Uamuzi wa serikali ya Uingereza kupiga marufuku Miraa au Khat baadaye mwaka huu unakabiliwa na upinzani mkali nchini Kenya kutoka kwa wakulima wa mmea huo unaosemekana kulewesha ingawa kwa kiwango kidogo sana.
Huku jua likichimoza mjini Meru, maeneo ya mlima Kenya , wakulima wa Miraa ndipo nao wanaanza kazi.
Wanaume kumi na wawili hivi, baadhi wakionekana kula chuvi nyingi, wanapanda miti kwa uangalifu mkubwa , hii ni biashara inayohitaji uangalifu mkubwa.
Wanataka majani yanayoonekana kuwa machanga kwa hivyo itawabidi kupanda hadi juu kabisa ya mti na lazima waharakishe.
"kazi hii huwa twaifanya asubuhi na mapema , inahitaji kupelekwa sokoni nbaada tu ya kuyachuna,'' anasema Jeff Kubai.
Katika kazi yake ya mchana bwana Kubai
ni prefoesa wa saikolojia.
Lakini kama wengi hapa, yeye hupanda
Miraa au Khat kama yanavyojulikana hapa.
Familia yake imekuwa ikipanda Miraa
kwa miaka mingi.
"ni mmea, ambao unalewesha
kidogo na kumfanya mtu kuwa na furaha isiyo na kifani,'' anasema huku akitafuna
majani hayo.
Miraa lazima ipate kuuzwa haraka
wakati majani yake yakiwa hai.
Lakini katika eneo hili, utafunaji
wa Miraa ni jambo ambalo lina mizizi yake katika tamaduni za Meru.
"Mashujaa zamani walikuwa
wakitafuna Miraa," asema bwana Kubai, "ili kuwaogopesha maadui na pia
kuwalinda mifugo malishoni.''
"Viongozi wa jamii zamani pia
walikuwa wakitafuna Miraa wakati wakijadili mambo yanayohusu jamii.''
Tunahisi uchungu sana na kama
tumesalitiwa. Tunamtaka waziri wa mambo ya ndani Uingereza kubatili uamuzi
wake, aliongeza Kubai''
Utafunaji Miraa umeenea kote Meru,
huku asilimia 80 ya wenyeji wakiwa wanategemea sana biashara ya Miraa kama pato
lao la maisha.
"Hili shamba hunipatia mazao ya
thamani ya dola elfu mbili miatatu ,'' anasema Kubai
"Hizi ndizo pesa nilizotumia
kujenga kanisa, kusaidia watoto mayatima na miundo mbinu mingine na mambo
mengine muhimu.
"Yaani kwa kifupi tu miasha ya
watu hapa yanategemea miti hii.''
Na ndio maana viongozi wengi wa hapa
wamepinga vikali hatua ya Uingereza kupiga marufuku biashara ya Miraa na kusema
ni dawa ya kulevya iliyo kwenye kiwango cha C
Omar Ahmed ni mfanyabiashara wa
Miraa kutoka jamii ya wasomali ambao hutumia sana Miraa.
Kiwango kikubwa cha Miraa inayouzwa
Uingereza takriban asilimia 15 hutoka Meru na ina thamani ya dola milioni 7.5.
Bwana Ahmed anakabiliwa na hasara
kubwa.
"Tutafanya kila tuwezalo,
kuonyesha serikali ya Uingereza kwamba ikiwa hawatajali maslahi yetu
wasitarajie kuwa na sisi tutajali maslahi yao, anasema Ahmed huku akitafuna
majani hayo.
Kila mtu hapa aneonekana kutafuna
Miraa kwa masaa kadhaa , na sasa hasira inapanda.
Bwana Ahmed mwenyewe anaonekana
amelewa kidogo.
Lakini kuna mengi zaidi kuhusu swala
hili kuliko vitisho vya mfanyabiashara huyu.
Mbunge wa eneo hili Kubai Kiringo,
anasema kuwa Kenya huenda ikatafakari upya kuhusu uhusiano wake na Uingereza
ikiwa haitabatilisha, uamuzi wake.
Miraa baada ya kutolewa shambani
huwekwa ndani ya magunia meupe na kusafirishwa hadi Nairobi na kwingineko.
Wakati marufuku hiyo itakapoanza
kutekelezwa baadaye mwaka huu,sera ya Uingereza itakuwa sawa na ile ya
Marekani, Canada na nchi nyinginezo za Muungano wa Ulaya zote ambazo zimeitaja
Miraa kuwa dawa ya kulevya
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment