Rais mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo yuko
nchini Zimbabwe kama mwangalizi wa uchaguzi mkuu
Kampeini za kisiasa nchini Zimbabwe zinamalizika hii leo kabla ya uchaguzi mkuu hapo Jumatano wiki hii.
Kiongozi wa chama cha Movement for Democratic
Change ambaye pia ni Waziri MKuu ,Morgan Tsvangirai, hii leo atahutubia
mkutano wa hadhara mjini Harare katika uwanja alikofanya mkutano wake
hio jana Rais Robert Mugabe.
Viongozi hao wawili wamekua katika serikali ya
muungano tangu mwaka wa 2008 na wametofautiana kuhusu muda uliowekwa
kufanyika uchaguzi. Kumekua pia na madai ya wizi wa kura, na vitisho
dhidi ya wafuasi wa MDC.
Shirika la kimataifa linalotathmini hali ya
mizozo The International Crisis Group limeonya kwamba hakuna mazingira
ya uchaguzi huru na haki Zimbabwe.
BBC
No comments:
Post a Comment