Watanzania wamezoeleka kuwa na ukarimu lakin mwisho wake wanaishia
kunyongwa na wengine kuishia jela kwa kusaidia watu wenye mzigo wa
madawa ya kulevya bila wao kujua.
Nakumbuka niliwai kutana na mnigeria fulani Kuala-Lumpur Intl Airport
akaniomba nimsaidie mzigo eti yuko na mizigo mingi lakini nikakataa huko
mbele akakamatwa na madawa ya kulevya.
Pia watanzania wenzetu wanakamatwa na kunyongwa China baada ya kuwasaidia watu wasiowajua mzigo.
Utakuta ukiwa na mzigo mdogo mtu anakuomba umsaidie kuupitisha sababu
yeye anayo mingi na anaogopa kuchajiwa pesa ya mzigo uliozidi, kumbe
wanakuwa na madawa ukipita salama anakushukuru na hakupi ata sh 10, ila
ukishikwa umuoni.
Hii ipo sana China, Dubai, South Africa, Kuala-Lumpur, Japan Etc.
Ukarimu wa watanzania umesababisha watu kunyongwa na jela kwa miaka mingi.
Hata mtu akiwa mjamzito usimsaidie mzigo, kuna mwanamuzik wa Uganda
Irene Namubiru alikamatwa Japan na madawa akakaa siku 21 jela baada ya
kugundulika alipewa na manager wake na hakuwa anajua yaliwekwa kwenye
ndizi.
Mwenye macho ataona, tafakari chukua hatua!
BY:
Money stunna
No comments:
Post a Comment