CUF TUNASHANGAZWA NA JINSI SERIKALI INAVYOSHINDWA KULICHUKULIA HATUA
GAZETI LA TANZANIA DAIMA KWA KUENDELEZA UCHOCHEZI WA KIDINI.
CUF-Chama cha Wananchi, kinasikitishwa sana na kitendo cha uchochezi wa
Kidini unaofanywa na Gazeti la Tanzania Daima chini ya Muandishi George
Maziku, kufuatia habari iliondikwa leo Tarehe 18/07/2013 toleo na 3149 .
Aina hii ya uchochezi na Chuki ya Kidini anayoiendeleza bw, Maziku
chini ya usimamizi wa Mmiliki wa Gazeti la Tanzania Daima na Mhariri
wake, kwa maslahi ya Kisiasa tu, yatatupeleka mahala pabaya sana kama
Taifa. CUF-Chama cha Chama Wananchi tunashangazwa na tuna hoji juu ya lengo na Dhamira ya Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake nini juu ya muendelezo wa habari wanayoitoa kwa muda wa miezi miwili sasa ? Habari hii ina lenga nini ? Kwamba Viongozi wa Kisiasa wanaotokana na Dini ya Kiislam hapaswi kujumuika na Waislam wenzao kwenye Nyumba za Ibada ? Au waislam hawapaswi kujadili Maendeleo ya Taifa lao ?
CUF-Chama cha Wananchi tunaona Lengo la Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake ni kupandisha hasira za Waislam kwa mtazamo wa Ubaguzi wa Kidini kupitia tasnia ya Habari na hivyo kuleta machafuko yasiokuwa ya lazima.
Hata hivyo ikiwa lengo ni kuondosha Dalili za Udini kwenye mambo ya Siasa, hivi Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake hawakuona Waraka wa Uchaguzi wa Mwaka 2010 uliotolewa na Kanisa Katoliki na kupewa jina la IIani ya Uchaguzi wa Kanisa Katoliki ? Waraka ambao uliwataka Wakristo kuichagua Chadema na wagombea wake, Sio hivyo tu Waraka huo ulikwenda mbali zaidi na kuwatahadharisha Wakristo wasichague CUF na CCM na kuvifananisha Vyama vya CUF na CCM ni sawa na Chui waliovaa Ngozi ya Kondoo kwa Kanisa.
Waraka huo ulipingwa vikali sana na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru. Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake walikuwa wapi ? Mbona hatukuona waandike KANISA LA CHOCHEA UDINI ? Kama hiyo haitoshi, hivi Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake mbona hawakumkemea wala kuandika kuhusu Askofu Kakobe alipokua anampigia debe Mgombea wa Urais kupitia Chadema 2010 tendo ambalo lilikuwa linaonyeshwa wazi wazi kupitia Star Tv.
Kama hiyo haitoshi katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika jijini Arusha na Chadema kushinda wafuasi na viongozi wake kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kuwa YESU AMESHINDA hilo nalo hukuliona?
Kama hiyo pia haitoshi ? Mwaka huu Mery Nagu amekwenda kusali Kanisani na kuwataka Wakristo wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya na kuwataka waumini hao wapinge mambo yote yanayotakiwa na kikundi kidogo cha baadhi ya watu kwa maslahi ya Kanisa, je huu haukuwa UDINI ? Lowasa kila kukicha yupo Makanisani na Misikiti na anatoa Fedha anatoa je hilo sio tatizo ?
Kwa mkusanyiko wa hoja zote hizi , CUF –Chama cha Wanainchi kinashindwa kuelewa kwanini Serikali haioni hatari inayofanywa na Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi kwa tendo hili la Uchochezi wa Kidini ? Ikiwa Serikali iliweza kuzifungia Radio Imani na Radio Maria zote zikiwa zinarusha matangazo yake kwa Malengo ya Kuendeleza Dini zao, inashindwaje kulitazama Gazeti hili la Tanzania Daima ? Hivi Serikali inasubiri nini ? mpaka hao Waislam wanaotumiwa kuwa wadini waje juu na kuleta vurugu ? Ni busara kwa Serikali kulitazama jambo hili kabla halijalet madhara.
CUF-Chama cha Wananchi kinaishauri Serikali kulitazama kwa makini jambo hili, kabla halijaleta madhara, uandishi wa aina hii ndio uliosababisha Mauaji ya Kimbali. Uandishi wa Uchochezi unaolenga kuligawa Taifa kwa misingi ya Ukabila au Udini ni uandishi hatari sana kwa Taifa letu.
Bahati mbaya Tanzania Daima hawajui au wamesahau kwamba kwa chuki ya Kidini wanayojitahitahidi kuipandikiza ndani ya Taifa letu kwa nguvu ya Tasnia ya Habari, haitawaacha SALAMA wao kama Gazeti wala Muandishi wa Habari hiyo ya Uchochezi na wanapaswa kutambua kwamba kwa kufanya hivyo tu, basi wanainunua hatari ya Taifa letu kwa gharama kubwa.
Malengo ya Kisiasa yasije kulisambaratisha Taifa letu eti kwa sababu tu Chadema ichukue Nchi. Mnaweza kufikia Lengo la kuchukua Nchi kwa Mtazamo na Mkakati huo wa Kidini, kama ambavyo mnaendlea kufanya, lakini mjue kwamba mtachukua Nchi isokuwa salama. Maana mtakuwa mmeigawa Nchi kwa Matabaka ya Udini.
Kama kweli wewe ni mwandishi mahiri na mpenda amani katika nchi, tafadhali soma kitabu cha KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA KUANZIA MWAKA 1953 HADI 1985 kilichoandikwa na Dr. John C. Sivalon na uje na uchambuzi wa dini uliomo katika kitabu hicho.
CUF- Chama cha Wananchi kinalitaka Gazeti la Tanzania Daima , kuanzia Mmiliki wake, Mhariri wake na Muandishi wa Habari hizi, ambae mara huandika kwa mtindo wa Makala , mara huzipa uzito mkubwa kadri anavyoona inafaa kwa utashi wa Kisiasa au Udini wake, kujitazama upya juu ya hili wanalolitengeneza kama litaiweka Nchi yetu katika eneo salama.
Mwisho CUF-Chama cha Wananchi kinaitaka Serikali kuchukua hatua juu ya Uchochozi huu.
Imetolewa na
Abdul Kambaya, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Haki za Bainaadam na Mahusiano ya Umma
0719 566 567
No comments:
Post a Comment