwa cha ng’ombe mwaka jana na la pili mwaka huu mwezi wa tano ambapo mwanamke alijifungua chura badala ya binadamu kwa hiyo hili ni tukio la tatu hivyo hakushangazwa na tukio hilo.
Hata hivyo mume wa Matrida amesema katika familia yao hilo ni tukio la kwanza na kwamba limewashangaza.
Baada ya tukio hilo mkunga alimtafuta mwenyekiti wa kijiji cha MBUYUNI bwana CONRAD WAMBOKA ambaye alimtaarifu mtendaji wa kijiji MICHAEL SANZIMWA ambao walishuhudia tukio hilo na walimwamuru mkunga huyo kuondoa kiumbe hicho ‘’CHURA’’ kwenye kondo la uzazi.
Aidha chura hicho kilikufa na ndugu siku moja baadae ambapo ndugu walikabidhiwa na taratibu za mila zilifuatwa.
Baadhi ya ndugu wamehusisha kitendo hicho na imani za kishirikina zilizokithiri huko wilayani chunya.
Mkunga akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.
\\
Kushoto ni Matrida Erick (20) aliyejifungua mtoto pamoja na kiumbe hicho cha ajabu akiwa na mkunga Agripina Sikanyika aliyembeba mtoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kujifungua kwa mkunga huyo
Mtoto aliyezaliwa pamoja na kiumbe cha ajabu kinachofanana na chura
chanzo:mbeya yetu
Thursday, 15 August 2013
Trafiki "feki" akamatwa Dar es Salaam
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam leo limefanikiwa kumkamata
askari bandia akiwa amevaa Sare za Jeshi la Polisi kitengo cha usalama
barabarani.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Suleiman Kova amesema leo majira ya saa moja na nusu asubuhi wamefanikiwa kumkamata James Hussen mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa Kimara Tangi Bovu akiwa amevaa sare hizo huku akiendelea na utapeli wa kujifanya askari wa kitengo cha usalama barabarani.
Aidha Kamanda Kova ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara wanapomtilia mashaka askari yeyote na pia kuwaomba wananchi wasikubali kupigwa bao bali kuwataka askari kwenda nao kituo cha polisi pindi wanapokamatwa na makosa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Suleiman Kova amesema leo majira ya saa moja na nusu asubuhi wamefanikiwa kumkamata James Hussen mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa Kimara Tangi Bovu akiwa amevaa sare hizo huku akiendelea na utapeli wa kujifanya askari wa kitengo cha usalama barabarani.
Aidha Kamanda Kova ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara wanapomtilia mashaka askari yeyote na pia kuwaomba wananchi wasikubali kupigwa bao bali kuwataka askari kwenda nao kituo cha polisi pindi wanapokamatwa na makosa.
HAYA NDO MASHITAKA ALIYOSOMEWA SHEIKH PONDA AKIWA HOSPITALINI
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda
Issa Ponda (54), amesomewa shtaka akiwa kitandani katika Kitengo cha
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI).
Katika shtaka hilo, Ponda anadaiwa kuwahamasisha wafuasi wake kufanya kosa.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Riwa, Mwendesha
Mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, alidai kuwa uhamasishaji huo
ulifanyika sehemu mbalimbali nchini kuanzia Juni 2 hadi Agosti 11 mwaka
huu.
Kweka alidai kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu 390 na 35 ya kanuni za adhabu.
Kutokana na shtaka hilo, Hakimu Riwa aliahirisha kesi hadi Agosti 28
na kutoa agizo Sheikh Ponda aendelee kuwa chini ya uangalizi wa vyombo
vya dola wakati akiendelea na matibabu.
Baada ya Hakimu Riwa kuahirisha kesi, wakili wa mshtakiwa Nasoro
Jumaa, alilaumu utaratibu uliotumika na kusema kuwa mahakama imefanya
kazi nje ya muda wa kawaida wa saa za kazi za kiserikali.
Alisema mawasiliano ya awali ilikuwa askari na Tume ya Haki Jinai ya
Jeshi la Polisi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanya mahojiano
na Sheikh Ponda.
Aliongeza kuwa baada ya maofisa hao kufika hali ya Sheikh Ponda
haikuruhusu mahojiano kufanyika na ilipofika saa kumi jioni kila mmoja
alitawanyika.
Jumaa alisema kuwa wakiwa wanakaribia geti la kutokea Muhimbili,
walipigiwa simu kuwa Sheikh Ponda anasomewa mashtaka, hatua aliyodai
kuwa iliwashangaza.
“Kama walikuwa na dhamira ya kumsomea mashtaka wangetuambia, kwa kuwa
ni haki ya msingi kwa mtuhumiwa kuwa na mwanasheria wake kwa ajili ya
kujua taratibu zilizotumika,” alisema.
Alisisitiza kuwa baada ya kupata hati ya mashtaka wanajiandaa kupinga
kosa hilo kwa kile alichoeleza kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
haina uwezo wa kusikiliza kosa la aina hiyo.
Aliongeza kuwa kabla ya kufikiwa kwa hatua ya kumsomea shtaka Sheikh
Ponda, walishaandika barua ya kutokuwa na imani na Tume ya Haki Jinai ya
Jeshi la Polisi katika uchunguzi wao kwa kile alichoeleza kuwa ni
watuhumiwa wa kwanza katika tukio la kujeruhiwa kwa mteja wake.
Awali kabla ya kesi hiyo kusomwa maeneo mbalimbali ya Hospitali ya
Muhimbili hususan jirani na jengo alilolazwa Sheikh Ponda, yalikuwa
yamezingirwa na makachero wa polisi wakiwa na magari matano ya Kikosi
cha Kutuliza Ghasia.
Magari mawili yenye namba PT 2072 na PT 2061 yalikuwa jirani na mlango
wa kuingilia katika kitengo cha mifupa huku askari wakiwazuia wananchi
wasiende kumuona Ponda kwa kile walichoeleza kuwa kuna shughuli za
kiserikali zinaendelea.
Miongoni mwa watu waliozuiwa ni wakili maarufu nchini, Profesa Abdallah Safari.
-Tanzania daima
China zoo under fire for disguising dog as lion
A Chinese zoo's supposed "African lion" was exposed as a fraud when the dog used as a substitute started barking.
The zoo in the People's Park of Luohe, in the central province of Henan, replaced exotic exhibits with common species, according to the state-run Beijing Youth Daily.
It quoted a customer surnamed Liu who wanted to show her son the different sounds animals made -- but he pointed out that the animal in the cage labelled "African lion" was barking.
The beast was in fact a Tibetan mastiff -- a large and long-haired breed of dog.
"The zoo is absolutely cheating us," the paper quoted Liu, who was charged 15 yuan ($2.45) for the ticket, as saying. "They are trying to disguise the dogs as lions."
Three other species housed incorrectly included two coypu rodents in a snake's cage, a white fox in a leopard's den, and another dog in a wolf pen.
The chief of the park's animal department, Liu Suya, told the paper that while it does have a lion, it had been taken to a breeding facility and the dog -- which belonged to an employee -- had been temporarily housed in the zoo over safety concerns.
Users of China's Twitter-like Sina Weibo service mocked the zoo.
"This is not funny at all. It's sad for both the zoo and the animals," said one.
"They should at least use a husky to pretend to be a wolf," said another.
SOURCE:AFP
Jeshi Nigeria "lamua" kamanda wa Boko Haram
Jeshi nchini Nigeria limetangaza kuwa limemua kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi la Boko Haram.
Taarifa hizo za kijeshi zemesema kuwa kiongozi huyo aliyeuwawa ni Momodu Bama,ambaye ni wa pili katika uongozi wa kundi hilo la wapiganaji.
Mapema mwezi huu wafuasi wengine wa kundi hilo la Boko Haram ambao walikuwa wamekamatwa walifichua kwamba huyo kamanda wao alikuwa ameuawawa.
Msemaji wa Jeshi Brig Jenerali Chris Olukolade amesema Momodu Bama, ambaye pia anafahamika kama "Abu Saad", alikuwa na ujuzi wa kufyatua makombora ya kutungua ndege.
Mapema mwezi wa Mei, Nigeria ilitangaza hali ya hatari katika maeneo ya kaskazini Mashariki mwa nchi ili kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.
Hata hivyo hadi sasa hakuna taarifa huru kuthibitisha kuuwawa kwa Bwana Momodu Bama nao Boko Haram wenyewe hawaja thibitisha kifo cha kiongozi huyo.
Jenerali Olukolade, alisema Momodu Bama alikuwa ni mmoja ya viongozi wa Boko Haram waliokuwa wakitafutwa zaidi na kulikuwa kuna zawadi ya dola $155,000, £100,000 kwa yeyote atakaye toa habari zitakazosaidia kukamatwa au kuuwawa kwake.
CHANZO:BBC
Vurugu Misri: Cairo kimya baada ya vifo.
Mji mkuu wa Misri Cairo umeripotiwa kuwa kimya, baada ya operesheni ya kinyama dhidi ya waandamanaji wanaomuunga mkono rais aliyepinduliwa Mohammed Morsi kupelekea vifo vya mamia ya raia. Mauaji hayo yamezua shutuma kutoka jamii ya kimataifa.
Zaidi ya watu 278 waliuwawa wakati maafisa wa usalama waliposhambulia kambi mbili za wafuasi wa Bwana Morsi. Kambi hizo zilianzishwa mwezi uliopita kupinga hatua ya jeshi kumng'oa rais huyo anayezingatia itikadi za kiislamu.
Hali ya hatari imetangazwa na amri ya kutotoka nje nyakati za usiku kutolewa katika miji mikuu ya Misri.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani John Kerry amesema matukio ''mabaya'' yaliyotokea ni ''pigo kubwa kwa juhudi za maridhiano''.
Afisa wa mashauri ya kigeni katika Muungano wa Ulaya, EU, Catherine Ashton na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kadhalika wamekosoa hatua ya maafisa wa usalama kutumia nguvu dhidi ya raia.
Raia wa Misri wanaamkia siku nyingine yenye shaka juu ya mustakabal wao, anasema mwandishi wa BBC Bethany Bell aliyepo mjini Cairo.
Hata baada ya amri ya kutotoka nje kuondolewa Alhamisi asubuhi, kumekuwa na magari machache katika barabara za katikati mwa Cairo na madaraja yanayovuka mto Nile, anasema mwandishi wetu.
'Pigo kubwa'
Waandamanaji wamekuwa wakiitisha bwana Morsi aliyetimuliwa na jeshi tarehe 3 Julai, kurejeshwa madarakani.
Vuguvugu la undugu wa Kiislamu, Muslim Brotherhood, ambalo lilifadhili maandamano ya hivi punde katika medani ya Nahda na pia karibu na muskiti wa Rabaa al-Adawiya, limesema kuwa idadi ya kweli ya watu waliouwawa siku ya Jumatano inazidi 2,000.
Kwa mujibu wa serikali ya mpito inayoungwa mkono na jeshi, raia 235 waliuwawa kote nchini, pamoja na maafisa wa polisi 43. Tarakimu hizi haziwezi kuthibitishwa kwa njia iliyo huru.
Bwana Kerry amesema juhudi za maridhiano ya kisiasa nchini Misri zimepata "pigo kubwa".
"Hii ni hatua muhimu kwa Wamisri wote," akaongeza bwana Kerry. " Mkondo wa vurugu utaelekea tu kwa msukosuko zaidi, mkasa wa kiuchumi na mateso."
Afisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon imesema kuwa ''anasikitika kwamba maafisa wa Misri waliamua kutumia mabavu wakati Wamisri wengi wanataka taifa lao kusonga mbele kwa amani katika mfumo utakaoongozwa na Wamisri wenyewe ili kuafikia maendeleo na demokrasia".
"Akilaani vikali" vurugu zilitokea Bi. Ashton amesema kuwa " ni juhudi za pamoja pekee kati ya Wamisri wote pamoja na jamii ya kimataifa ndizo zitakazorejesha taifa hilo katika demokrasia inayowashirikisha wote na kukabili changamoto zinazokabili Misri"
CHANZO:BBC
Wednesday, 14 August 2013
SHIRIKI KUJADILI NA TUMA MAONI YA RASIMU, MABARAZA YA CHADEMA KATIBA MPYA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Mikutano ya hadhara, itakayoanza leo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiongozwa na
timu mbili za viongozi wakuu, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt.
Willibroad Slaa.
Mikutano hiyo itafanyika nchi nzima. Ratiba ya mikutano yote, itatolewa kwa umma,
kupitia vyombo vya habari (mainstream & social media).
2. Kutuma ujumbe mfupi kwa simu. Mwananchi anaweza kutuma maoni yake ya Katiba
Mpya kupitia simu ya mkononi, kwenye NAMBA HII YA SIMU; 0789 24 82 24.
3. Email; chademamaoni@gmail.com & chademamaoni@chadema.or.tz
4. Mitandao ya kijamii, mf; Jamii Forums, facebooks, twitter, group emails, k.m mabadiliko,
wanabidii n.k, utaratibu wake utatolewa kwa umma, kupitia vyombo vya habari, ikiwa ni
pamoja na kuwekwa hapa, namna ambavyo Watanzania wote watashiriki kutoa maoni
yao kwa njia hii.
Tumaini Makene
CHADEMA Senior Information(Press) Officer
0752 691569/ 0688 595831
CHIDI BENZ ASIMULIA JINSI ALIVYOTHIRIWA NA BANGI NA MADAWA YA KULEVYA..
Rapper Chidi Benz leo kwa mdomo wake mwenyewe amekiri kuwa alikuwa
akitumia madawa ya kulevya kwa miaka mingi. Chidi amefunguka leo kwenye
kipindi cha XXL cha Clouds FM.Alisema japo hakwenda Nairobi kwaajili ya rehab, mazingira
yalimlazimu kutafuta tiba ili aondokane na madhara ya madawa hayo.
Alieleza kuwa alipofika jijini Nairobi alikuwa akitakiwa kufanya show
nyingi na mwandaaji alimuuliza kama kuna kitu atahitaji ili awezE
kufanya show vizuri.
“Nikamwambia Yeah kuna vitu ntavihitaji,” alisema Chidi. “Nikamwambia
‘mimi bana kuna vitu ninavyovitumia nikikaa 20 minutes bila hivyo vitu
ni noma nachanganyikiwa na akili tena sina, kwahiyo sijui tutafanyaje’.
Akaniambia ‘mimi ntapataje hivyo vitu Chidi na Nairobi ni gharama sana.
Nikamwambia ‘mimi pia nina wazo jingine kuna mtu alinitonya kwamba kuna
kitu kinaweza kikafanyika na pesa Fulani, pesa nyingi kama milioni 15,
16 hivi za kibongo.
Akaniambia kikifanyika hicho maanake vinavyofolewa kabisa hivyo vitu
vilivyokuwa vinanifanya niwe hivyo. Akaniambia ‘hiyo naijua lakini ni
process, ndio maana dunia nzima haifanyi’. Nikamwambia ‘mimi nafanya
kwasababu nilishakutwa na vitu vingi mimi ntafanya.”
Chidi anasema hela hiyo ilipatakana na wakapanga kwenda kufanya mchakato huo wa kuonana na daktari ili kutibiwa.
“Kwahiyo mimi sijaenda rehab na wala sijanywa zile methodone sijui watu wanasema watu wanywe methodone.”
Amesema dawa aliyotumia inanunuliwa na mtu huchomwa kama mgonjwa wa kawaida.
“Yenyewe inakusafisha wewe pale ambapo ulikuwa ukivuta inakukaa then
baada ya dakika kadhaa pakikauka panakuwa pakavu ni kama ile sehemu
inakuwa mbichi wewe ukivuta. Huna hela lakini huvuti panakuwa pakavu,
pakikauka ndio unachanganyikiwa unaanza sasa kuona alosto lakini kama
ukiendelea kuvuta panakuwa pabichi unaendelea.
So yenyewe inaenda kama
mapovu, ni kama sabuni inaenda inakusafisha pale kote panabaki empty.
Kwahiyo ni wewe sasa uamue tena kuvuta tena au uache kabisa. Lakini mimi
nilienda kusafishwa pote, inakuweka unakuwa na power, inakupa akili,
uso rangi, mwili unaanza kubadilika.”
Anasema kabla ya kupata tiba hiyo alitakuwa kusaini karatasi kadhaa kuthibitisha kuwa amekubali kupewa dozi.
“Mama yangu pia alikuwa anajua, nilimwambia kwamba mimi bana inabidi nitibiwe.”
“Niko fresh, niko healthy, nakula vizuri, naishi vizuri, nafikiria
vizuri na nimecalm down,” alisema Chidi kuelezea hali yake ya sasa.
Chidi amekiri kuwa alianza kutumia madawa ya kulevya muda miaka mingi
iliyopita lakini ilikuwa ngumu wengi kujua kwasababu alikuwa akiutunza
vizuri mwili wake.
“Naoga vizuri, nakula vizuri, nafanya mazoezi daily, gym daily,
kwahiyo hata nikivuta hayanitibui kitu lakini yalikuwa yananijaza tu
anger ndani, chuki na ule unoma unoma.”
Tamko la CCM kufuatia mgogoro wa madiwani Bukoba (kuhusu utaratibu)
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika
kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi
wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane
wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.
Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye
vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya
Mkoa sio wa mwisho. Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.
Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa
kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini
Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa
Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.
Pamoja na hilo, tumepokea barua za Madiwani hao za kukata rufaa kupinga
uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa
kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.
Tunawasihi wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote
kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na
vikao vya Kitaifa.
Imetolewa na:-
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
14/08/2013
Sakata ya ugaidi dhidi ya CHADEMA: Shibuda, Sofia Simba watajwa
Katika
ile sakata ya kesi ya ugadi dhidi ya makada wa CHADEMA iliyofutwa hivi
karibuni mkoani Tabora, mbunge wa CHADEMA Maswa Magharibi atajwa
hadharani. Kwa habari kamili soma hapa chini.
Mapya yaibuka
• Makachero wahaha kuwaingiza Dk. Slaa, Mbowe matatani, wakwama
Na Mwandishi wetu
IMEBAINIKA kuwa
baadhi ya maofisa wa polisi na makachero wao wamekuwa wanatumia vibaya
majina ya viongozi wakuu wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama
kisingizio cha kupika kesi za ugaidi dhidi ya viongozi wakuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katika tukio la hivi karibuni, makada wa CHADEMA waliokuwa rumande
wakikabiliwa na mashitaka ya ugaidi, ambayo hatimaye yalifutwa na
mahakama, wametoboa siri kuwa miongoni mwa majina yaliyotumiwa na baadhi
ya polisi na makachero waliowatesa ni ya Rais Jakaya Kikwete; na Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wiki hii, makada hao -
Evodius Justinian, Oscar Kaijage, Rajabu Kihawa, Seif Magesa na Henry
Kileo, wamesema pia kuwa njama hizo za polisi na makachero wao,
zililenga kuwalazimisha vijana hao wawahusishe viongozi wakuu wa CHADEMA
(hasa Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa) na
ugaidi na utesaji watu ambao umekuwa unaendelea.
Wengine ambao polisi walitaka watajwe ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Hata hivyo, vijana hao wanasema waligoma kuwahusisha, hata baada ya kuteswa kikatili.
Makada hao wanadai kwamba mateso waliyopata yaliratibiwa na viongozi wa Jeshi la Polisi, Advocate Nyombi na afande Pasua.
Mmoja wa makada hao, Kihawa, aliyekamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi
Dodoma, anadai kuwa alipokuwa anahojiwa, alilazimishwa aseme kuwa
viongozi wa CHADEMA ndio wanahusika na utekaji na tindikali.
Akiendelea kusimulia mkasa huo, Kihawa alisema kuwa baada ya kauli hiyo,
aliingizwa katika chumba namba 114, ghorofa ya pili, chenye kamera
nyingi katika moja ya hoteli maarufu Mjini Dodoma (jina tunalihifadhi
kwa sasa) akavuliwa nguo zote, akakalishwa kwenye chupa ya soda kisha
akapigwa sana.
“Nilipoteza fahamu lakini nilipozinduka nilikuta nimevalishwa nguo, na
nimekalishwa kwenye kiti na kuwekewa chakula karibu,” anasema, na
kuongeza kuwa hakula chakula hicho, lakini alipotoka nje ya chumba
hicho, kwenye ukumbi wa hoteli, aliwakuta vijana waliofukuzwa CHADEMA, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba na Habib Mchange wakinywa na kula.
“Walinikejeli sana, wakasema wanashangilia ushindi,” alisema.
Kutoka pale nilichukuliwa na Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda,
akaniingiza chumbani akadai anampigia simu Waziri Simba, akamwambia,
“mama, huyu kijana ninaye hapa. Ungeongea naye ili akubali kulegeza
msimamo, au umpigie mwanao Jakaya anipigie, pengine atabadili msimamo
wake kama tulivyokuwa tumekubaliana awali.”
Kihawa anadai kuwa mtu huyo aliyedaiwa kuwa Waziri Simba alimjibu
Shibuda kuwa asingeweza kuzungumza yeye kwa kuwa alikuwa hajisikii vema,
ila kwa suala la kuongea na Rais Kikwete, atafutwe Katibu Mkuu wa chama
hicho, Abdulrahman Kinana au Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwigulu Nchemba,
ili awaunganishe Shibuda na rais.
Kwa mujibu wa Kihawa, baada ya kupewa ushauri huo, Shibuda alijibu:
“Mwigulu ni mropokaji, hawezi kuingizwa katika mkakati huu; na Kinana ni
mgumu kuingilika katika suala hili.”
Anasema alisikia mazungumzo yao kwenye loud speaker ya simu ya Shibuda,
na baada ya kukata simu Shibuda alimwambia kuwa alikuwa anazungumza na
Simba, ambaye alidai ni ‘mama mdogo wa Kikwete.’
Kihawa anasema wakati anahojiwa hayo hapo hotelini, maofisa wa polisi walisimama kwa mbali wakimsubiri.
Wengine waliokuwapo wakishuhudia mahojiano hayo ni Meya wa Ilemela,
Henry Matata na aliyekuwa Diwani wa Igoma, Adam Chagulani. Matata na
Chagulani walishavuliwa uanachama na CHADEMA.
Wahusika walipohojiwa na Tanzania Daima jana, kila mmoja alikuwa na kauli yake kama ifuatavyo:
Tanzania Daima Jumapili: Afande Nyombi, vijana waliokuwa wametuhumiwa
kwa kesi ya ugaidi kule Tabora, wamekutaja wewe kuwa ulishiriki kuwatesa
ukiwalazimisha wawataje viongozi wakuu wa CHADEMA kuwa walishiriki
kutenda ugaidi na utekaji. Unatoa ufafanuzi gani?
Advocate Nyombi: Mimi si msemaji wa Jeshi la Polisi, siwezi kusema chochote.
Tanzania Daima Jumapili: Msemaji atajuaje kama mliwatesa watu wakati wa
mahojiano? Mbona huku ni kumwonea msemaji wa Jeshi la Polisi kusemea
kila kitu hata mambo ambayo askari fulani ametenda kwa utashi wake?
Advocate Nyombi: Nimekwambia mtafute, msemaji katika hayo yote. Mimi siwezi kuongelea suala hilo, nakutakia Idd Mubaraka njema.
Tanzania Daima Jumapili: Afande Pasua, vijana waliotuhumiwa katika kesi
ya ugaidi kule Tabora wamekutaja wewe kuwa ulishiriki kuwatesa,
ukiwalazimisha wataje viongozi wa CHADEMA kuwa walishiriki kutenda
ugaidi na utekaji. Unatoa ufafanuzi gani?
Afande Pasua: Kwani wewe uko wapi?
Tanzania Daima Jumapili: Nipo Dar es Salaam, hapa ofisini.
Afande Pasua: Njoo ofisini tuongee tuyaweke sawa unayouliza. Umesema unatoka gazeti gani?
Tanzania Daima Jumapili: Nimekwambia Tanzania Daima.
Afande Pasua: Mashtaka hayo kwanza yalikuwa ya serikali, mimi sifanyi
kazi ya kubahatisha, mpigie msemaji wa Jeshi la Polisi mimi si msemaji.
Alikata simu.
Henry Matata
Tanzania Daima Jumapili: Mstahiki Meya, vijana waliokuwa wanakabiliwa na
kesi ya ugaidi wanadai walihojiwa mbele yako Dodoma. Je, unafahamu nini
kuhusu suala hili?
Matata: Kijana Rajab Kihawa ndio namfahamu. Huyu alikuwa mfanyakazi
wangu, ila tangu aache kufanya kazi hapa sijaonana naye. Lakini mimi
nina ugomvi na wafanyakazi wote wa gazeti lenu na gazeti lenu.
Nisingependa kuongea na nyie. Tangu nifukuzwe CHADEMA gazeti lenu
linaongeza chumvi habari zinazonihusu. Mimi si meya kwa kura za CHADEMA.
CHADEMA walinifukuza, CCM wakaona nafaa, wakanipa kura nikawa meya.
Tanzania Daima Jumapili: Ulikutana na Rajab Dodoma hotelini?
Matata: Nimekwambia sitaki kuongea na gazeti lenu.
bi Mheshimiwa, vijana waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi
wamekutaja kuwa ulikuwepo wakati wanahojiwa Dodoma. Je, una kauli gani
kwa yao hii?
Chagulani: Mimi nilikuwa Dodoma mwezi wa nne lakini nilikuwa Kondoa kwa
ajili ya uhamisho wa mke wangu. Hayo unayonieleza siyajui.
Waziri Simba hakupokea simu, na alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu lolote.
Msemaji wa jeshi la Polisi, Advera Senso, alipoulizwa kama jeshi ndilo
linawatuma polisi kutesa watu wakati linawahoji, alisema: “Mhalifu
asitafute huruma ya jamii kwa kuzushia jeshi kwa uhalifu alioutenda
yeye, na endapo ikibainika anasingizia uongo na hilo ni kosa pia, kwani
Jeshi la Polisi linafuata taratibu za sheria.”
Shibuda alipoulizwa jinsi alivyohusika katika sakata hilo alisema kuwa
kwa sasa hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa alikuwa Agha Khan Hospitali
akihangaikia mgonjwa wake.
“Niacheni kwa sasa kwa kuwa nahitaji utulivu wa akili niweze
kushughulikia afya ya mgonjwa wangu. Nadhani hata kama ni wewe sijui
katika mazingira kama haya ungeweza kweli kuongea?” alisema.
Msemaji wa Ikulu, Salva Rweyemamu, alipopigiwa simu kuulizwa ikiwa
wanayo taarifa ya watu wanaotumia vibaya jina la rais katika matukio ya
kihalifu aliomba jambo lolote linalohusiana na kazi, lisubiri kwa kuwa
alikuwa katika mapumziko ya sikukuu.
“Ndugu yangu, unajua leo ni sikukuu na ni usiku, nitafute wakati
mwingine, maana siwezi kuzungumzia mambo ya watu wa CHADEMA muda huu.
Niache nipumzike kidogo halafu tuwasiliane siku ya kazi,” alisema.
Source: Tanzania Daima
"NITAENDELEA KUTETEA HAKI ZA WAISLAMU NA SITARUDI NYUMA NA RISASI ZAO
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda amesema alichanganyikiwa kiasi cha kushindwa kujielewa
kwa muda baada ya kupigwa risasi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi kwenye wodi binafsi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) alikolazwa jana, Sheikh Ponda alisema kutokana na hali hiyo hakumbuki matukio yaliyofuata baada ya hapo.
“Sikumbuki hata nilipata huduma ya kwanza hospitali gani kwa sababu sikuwa katika hali ya kawaida. Mambo mengine yaliyotendeka kabla ya kujeruhiwa ninayakumbuka vizuri,” alisema Ponda ambaye inasadikiwa kwamba alipigwa risasi ya begani, Ijumaa iliyopita mjini Morogoro.
Alisema alihutubia katika Kongamano la Waislamu kwa muda mfupi akizingatia muda uliokuwa umetolewa kumaliza mkutano huo na baada ya hapo alishuka na kupanda kwenye gari binafsi ambalo lilizingirwa na polisi ndipo akaamua kushuka na kuanza kutembea kabla ya kujeruhiwa.
Mahojiano maalumu na Sheikh Ponda
Swali: Je, watu waliokupa huduma ya kwanza mara baada ya kujeruhiwa walikuta risasi iliyokujeruhi?
Jibu: Nilipigwa risasi kwa nyuma ikatokea mbele kwa hiyo haikubaki mwilini wala haikuonekana ilipoangukia kwa wakati huo maana kulikuwa na purukushani.
Swali: Ulipata wapi huduma ya kwanza?
Jibu: Kwa kweli kwa sasa siwezi kukumbuka nilihudumiwa wapi kwa sababu mara baada ya kujeruhiwa sikuwa katika hali yangu ya kawaida, nilichanganyikiwa.
Swali: Utathibitisha vipi kama ulipigwa risasi?
Jibu: Bahati nzuri ni kwamba tukio hili lilitokea kweupe wapo wengi walioshuhudia, kwa hiyo wanaweza kusaidia kuthibitisha na ushahidi mwingine ni jeraha hili.
Swali: Nini msimamo wako baada ya tukio?
Jibu: Nitaendelea kuzungumzia haki za Waislamu na siwezi kurudi nyuma. Pamoja na kwamba wananiona mimi ni mtu mchochezi lakini wanaeneza chuki dhidi yangu kwa njia wanazojua wao. Nitaendelea, risasi haitaninyamazisha.
Swali: Umehusishwa kufanya uchochezi Zanzibar, unalizungumzia vipi hilo
Jibu: Zanzibar nilichozungumza ni kuhusu kesi dhidi ya viongozi wa Kundi la Uamsho. Watu wamewekwa ndani kwa miezi tisa sasa, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, kesi wanayoshtakiwa ina dhamana, sasa nikauliza kwa hao viongozi, kwa nini hawazingatii sheria?
Kesi zina muda mrefu hazitolewi uamuzi, nikawasisitiza wazingatie misingi ya sheria kwa kuwa hivyo wanavyowatendea wananchi wajue kwamba hawastahili kupewa tena ridhaa ya kuongoza nchi, nilifikisha ujumbe wangu.
Swali: Kuna tukio la kumwagiwa tindikali mabinti wawili wa Uingereza lililotokea Zanzibar, ambalo wewe pia unahusishwa, hili unalizungumziaje?
Jibu: Sijaona huo ushahidi ambao wanahangaika kunihusisha na tukio hilo, nahusishwa vipi? Matukio ya kumwagiwa tindikali yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara huko kabla sijakwenda kuhutubia. Vyombo vya dola vifanye kazi yake vyema ili kubaini ukweli wa jambo hili.
Pia Mwananchi ilizungumza na mke wake, Sheikh Ponda, Hadija Ahmad ambaye alikuwa ameketi pembeni ya kitanda alicholazwa mumewe.
Swali: Unazungumziaje tukio hili la kujeruhiwa kwa mumeo?
Jibu: Hili ni dhumuni la Serikali, lililenga moja kwa moja kumdhuru ili kunyamazisha harakati zake za kutetea wanyonge. Ni tukio la kupangwa, halijatokea bahati mbaya. Serikali inamfuatilia sana hivyo ililenga kumnyamazisha.
Namshauri Rais (Jakaya Kikwete), kuhakikisha kwamba haki za wanyonge zinawafikia, asije akafikiri hili lililotokea kwa Sheikh Ponda ni suluhisho, ni vyema kufanya mazungumzo ili kuweka mabadiliko.
Alivyowaponyoka polisi
Mtu wa karibu wa Sheikh Ponda alisimulia jinsi walivyomsafisha kiongozi huyo kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam na kukwepa vizuizi vya polisi ambao walikuwa wakiendelea kumsaka.
“Msafara ulikuwa na magari mawili. Moja lilitumika kwa uangalizi, lingine lilimbeba Sheikh Ponda. Tulipofika Chalinze tulikuta kizuizi tukakikwepa kwa kupitia Msata kisha Bagamoyo hadi Dar es Salaam na kumfikisha Muhimbili,” alisema.
Waigomea polisi
Msemaji wa familia ya Sheikh huyo, Isihaka Rashid alisema hawaitambui tume iliyoundwa na polisi kwa kuwa jeshi hilo ndilo linalotuhumiwa.
“Tunachofanya hivi sasa ni kukusanya ushahidi wetu, kwa bahati nzuri tayari tumepata mkanda wa tukio lenyewe ambao utatuwezesha kumbaini aliyemshambulia Sheikh Ponda.
“Hatuwezi kuhitaji majibu ya hiyo tume yao na hata leo kuna maofisa wa polisi kutoka Makao Makuu na Kituo cha Kati, Dar es Salaam walifika wakitaka kumhoji eti kuhusu uchochezi lakini alikataa kuzungumza hadi mwanasheria wake awepo, wakaondoka,” alisema Rashid.
Mwananchi
CCM YAFUKUZA MADIWANI 8 BUKOBA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera, leo kimewafukuza madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kupitia chama hicho na kufutwa nyadhifa zao za udiwani kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea
Waliofukuzwa ni:
- Richard Gaspar (Miembeni )
- Murungi Kichwabuta (Viti maalum)
- Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)
- Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)
- Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)
- Robert Katunzi (Hamugembe)
- Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na
- Dauda Kalumuna (Ijuganyondo)
Tuesday, 13 August 2013
Gay clergy don't belong in Anglican church, archbishop says
Archbishop Stanley Ntagali, the Church of Uganda supremo, has finally broken his silence on gay clergymen: they don’t belong in the Anglican faith.
Speaking at a press conference at his residence on Namirembe Hill on Tuesday, Archbishop Ntagali said the idea of having gay bishops is an ‘unbiblical decision’ and a ‘spiritual cancer’ in the Anglican faith.
The remarks come ten years after the first gay bishop, Gene Robinson, was consecrated in the Diocese of New Hampshire, in the United States. Bishop Robinson’s consecrated caused a rift in the global Anglican faith, which Archbishop Ntagali calls tearing the fabric of the Anglican Communion at its deepest level.
Ntagali, the former Masindi Kitara Diocesan bishop, was installed as archbishop in December last year.
The archbishop said the Anglican Church is built on the doctrines of Biblical teaching which only recognize hetero-sexual relationships.
The Ugandan Anglican community takes exception of the decision by the England House of Bishops to allow gay bishops as part of the Anglican clergy, he said, and thus will have a Global Anglican Future Conference in Nairobi, Kenya this October to resolve the issues.
The Global Anglican Future Conference (Gafcon) will be the second of its kind that brings together Archbishops around the world who oppose gay bishops. In 2008, the anti-gay Anglican Church leaders gathered in Jerusalem, Israel to reflect on the future of the church.
Archbishop Ntagali, with these remarks, is picking off from where his predecessor left off: Henry Luke Orombi was one of the main organizers of Gafcon 2008, and also made several pastoral trips to several countries to preach against gay clergy and gay marriage.
SOURCE:Daily Monitor
Dk Ndalichako ‘achanachana
Arusha: Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Nchini (Necta), Dk Joyce Ndalichako amesema karatasi za majibu ambazo wamekuwa wakizipata kutoka kwa wanafunzi zinaonyesha kuwa, watoto wengi wanahudhuria shuleni lakini hakuna wanachojifunza.
P.T
Dk Ndalichako aliyasema hayo jana jijini hapa alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa mabaraza ya mitihani ya Afrika, ambao umejikita kujadili suala la tathimini ya elimu kwa nchi za Afrika.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Ndalichako kuzungumza tangu Serikali itangaze kufuta matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 na kutaka yapangwe upya, suala ambalo lilipingwa na wadau wengi wa elimu.
Alisema kuwa wakati nchi nyingi za bara hili zikiwa zimejitahidi kuongeza upatikanaji wa elimu kwa watu, ubora wa elimu unaendelea kuwa tishio kwa watu wa bara hili kwa vizazi vijavyo.
"Kama mabaraza ya mitihani, tumekuwa tukiona karatasi za majibu kutoka kwa wanafunzi ambazo zinaonyesha kwa uwazi kabisa kuwa watoto wanahudhuria shuleni lakini hakuna wanachojifunza," alisema Dk Ndalichako.
Kwa upande wake Profesa Justinian Galabawa, alisema ili kuendeleza elimu, lazima uamuzi wa kitaalamu usiingiliwe na siasa kwa namna yoyote ile.
Alitolea mfano kitendo cha Serikali kufuta matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2012 akisema hakikuwa sahihi hata kidogo.
Alisema lazima vyombo vilivyopewa mamlaka kisheria kama Necta viachwe vifanye kazi bila kuingiliwa kwani kufanya hivyo kutaporomosha elimu.
Alisema pia lazima kuwa na sera ya nchi ya kufanya tathmini ambayo ili ifanye kazi lazima ishirikishe wadau wote na kila anayehusika kuitekeleza awe nayo.
"Jambo la kwanza ni lazima tuheshimu wataalamu na wasiingiliwe na wanasiasa, taasisi zilizoundwa kisheria na kupewa mamlaka ya kupima na kutambua watu ni lazima ziheshimiwe. Kama mtoto amepata daraja la nne huwezi kumpa la kwanza," alisema Profesa Galabawa.
Kwa upande wake, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Seif Ali Iddi alisema mkutano huo ni sehemu nzuri ya Tanzania kujifunza kutoka kwenye nchi nyingine kujua ni nini watu wengine wanafanya.
Alisema uzoefu utakaopatikana kutokana na mkutano huu utasaidia katika kujipima na kuendeleza elimu nchini.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo, Philipo Mulugo alisema kwa siku ya kwanza tu wamebaini kuwa zaidi ya asilimia 80 ya nchi za Afrika tayari wanatumia mfumo wa usahihishaji kwa kutumia mashine maalumu (OMR) ambao bado baadhi ya watu nchini wanaulalamikia.
Alisema baadhi ya nchi sasa wameanza kusahihisha kwa kutumia kompyuta hata maswali ya kujieleza, hivyo akawataka Watanzania waache kujirudisha nyuma.
P.T
chanzo: mwananchi
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza dau la Sh100 milioni kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwahusika wa tindikali
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza dau la Sh100 milioni kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia maji baadhi ya watu yanayodhaniwa ni tindikali.
Hatua hiyo inatokana na vitendo hivyo kushamiri maeneo mbalimbali nchini.
Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema vitendo hivyo havipaswi kuvumiliwa na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu hao.
“Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa,” alisema Kova.
Hivi karibuni Mkurungezi wa Maduka ya Home Shopping Center, Mfanyabiashara wa Lebonon na raia wawili wa Uingereza walimwagiwa maji yanayodhaniwa ni tindikali.
Mbeya wataka Z’bar iwe mkoa
Kyela. Imependekezwa kuwa Katiba Mpya itamke kuwepo kwa muundo wa Serikali moja ili kuweza kuulinda Muungano na kuondoa migogoro na migongano ya kimaslahi katika mgawanyo wa rasilimali.
Mapendekezo hayo yametolewa na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya waliokuwa wakijadili ibara ya 57 iliyohusu muundo wa muungano.
Diwani wa Kata ya Ngonga, Kileo Kamomenga alisema muundo wa Serikali mbili au tatu ni hatari, kwani unahatarisha Muungano na pia unatoa mwanya kwa Serikali moja kufanya uhusianona nchi nyingine ambazo hazitakuwa na nia njema na Watanzania .
“Kwa mfano katika ibara 62 kifungu kidogo cha (2) kinatoa uhuru kwa kila mshirika wa Muungano kuwa na uwezo wa kuanzisha uhusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kitu ambacho mimi naona ni hatari kwa taifa letu, ni vema tukawa na Serikali moja, Zanzibar iwe ni moja ya mikoa ya Serikali moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”alisema
Alisema kitendo cha Zanzibar kuwa na bendera yake, wimbo wake wa Taifa, Rais wake ni kuifanya kuwa nayo ni nchi inayojitegea na watu wake kujiita wao ni Wazanzibari na siyo Watanzania “Hivyo kama tuna lengo la kudumisha Muungano ni lazima tuwe na Serikali moja kuliko ilivyo hivi sasa,”alisema
Naye mjumbe, Clifford Mwaikinda alisema kuwa muundo wa Serikali moja utapunguza kubeba nzigo mkubwa kiuchumi na madaraka na kuwepo kwa usawa katika kugawanya rasilimali za nchi na kuondoa upendeleo kwa Serikali ya Zanzibar ambayo ilikuwa inanufaika na mambo mengi kutoka Tanganyika.
CHANZO:Mwananchi
NGOMA AFRICA BAND
Mzimu wa Dansi "Ngoma Africa Band umetimiza miaka 20 na bado unatisha!
Mabalozi wa kiafrika nchini Ujerumani wamewapongeza FFU wa Ngoma Africa Band kwa kuchukua tena International Diaspora Award 2013 Bendi bora ya Kiafrika Ulaya.
Ngoma Africa Band ilifanikiwa kuutetea ubingwa wake wa bendi bora na kujichukulia Tuzo ya kimataifa ya IDA mjini Tubingen, Ujerumani katika maonyesho ya kimataifa ya International African Festival Tubingen 2013.
TAARIFA YA CUF KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA KAULI YA KOVA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia
tamko la Kamanda wa Kanda Maalum wa Mkoa wa Dar es Salaam la kutoa onyo
kwa Waislam na kusema kwamba wanamshikilia Sheikh Ponda kwa tuhuma
mbili za, kwanza, kutokana na tukio la Morogoro na, pili, kukiuka
masharti ya kifungo cha nje alichohukumiwa mwanzoni mwa mwaka huu, CUF –
Chama cha Wananchi kinatafsiri tamko hili kama muendelezo wa kile
kinachoonekana kuwa ni hujuma dhidi ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Hatuoni
sababu ya Kamanda Suleiman Kova kutoa onyo kwa Waislamu kwa jambo
ambalo Waislamu wameshatoa tamko kupitia Amiri wao, Sheikh Mussa
Kundecha, na kuiomba serikali kuunda tume huru ya kuchunguza tukio hilo.
Tangu
litolewe tamko hilo, hakuna Muislamu yoyote aliyefanya jaribio lolote
la kutaka kulipa kisasi kwa polisi au kwa mtendaji yoyote wa serikali.
Sasa kuna haja gani ya kutoa onyo kwa jambo ambalo Waislamu
wameshakubali maelekezo ya viongozi wao?
Pili, kutangaza
kumshikilia Sheikh Ponda akiwa hospitalini, ambako anapatiwa matibabu,
kwa kisingizio au kwa tuhuma za tukio la Morogoro au kukiuka masharti ya
kifungo cha nje ni hoja zisizo na mashiko.
Juu ya suala la Morogoro, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi imeunda tume ya kuchunguza tukio hilo, na tayari
tume hiyo imeshaanza kazi ya kukusanya taarifa kwa watu mbalimbali mjini Morogoro.
Sasa wewe Kamanda wa Kanda Maalum unahusikaje kwenye jambo hilo la Morogoro? Au umepewa maagizo ya kumkamata Ponda na Tume iliyoundwa toka Makao Makuu?
Iwapo umepewa amri, je Tume hiyo imeshakabidhi ripoti yake kwa IGP Saidi Mwema na imependekeza Ponda akamatwe kwa tukio hilo kwamba yeye ndiye muhusika alimpiga risasi Sheikh Ponda? (Hapa nina maana amejipiga risasi mwenyewe?). Hivi Kova ni Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu?
Suala la kukiuka masharti ya kifungo cha nje, hivi Kova unayafahamu hayo masharti na umepata agizo lolote toka kwa Hakimu au Mahakama ilimuhukumu Sheikh Ponda, kwamba umkamate kwa kuwa amekiuka masharti?
Maswali yote haya yanakupa majibu na mtazamo sahihi kwamba Kova unafanya kazi ya kumuhujumu Rais.
CUF – Chama cha Wananchi kinaitafsiri kauli ya Kamanda Kova kama imelenga kutoboa jahazi lililobeba hasira za Waislamu katika suala hili la kupigwa risasi Sheikh Ponda.
Kauli hii inapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote. CUF -Chama cha Wananchi kinamshauri Kamanda Kova kwa sio lazima kujibu kila jambo unaloulizwa na waandishi wa habari, na ikiwa lazima kujibu, basi upime kile unachojibu kwa maslahi ya nchi na usijibu tu kwa maslahi yako.
Mwisho kabisa CUF – Chama cha Wananchi kinamtaka IGP Saidi Mwema kutoa ufafanuzi juu ya kauli tata za Kamanda Kova.
Imetolewa na:
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Sheria na Uenezi, CUF
Tanzania ya enzi hizo
kituo cha Mabasi ya Ekarusi Kumbakumba kwa nyuma Azania Front
Subscribe to:
Posts (Atom)