Monday 30 March 2015

Mkutano Mkuu wa ACT-Tanzania


Zitto Kabwe akihutubia na kuomba kura kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT-Tanzania.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa ACT wazalendo wakisikiliza wagombea nafasi mbalimbali


Wajumbe wakishangilia kwa pamoja hotuba ya hotuba ya Prof. Kitila ndani mkutano Mkuu


Walio makini husikiliza kwa makini ili kufikia maamuzi makini.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Act wakifuatilia taarifa ya Chama Kwa umakini

Rais Nkurunzinza wa Burundi amfuta kazi msemaji wake mkuu

 

Kufuatia joto la kisiasa ambalo limeendela kupanda nchini Burundi, huku chama tawala Cndd- Edd kikikumbwa na mgawanyiko, rais Pierre Nkurunziza, amemfuta kazi msemaji wake, Léonidas Hatungimana.

Wakati huohuo, Pierre Nkurunziza amewateua wasemaji wake wapya, ikiwa ni pamoja na msemaji wake mkuu, Gervais Habayeho pamoja na naibu msemaji wake Louis Kamwenubusa, aliyekua mkurugenzi wa redio inayomilikiwa na chama cha Cndd-Fdd, Rema Fm. Mkurugenzi mkuu wa redio na televisheni vya serikali (Rtnb), Thadée Siryuyumunsi amefutwa kazi, na nafasi yake, ameteuliwa Jérôme Nzokirantevye, aliyekuwa msemaji wa spika wa Bunge.

Sakata hilo lakuwafuta kazi baadhi ya vigogo katika taasisi mbalimbali za nchi linakuja baada ya vigogo hao wakiwa pia wafuasi wenye ushawishi mkubwa katika chama tawala Cndd-Fdd kutia saini kwenye waraka unaomtaka rais Pierre Nkurunziza kutogombea muhula wa tatu katika uchaguzi ujao wa urais.

Hata hivyo wafuasi hao wa chama tawala wameapa kutotetereka na uamzi huo wa kuwafuta kazi, huku wakibaini kwamba wataendelea na msimamo wao hadi pale rais Nkurunziza atakubali kusitisha nia yake ya kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwezi Juni.

Sunday 29 March 2015

Arsenal kumnunua Wanyama na Mitrovic

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kumnunua kiungo wa kati wa Southampton Mkenya Victor Wanyama na mshambuliaji wa Anderlecht Aleksandr Mitrovic kulingana na gazeti la the Sun nchini Uingereza.

Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni millioni 30 kwa wachezaji hao wawili,huku Wanyama akigharimu kitita cha pauni millioni 20 naye mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic akigharimu pauni millioni 10.

Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka katika kilabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na kilabu kikubwa huku naye Mitrovic akiwa amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal katika kipindi cha wiki chache zilizopotea.

Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier Drogba kutokana na mchezo wake.

Credits:BBC

Pengo: Nimesamehe

Askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polcarp Kadinali Pengo amesema amemsamehe mchungaji Gwajima(hakuumtaja) na wote walioguswa ,ameyesema hayo wakati wa Misa Takatifu ya Jumapili ya matawi tarehe 29th March 2015 katika kanisa kuu la ST Joseph Cathedral .

"Naomba niseme kutokana na hali iliyopo kuwa kutoka moyoni kabisa nimesamehe yote yaliyosemwa na naomba tumuombee na kuwaombea wote walioguswa sina kinyongo chochote"

Waumini walilipuka kwa makofi baada ya kusikia kauli ya mwadhama.

Thursday 26 March 2015

Marekani:Uganda hatarini kushambuliwa



Ubalozi wa Marekani nchini Uganda, umesema una taarifa za uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo.
Aidha Marekani pia imetoa tahadhari kwa raia wake.
Taarifa ya ubalozi huo umebainisha kwamba shambulio hilo linaweza kutekelezwa wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa mataifa ya Magharibi na Marekani hukutana.
Katika kipindi kilichopita, kundi la Al-Shaabab lenye makao yake Nchini Somalia, limetekeleza mashambulio Nchini Uganda.
CHANZO:BBC

Man held over illegal gecko import


             

A man has been arrested on suspicion of illegally importing a haul of critically endangered geckos into the country.
The 41-year-old man, from the Swindon area of Wiltshire, has been held on suspicion of an importation offence after Border Force officers at Heathrow Airport found 165 rare turquoise dwarf geckos as part of a consignment of creatures, officials said.
The geckos, which are found in just two locations in Tanzania and protected under international laws, were said to be 7cm (2in) long, weighing 5g, and in good condition when they arrived in freight.

Police are investigating whether the geckos were intended for sale on the black market.
Grant Miller, head of the Border Force Convention on International Trade in Endangered Species team, said: "This was a highly significant seizure. This particular species of gecko is incredibly rare and there are strict laws against its capture in Tanzania.
"The movement of endangered species is part of an illicit and often cruel trade that Border Force, together with other agencies, is rigorously determined to stop."
The geckos are now being cared for at a secure facility.
Also seized from the same consignment were 136 bearded pygmy chameleons, 112 peacock tree frogs, 192 whip scorpions and 66 yellow-headed geckos. These species are not listed as endangered.
:: Anyone with information about activity they suspect may be linked to smuggling is asked to contact the Border Force hotline on 0800 59 5000.
SOURCE: DAILYMAIL

Prof. Baregu: Zitto ni mzigo

Profesa Mwesiga Baregu
         PROFESA Mwesiga Baregu

PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye.

Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.


“Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu.”

Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.

Prof. Baregu aliwahi kuwa “mlezi wa Zitto” ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho “kusaidia kumlea.”

Prof. Baregu ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anasema, “Zitto hamnazo. Amekuwa anajiona yeye ni zaidi ya chama. Hashauriki.”

Anasema wakati ule alipopewa kazi ya kumlea Zitto “katikakati ya migogoro, tulikuwa tunazungumza naye mara kwa mara. Ninamfahamu. Kazi hii ya kumlea tulikabidhiwa mimi na mama yake mzazi, Bi. Shida Salum,” anaeleza Baregu.

Mama mzazi wa Zitto, alifariki dunia Juni mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kauli ya Prof. Baregu ilifuatia gazeti hili kutaka maoni yake juu ya mustakabali wa kisiasa wa Zitto baada ya kuwahi kujiondoa ndani ya Chadema.

EDWARD LOWASA WASHAURI WATU WASUBIRI MUDA WA CHAMA

Lowasa ameshauri kuwa watu wanaotaka kwenda nyumbani kwake kumuomba kwamba ajiandae kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Urais waache kwanza hadi pale Chama chake kitakapotoa taarifa za kuanza kufanya kampeni.
Tamko lake linakuja baada ya baadhi ya watu tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kufika nyumbani kwake na kumtaka kuwa ajiandae kwa kutangaza nia ya kugombea na wao watamchangia fedha za kuchukulia fomu.

Chanzo: Chanel 10

CWT yapasuka, Chama kipya cha Walimu chasajiliwa na Wanachama zaidi ya 9,000

Rais wa CWT, Gratian Mukoba  CHAMA kipya cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) kimesajiliwa rasmi na kupata cheti cha usajili wa kudumu kutoka Wizara ya Kazi na Ajira

 Katibu Mkuu wa Chakamwata, Mwalimu Meshack Kapange, anasema chama hicho kipya kinaundwa na walimu nchini waliojiondoa kutoka mikononi mwa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT). Kapange amesema mchakato wake wa kukisajili chama hicho ulianza miaka minne iliyopita, hadi hivi juzi kilipopewa usajili wa kuendelea na shuhuli zake kisheria.

“Ni furaha iliyoje kupata usajili huu wa chama chetu cha kutetea haki na maslahi ya walimu? Huu ni ukombozi kwa walimu wanaokatwa asilimia mbili za mishahara yao bila kurejeshewa wanapostaafu,” anasema Katibu Mkuu huyo.
Kuundwa kwa chama kipya hicho kumetajwa na wachambuzi wa mambo kwamba kunaweza kuipasua CWT na pia kutahitimisha ukiritimba wa muda mrefu mrefu wa chama hicho. Aidha, chama hicho kitatoa fursa sasa kwa walimu nchini kuwa na hiyari ya kujiunga na chama ambacho wataona kina maslahi kwao badala ya ilivyo sasa ambapo walimu walikuwa hawana chaguo zaidi ya kujiunga na CWT.
Kwa mujibu wa Mwalimu Kapange, Makao Makuu ya sasa ya chama hicho yatakuwa Jijini Mbeya. Anasema walimu watakaohitaji kujiunga na chama hicho kipya, watafanya hivyo kwa hiari yao kama sheria za kazi zinavyoelekeza tofauti na CWT ambayo kila mwalimu anayepata ajira serikalini alikuwa analazimishwa kujiunga na kuanza kukatwa fedha zake kutoka kwenye mshahara wake bila ridhaa yake na kinyume cha sheria za ajira.
“Kila mwanachama atachangia asilimia moja tu ya mshahara wake kwa kila mwezi badala ya asilimia mbili kama ilivyo kwa CWT. Wakati mwanachama anapostaafu, atapewa ‘bonus’ kama asante kwa kuchangia Chama,” anasema Mwalimu Kapange.
Mbali na hilo, Kapange anasema Chakamwata kitafanya jitihada za kuwajengea wanachama wake uwezo wa kutambua wajibu wao, haki zao na jinsi ya kuzidai, badala ya kutambua wajibu pekee kama ilivyo ndani ya CWT, kwa maelezo kwamba hakuna wajibu kwa mtumishi yeyote wa umma usiokwenda sambamba na haki yake.
“Tulipokuwa tukiomba usajili kwa mara ya kwanza Mei, 2012, tulikuwa wanachama 400 ingawa masharti ya kisheria ya kuanzisha vyama kama hivi yanataka wanachama 20 tu. Nashukuru kwamba hadi tunapata usajili huu, wanachama wetu wanafikia 9,743, wengi wao wakitokea mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Arusha, Mara, Morogoro, Singida na Kagera,” amesema.
Chama kipya hicho, kabla hakijasajiliwa, kilikuwa kikijulikana kwa jina la Umoja wa Maofisa Elimu Tanzania (UMET). Hata hivyo, uongozi wa muda wa chama hicho ulikaa tena na kukipa chama hicho jina la Chakamwata. Chama hicho kimepewa usajili kwa namba 031, huku cheti chake kikiwa kimesainiwa na Msajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri nchini, Doroth Uiso.