Mbunge wa Kinondoni-CCM, Iddi Azan
Mbunge
Wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania kutoka jimbo la
Kinondoni, inasemekana ametajwa na wafungwa wa kitanzania waliofungwa
jela huko nchini Hong Kong kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Taarifa
hiyo iliyomhusisha Mbunge huyo na mtandao huo mkubwa wa biashara hiyo
ya madawa ya kulevya nchini Tanzania, ilitolewa katika barua maalum
iliyoandikwa na mmoja wa Wafungwa katika magereza ya nchini Hong Kong
ambapo inasemekana kuna wafungwa wa kitanzania wanaofikia 200.
Kati
ya hao wafungwa 200 waliopo magerezani na vizuizini, 130 tayari
wameshahukumiwa na 70 bado wanasubiri kesi zao kutajwa. Kuanzia Mwezi wa
Tano mpaka wa Sita mwaka huu wa 2013, tayari Watanzania wapatao 50
wameshakamatwa na madawa ya kulevya wakati wakijaribu kuingia katika
viwanja vya ndege vya nchi za China na Hong Kong.
Mbali
na Hong Kong, pia kumekuwepo na taarifa mbalimbali za raia wa Tanzania
ambao wamekatwa na madawa ya kulevya nchini Afrika ya Kusini na
kwingineko duniani. Mmoja kati ya waliokamatwa na madawa hayo ni
mwanadada mahiri wa Kitanzania ambaye alikuwa mrembo katika video
mbalimbali za Bongo Flava anayeitwa Agnes Gerald au kama anavyojulikana
na wengi kwa jina la Masogange.
Waraka
huo wa mfungwa huyo wa Kitanzania pia umeorodhesha idadi kubwa ya
wafanyabiashara wengine nchini Tanzania ambao ni wahusika wakubwa katika
biashara hii haramu ya madawa ya kulevya.
Madawa
hayo ya kulevya yanasemekana yanaingizwa nchini Tanzania kwa wingi kwa
njia ya meli na boti mbalimbali yakitokea katika nchi za Pakistan,
Afghanistan na nchi nyingine za Mashariki ya mbali.
Ni
muhimu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha
kampeni kubwa ya kuwakamata wahusika wote katika biashara hii na
kuwafikisha katika vyombo vya sheria, athari za madawa hayo zimezidi
kuonekana sehemu mbalimbali nchini Tanzania na dunia nzima.
Soma barua iliyowataja wafanyabiasha hao wakubwa wa madawa ya kulevya nchini Tanzania hapo chini.
SOURCE:Bongo celebrity
No comments:
Post a Comment