Askari akamatwa kwa kudhalilisha maiti
Afisa mmoja wa jeshi la Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo ametiwa nguvuni baada ya kuchafua maiti za wapiganaji wa
waasi nchini humo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
wa DRC, Lambert Mende, ameiambia BBC kwamba Luteni Solomo Bangala alizuiliwa jana
Alhamisi na maafisa wa kijeshi baada ya mapigano kuzuka kati ya jeshi na waasi
wa M23 katika eneo la mashariki karibu na mji wa Goma.
Kukamatwa kwa afisa huyo kunajiri
muda mfupi tu baada ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon kuzungumzia
madai ya kuwepo dhuluma na mateso dhidi ya wafungwa kutoka makundi ya waasi
pamoja na wale waliouwawa zinazotekelezwa na wanajeshi wa Kikongomani.
Kikosi cha kulinda amani cha umoja
wa mataifa kinatathmini upya hatua yake ya kuunga mkono vikosi vya serikali ya
DRC kufuatia shutuma hizo.
Waasi wa M23
Mapigano kati ya jeshi la DRC na
waasi wa M23 yalianza siku ya Jumapili karibu na mji wa Goma.
Mwandishi wa BBC Maud Jullien
aliyepo katika mji wa Goma anasema uwanja wa mapigano ulikuwa takriban kilomita
7 katika vilima kutoka mji huo.
Hapajakuwa na mapigano yoyote katika
kipindi cha siku mbili zilizopita na jeshi limesema limefanikiwa kuwafukuza
waasi yapata kilomita 6, anasema mwandishi wetu.
No comments:
Post a Comment