Wacheza soka Nigeria wapigwa marufuku
Wachezaji na maafisa wa vilabu waliohusishwa na kupanga mechi ambazo
hatimaye zilimalizika kwa mabao 79-0 na 67-0 wamepigwa marufuku maisha
Kilabu cha Plateau United Feeders walishinda mchuano wako kwa mabao
79-0 dhidi ya kilabu cha Akurba FC wakati kilabu cha Police Machine FC
kilipoibwaga Bubayaro FC kwa mabao 67-0.
Vilabu hivyo vimepigwa marufuku kushiriki michauno yoyote kwa miaka 10.
Kamati moja ya Shirikisho la soka la Nigeria
ilipendekeza kuwa maafisa wa soka waliohusika katika upangaji huo wa
michuano miwili kupigwa marufuku maisha.
Plateau United Feeders na Police Machine
waliingia kwenye mechi yao wakiwa na pointi sawa huku wakiwa katika
hatari ya kuvuka na kuingia daraja ya chini ya ligi ya kitaifa ikiwa
wangepoteza mechi .
Feeders ilishinda kwa mabao 72 katika kipindi
cha pili cha mechi, wakati Police Machinen nao wakipata mabao 61 baada
ya kipindi cha mapumziko.
Matokeo hayo yalimaanisha kuwa Plateau ilipanda daraja juu ya Police Machine kwa toafuti ya mabao.
Shirikisho la soka Nigeria limesema kuwa limekubali mapendekezo hayo na kuwa litawasiliana na vilabu husika, pamoja na FIFA.
Shirikisho hilo lilisema litachapisha majina ya wachezaji , picha zao na maelezo kuwahusu.
CHANZO:BBC SPORT
No comments:
Post a Comment