Thursday, 25 July 2013

pAPA AWATAKA WAKRISTO KUTOPENDA MALI NA MADARAKA

  Papa Francis

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis, amewataka Wakristu Wakatoliki kuachana na kile alichokiita kupenda mali na madaraka.

Wito huo ameutoa wakati akiadhimisha Ibada ya Misa katika Pango Takatifu huko Aparecida, kwenye jimbo la Sao Paulo nchini Brazil.

Akihubiri wakati wa Ibada ya Misa yake ya kwanza kuadhimisha tangu awasili Brazil, katika Kanisa Kuu la madhabahu ya Mama Bikira Maria wa Aparecida, Baba Mtakatifu Francis, amewasihi Wakatoliki na hasa vijana wajiepushe kufata njia zinazopotosha na hatimaye kuwaweka njia panda.

Amesema siku hizi watu wamekuwa wakivutiwa zaidi na starehe, mafanikio, utajiri na madaraka na hivyo kuwasihi wazingatie suala zima la imani na ukarimu, ili kurejesha matumaini yanayoanza kupotea miongoni mwa jamii.

Mahujaji vijana wanaohudhuria kongamano lao Brazil

Amesema amemuomba Mama Maria aliyempenda na kumtunza Yesu awasaidie watu wote wakiwemo viongozi wa Kanisa, wazazi na walimu, ili waweze kufikisha ujumbe wa maadili mema kwa vijana, ambao utawasaidia kulijenga taifa na dunia itakayozingatia haki, usawa, umoja na udugu.

Maelfu wabarikiwa

Baada ya Ibada ya Misa, Baba Mtakatifu alisali tena kwenye Pango la Mama Maria wa Aparecida na kisha akawabariki maelfu ya waumini waliokuwa nje ya Kanisa Kuu na kutangaza kwamba atarejea tena Aparecida mwaka 2017, wakati wa kuadhimisha miaka 300 ya mvuvi aliyeiokota picha nyeusi ya Mama Maria, karibu na mto.

Kisha Papa huyo, alirejea mjini Rio de Janeiro, ambapo alifungua hospitali ya Mtakatifu Francis wa Asizi kwa ajili ya wagonjwa wa akili na hasa waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya, iliyopo mjini Rio de Janeiro.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amesema kuwa tatizo la biashara na matumizi ya dawa za kulevya ni janga kubwa katika eneo la Amerika ya Kusini. Amesema jukumu kubwa lililoko sasa ni kuwaelimisha vijana maana na tunu za maisha ya pamoja, pamoja na kuendelea kuwasaidia walioathirika na dawa hizo.

Shughuli za Papa siku ya leo (25.07.2013)

Leo, Baba Mtakatifu ambaye yuko nchini Brazil kwa ziara ya wiki nzima, ataianza siku yake kwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye makaazi yake ya muda huko Sumare, Rio de Janeiro na kisha atapewa ufunguo wa mji huo pamoja na kubariki bendera za Olimpiki.

 

Aidha, Papa atatembelea eneo la mitaa ya mabanda na baadae jioni atawakaribisha zaidi ya vijana milioni moja kutoka sehemu mbalimbali duniani katika ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Vijana wa Kikatoliki Duniani kwa mwaka wa 2013. Shughuli hiyo itafanyika katika ufukwe wa Copacabana, huko Rio de Janeiro.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu ametoa pole kwa familia za watu waliopoteza maisha katika ajali ya treni iliyotokea nchini Uhispania jana. Abiria wengi katika treni hiyo, walikuwa mahujaji wanaoelekea Santiago de Compostela, kuhudhuria sherehe za mtakatifu msimamizi wa mji huo.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/APE,DPAE
Mhariri: Josephat Charo

source:dw.de

Islamic Banking - NBC yawatoa hofu wananchi kuhusu akaunti ya Kiislamu

Baadhi ya wateja wa Benki ya NBC, wakifuturu katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Dar es Salaam. Serikali imewatoa hofu Watanzania ikiwataka kutosita kujiunga na kutumia huduma za kifedha zinazofuata kanuni za Kiislamu kwa kuwa huduma hiyo ni mkombozi kwa wananchi wengi.
Akizungumza wakati wa hafla ya futari kwa wateja iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema bidhaa hiyo imeletwa katika muda mwafaka.
Huduma hii hufuata sheria na kanuni za Kiislamu. Ni huduma inayojali na kufuata maadili na ni furaha kwa Serikali kuona kwamba hatimaye maadili sasa yanaingia hadi kwenye huduma za kifedha.
Maadili yakiwa imara katika jamii, tunatarajia pia kupata uchumi imarawenye kukua na viwanda vyenye kuzalisha bidhaa na huduma zenye kukidhi mahitaji ya wote, alisema.
Saada aliiomba NBC kuendelea kubuni na kuwaletea Watanzania huduma nyingine zenye kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja, wakubwa kwa wadogo, hususan mikopo kupitia Huduma ya Kibenki ya Kiislamu.
Aliitaka pia benki hiyo kutoa elimu kwa Watanzania ili waweze kufahamu kwa undani faida ya huduma hiyo ambayo iko wazi kwa yeyote bila kujali itikadi au imani yake ya kidini.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu alimuahidi Naibu Waziri kwamba benki hiyo haitaacha mipango yake ya kuisaidia Serikali kutekeleza kauli mbiu yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania .
Naye Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Kibenki ya Kiislamu, Yassir Masoud alisema kuwa muda si mrefu NBC itaanzisha huduma za mikopo kupitia bidhaa hiyo, akisisitiza kwamba wanaelewa kuwa watu wengi wanaisubiri kwa hamu kubwa.
Huduma ya Islamic Banking ya Benkiya NBC ilizinduliwa Mei 2010
 

source:MCL

Kim Kardashian, Kanye West Spent Sh 63.7M on Gold Toilet

 Kanye West 

   Kim Kardashian and Kanye West     Photo:Courtesy

When it comes to money, Kim Kardashian and Kanye West definitely have a lot of it. That is why it may not be such a big deal for them to drop more than $750,000 on, say, something like gold toilets.

British tabloid The Sun claims Kardashian and West spent around $767,000 on four gold-plated toilets for their swanky new Bel Air, Calif., mansion.

They also reportedly dropped $444,000 on six special beds and nearly $325,000 on kitchen appliances, plus a Swarovski crystal-encrusted fridge freezer.

This isn't the first time the reality star has been linked to an over-the-top commode. Last year, another tabloid report claimed Kardashian spent $100,000 on a self-flushing toilet. She purportedly made the purchase because she was scared of guests forgetting to flush on their own.

Even though they might have a combined net worth of around $140 million, we aren't so sure Kardashian and West would choose to spend their hard-earned cash on luxury latrines.

What we do know for certain is that Kardashian is very particular about her bathrooms and what goes on in them.

While staying with mom Kris Jenner, the 32-year-old has criticized the black shower and black toilet paper in Jenner's house. Back when she was married to Kris Humphries, she complained about the NBA star's bathroom habits, including how he spritzed the mirror while brushing his teeth.

-Huffington Post

Influential midfielder Yaya Toure on Thursday backed new manager Manuel Pellegrini to bring silverware to Manchester City, describing him as "unbelievable".

The former Malaga coach got his first victory as City boss in a 1-0 win over South China in Hong Kong on Wednesday, having only arrived in the region a day earlier after the death of his mother.

Toure said he hopes the Chilean, who replaced the sacked Roberto Mancini, can bring trophies to the Etihad after rivals Manchester United romped to the Premier League title last season.

"Last year, we have to be honest, United were much better than us," said the former Barcelona man, 30.

"We are working and trying to understand and learn from the new manager, who had a fantastic record in the past in Spain."

He added of Pellegrini: "Unbelievable, great things, his ability to manage is unbelievable and he's doing fantastically well. We are all focused on him and trying to understand what he wants us to deliver and what he wants us to do on the pitch.

"He's an unbelievable guy, a very good guy, and dedicated to his work, and you can see his commitment. He's a very good choice for Man City and I hope he's going to bring a lot of trophies to Man City.

"When you change mangers, sometimes it is quite hard because you need to adapt to the new formation. But with the new signings I think it is going to be very exciting."

City have been the biggest spenders over the summer as they attempt to wrestle the Premier League crown back from Old Trafford, shelving out 83 million pounds ($126 million, 96 million euros) on new players.

They have brought in strikers Alvaro Negredo from Sevilla and Stevan Jovetic from Fiorentina, as well as Spanish midfielder Jesus Navas and Brazil midfielder Fernandinho from Shakhtar Donetsk.

"They are amazing, amazing. I already know them because some of them have come from Spain... They are great players and we welcome them to Man City.

"I hope the fans will enjoy them and they will help the club lift a couple of trophies this year."

SOURCE: AFP

ERO LINK RECRUITMENT AGENCY SCANDAL

 

The government has formed a team to investigate complaints of workers against recruitment agencies they accuse of engaging in exploitative arrangements, to determine if they are observing the Labor Relations Act of 2004.

Speaking of initiatives taken by the government to address problems facing workers recruited by private agencies, Deputy Minister for Labor and Employment Dr Makongoro Mahanga told The Guardian in a telephone interview that among other things the government will consider the essence of having such agencies in the first place.

He said his ministry will also liaise with the Tanzania Revenue Authority (TRA) to find out the mode through which they pay their taxes.

The minister said the issue of workers in a particular company working under different recruiting agencies’ payrolls has prompted misunderstandings between employees and the employers.

The Guardian recently came across letter complaining against the arrangement, saying workers are being cheated by some recruiting agencies.

When interviewed some of the employees who blame the recruiting agencies for taking advantage of the employment crisis to offer their clients workers recruited at much lower salaries compared to the actual amount paid by these companies.

Some employees recruited by the Erolink recruiting agency, claimed that the agency is full of nepotism and tend to favour the experienced personnel.

They alleged that Erolink has entered a contract of recruiting workers for some giant corporate companies and that it signs renewable three to six-month contracts with the recruited workers, apparently to avoid employing them on full term basis.

“Within the three-month contracts, salaries are indirectly paid to workers through Erolink management which determines the amount of salary to be paid to the workers,” read part of the letter.

The letter claimed that such arrangements deny workers basic rights such as health insurance, job security, being eligible to access loans and extra hours’ payments which are exclusive to their counterparts who are directly employed by the companies.

Reacting to the claims, Erolink Tanzania General Manager Natasha Ng’wanakilala and two advocates Evold Mushi and Godfrey Tesha refuted the claims saying the agency has been working according to the Labour Relations Act 2004 and that all workers were treated equally, stressing that her agency is ready for any assessment by the government.

When queried on the actual payments the agency gets from the companies for every worker they recruit, she said the payments are confidential under the contract agreement between the two parties, but that the documents will be disclosed if required by the ministry of Labour or any legal organ.

On claims of variation in payments between workers recruited by the agency and those directly employed by their clients despite being of the same rank and having similar qualifications, she said the arrangement is due to policies of the respective companies.

Tanzania Employment Service Agency (TaESA) Chief Executive Eliezer Mwasele told this paper in a telephone interview that the outsourcing agencies are supposed to work according to the country’s Labour laws and directives of the International Labor Organization (ILO).

For his part, TaESA Acting Chief Executive Officer Boniface Chandaruba said his office was aware of the matter, noting that he could not comment anything as there was a team which had already formed by his boss to investigate the matter.

SOURCE: THE GUARDIAN

Mgoni akatwa miguu yote miwili baada ya kunaswa akila uroda na mke wa mtu

 
 ALI Omar, mkazi wa Kijiji cha Mabana, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumkata miguu Said Iddi kwa kumtuhumu kumfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la mama Ali, mkanda mzima upo mikononi mwa Amani.

Tukio hilo la kikatili lilijiri Julai 15, mwaka huu wakati Said na mama Ali walipokuwa ndani ya nyumba ya Ali iliyopo kijijini hapo.



MANENO YA SHUHUDA
Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisema Said alifumaniwa ndani ya nyumba asubuhi akiwa na mke wa Ali baada ya kuwekewa mtego ambao ulimnasa vizuri.

Ali alipewa habari na kijana mmoja aitwaye God kwamba mkewe si mwaminifu katika ndoa, akamwongezea kuwa anatoka kimapenzi na Said. Ndipo Ali na mnyetishaji wake huyo walipopanga kumfumania jamaa,” alisema shuhuda.
Aliongeza kudai kuwa, Said ni msimamizi wa mashamba ya Ali kijijini hapo na kwamba God ni mtoto wa mwenye nyumba ambayo Ali amepanga kijijini hapo.

MPANGO WA FUMANIZI
Habari zinapasha kuwa mara baada ya mnyetishaji kutoa taarifa za usaliti huo, Ali alimtafuta ‘baunsa’ ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja na wakaweka mtego kwa kujificha karibu na nyumba hiyo ambayo Said angeingia ili kuivunja amri ya sita ya Mungu.


Katika kufanikisha mtego huo, mmbeya huyo alipewa jukumu la kuhakikisha nyendo za Said na mama Ali siku hiyo zinarekodiwa mpaka kuingia ndani ya nyumba hiyo na kumtaarifu Ali ambaye siku hiyo alimuaga mkewe kwamba amesafiri.

SAID ATINGA NYUMBANI KWA ALI
Habari zinasema mtoboa siri huyo alimwambia Said kuwa Ali amesafiri na ndipo jamaa akafunga safari kwenda kwa mama Ali kwa nia ya kujivinjari licha ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukifikia katikati.

Habari zinadai mara baada ya kufika kwa Ali, Said aliingia ndani ya nyumba bila kujua kwamba mwenye mke alikuwa amejificha jirani akisubiri mtego unase.

Inasemekana Said akiwa ndani, Ali na baunsa wake waliibuka kwa kutaarifiwa na God na kumnasa jamaa huyo huku akidai ni mgoni wake. Alimuuliza maswali kadhaa, yakiwemo haya:“Umekuja kufanya nini ndani ya nyumba yangu? Kwa nini umekaa na mke wangu?”
Habari zinasema Said alijibu hakuona ubaya kwa kuwa yeye ni mwangalizi wa mashamba ya mwanaume huyo hivyo anaweza kuingia ndani kwake wakati wowote.

MWENYE MKE ATIBUKA NA MAJIBU, AMWAGA DAMU
Jibu hilo lilidaiwa kumtibua Ali na ndipo yeye na baunsa wake wapomfunga kamba miguuni Said na kuanza kumkata kwa panga mguu mmoja kisha kuugeukia wa pili.

Said alipiga mayowe yaliyowafanya wanakijiji kukimbilia eneo la tukio kwa lengo la kujua kulikoni ambapo walimkuta Said akiwa anavuja damu na sehemu ya nyuma ya miguu ikiwa nyanga’nyang’a.

MWENYE MKE AKIMBIA, ANASWA
Ali, God na baunsa walikimbia eneo hilo. Baadhi ya wanawake walitumia khanga zao kuifunga miguu ya Said kwa lengo la kujaribu kuzuia damu isiendelee kumwagika. Said alikuwa akilia sana.

Wanakijiji walichukizwa sana na ukatili uliofanywa na Ali, hivyo wakaanza kumsaka na kumkamata kichakani akiwa amejificha pamoja na God. Alipewa mkong’oto kwa lengo la kutaka kumuua, lakini viongozi wa kijiji walisihi asiuawe bali afikishwe kwenye kituo cha polisi,” alisema shuhuda.

MKE, MUME, MMBEYA WAFIKISHWA POLISI
Polisi wa Kituo cha Dumila waliitwa na kumchukua Said, Ali na God kwa kutumia gari aina ya Land Rover lenye namba za usajili T 750 AAJ. Mke wa Ali yeye alipelekwa polisi kwa pikipiki.

Walipofika kituoni, Said alipewa fomu ya matibabu ya polisi (PF 3) na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa matibabu.
Pale hospitali Said alishonwa miguu yote lakini madaktari wakaamua ahamishiwe katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi,” alisema shuhuda huyo.

ANAWEZA ASITEMBEE TENA
Akaongeza: Daktari mmoja alisema haamini kama jamaa (Said) atatembea tena kwa sababu zana iliyotumika kumkata ilifika hadi kwenye mishipa ya nyuma ambayo ndiyo humfanya binadamu aweze kusimama na kutembea.

BAUNSA ASAKWA
Afisa mmoja wa polisi kituoni hapo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji, alisema wanaendelea kumsaka baunsa aliyeshirikiana na Ali kumkata miguu Said.

SOURCE: GLP

Wednesday, 24 July 2013

SHILOLE MATATANI WIZI SIMU ZA DIAMOND

 

Stori:Shakoor Jongo na Musa Mateja
STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.
Msanii huyo alikumbwa na kasheshe hilo Julai 19, 2013 nyumbani kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mori, Dar.
Siku hiyo Diamond alikuwa akifuturisha na aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa lakini nusura futuru iingie doa kufuatia zogo hilo.

ISHU ILIKUWAJE?
Ndugu wa Diamond aitwaye Majaliwa Majuto ‘Q Boy’ alidai ndiye mwenye simu hizo. Alisema miezi kadhaa iliyopita, Shilole alikwenda nchini humo kufanya shoo ya muziki. Wakati wa kuondoka alimpa simu tatu, Ipad, Samsung Galaxy na Blackberry ili akifika Bongo ampe Diamond lakini msanii huyo hakufanya hivyo.

“Alikuja Sauzi kufanya shoo, wakati wa kuondoka nilimpa simu tatu amletee Diamond lakini nashangaa hakufanya hivyo na mimi tangu nirudi Bongo simpati, kila nikimpigia simu hapokei, leo ndiyo tumekutana hapa kwa Diamond,” alilalama Q Boy.
DIAMOND ALIAMBIWA SIMU ANAZO SHILOLE
Alisema awali akiwa nchini humo baada ya kumkabidhi mali hizo, alimpigia simu Diamond na kumtaarifu kuwa ‘mzigo’ anao Shilole, akashangaa staa huyo kujibu kwamba hajazipata wala hajamwona Shilole.

SHILOLE AJITETEA
Katikati ya mzozo huo, Shilole alijitetea kwa kusema: Mi namdai rafiki yake fedha yangu ya shoo iliyobaki, kama shilingi laki nane hivi ndiyo maana nikaamua kuzizuia simu za huyu (Q Boy) hadi nimaliziwe pesa yangu.
Hata hivyo, katika sakata hilo ilielezwa kuwa Shilole na Q Boy hawakuwa na makubaliano yoyote kuhusu shoo hiyo na simu hizo hivyo madai ya mwigizaji huyo ni ‘usanii’ tu.

MAMA DIAMOND AINGILIA KATI KUOKOA
Zogo hilo lilipopamba moto na kuashiria kuvurugika kwa amani, mama mzazi wa Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ aliamua kuingilia kati na kuagiza suala la kudaiana simu lifanyike kesho yake (Jumamosi) kwa vile siku hiyo haikuwa muafaka.
“Jamani! Jamani! We nani, Shilole na we Majaliwa, naomba kwa leo muepusheni shetani kwani hapa si mahali pake, ila kesho tutaitana na kumaliza suala hili, mimi mwenyewe nitalisimamia,” alisema bi mkubwa huyo na kumaliza henyahenya iliyoibuka.

JUMAMOSI YAFIKA, KIKAO VIPI?
Jumamosi, mapaparazi wetu walifuatilia ishu hiyo nyumbani kwa akina Diamond na kuulizia ili kujua kama kikao cha usuluhishi kilifanyika kama mama Nasibu alivyoagiza.
“Mh! Sijaona kikao chochote, kwanza Shilole mwenyewe akipigiwa simu hapokei,” alisema ndugu mmoja wa Diamond huku akiomba hifadhi ya jina lake.

MSIKIE DIAMOND
Juzi, Diamond alipopigiwa simu na kuulizwa kama anaijua ishu ya simu, alikubali.
Staa huyo alisema anashindwa kuingilia kati sakata hilo kwa sababu wahusika wote ni watu wake wa karibu kikazi.
“Yeah! Ishu ni kweli ipo, lakini mimi nilijiweka kando mapema, nikamwambia dogo (Q Boy) afuatilie mwenyewe baada ya kuona Shilole haeleweki.
“Unajua Shilole ni mwanamuziki mwenzangu, dogo yupo ndani ya Kampuni ya Wasafi Entertainment (ya Diamond), sasa kukomaa na ishu za simu tu nahisi itanishushia hadhi, napiga shoo za hela nyingi halafu leo nakomaa kwa hela ndogo, inakuwa siyo,” alisema Diamond.

SHILOLE TENA
Baada ya kuzungumza na Diamond, Shilole alipigiwa simu na kuomba kufafanua kwa undani ishu hiyo ambapo katika hali isiyotarajiwa, alimlalamikia paparazi wetu akidai anapendelea katika sakata hilo.
“Nyiye mnamtetea tu yule dogo, mimi sina tatizo, kama rafiki yake (aliyemuitia shoo Afrika Kusini) akinilipa hela yangu nawapa simu zao,” alisema Shilole.
Msanii huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia paparazi kuwa atatia timu kwenye Ofisi za Global Publishers ili kuzungumzia suala hilo na viongozi.
Baadaye Shilole alifika ofisini kwetu na kufafanua juu ya sakata hilo ambapo alirudia kukiri kuzuia simu hizo akidai kwamba anamdai Q Boy hivyo mpaka atakapomlipa ndiyo atampa simu zake.

Q BOY NAYE TENA
Kwa upande wake, Q Boy alipozungumza na paparazi wetu siku hiyo alisema amekusudia kwenda kufungua kesi kituoni ili apewe msaada zaidi wa kisheria kwa vile simu hizo zinamuuma hasa ukizingatia kuwa yeye siye aliyempeleka Shilole Afrika Kusini kufanya shoo.
“Mimi leo (Jumatatu) nimebanwa sana, kuna sehemu nakwenda na Diamond, nadhani nitamaliza jioni. Lakini kesho (Jumanne) nitaamkia polisi kufungua kesi nione watanisaidiaje?” alisema Q Boy.

POLISI AGUSIA ISHU
Risasi Mchanganyiko lilizungumza na askari mmoja kutoka Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kummegea mtiririko wote, kisha kumuuliza kama kuna kesi ambapo alijibu:
“Japokuwa mimi si msemaji wa jeshi (la polisi), lakini ishu kama hiyo shitaka lake lipo, ni wizi wa kuaminiwa. Unajua wengi wanadhani kuibiwa lazima mtu uwe hujui, lakini mtu akifanya kama hivyo alivyofanya huyo msanii nani sijui (Shilole), kama ni kweli, kosa linakuwa wizi wa kuaminiwa endapo atafikishwa polisi.”

DIAMOND, Q BOY WALIFANYA MCHEZO?
Hata hivyo, baadhi ya watu walioshuhudia sakata hilo walikuwa na maswali kibao yaliyokosa majibu.
Swali la kwanza: Shilole alikwenda kufuturu kwa mwaliko wa Diamond na alijua staa huyo na Q Boy ni wamoja na simu alizopewa ilikuwa amletee msanii huyo, kwa nini alikwenda huku akijua ana msala?
Swali la pili: Kama Shilole alikwenda akijua Q Boy hayupo Bongo, je! Si kwamba ulikuwa mpango wa wawili hao kumwita ili wampe kibano ateme simu zao?
Swali la tatu: Je, ni kweli Shilole alizuia simu ili amaliziwe deni lake kwa mtu aliyemuitia shoo Afrika Kusini au shetani alimwingia baada ya kutua Bongo na kuamua kuzitumia hasa ikizingatiwa kuwa siku hizi mambo ya Instagram ndiyo habari ya mjini? 

CHANZO: GPL