Monday, 13 July 2015

Rais Kikwete na Mkapa wakishangilia na kufurahi baada ya kuzima maasi ndani ya CCM!


Rais Kikwete na Mzee Benjamin Mkapa hawakujizuia kuonyesha furaha zao baada ya kuyakata majina ya baadhi ya wagombea na kuzima maasi ya baadhi ya wagombea na wafuasi wao ndani ya NEC na Mkutano Mkuu.

Hii ilitokea baada ya kumaliza kikao cha Mkutano Mkuu ambao ulimteua John Pombe Magufuli kuwa mgombea Urais wa Tanzania kwa Tiketi ya CCM na Samia Hassan Suluhu kuwa Mgombea Mwenza.

Baada ya kutoka nje ya ukumbi wa mikutano huku wakiongozana, Rais Kikwete alisikika akipaza sauti na kusema ‘mission accomplished’ akimaanisha mikakati yao timilifu imezaa matunda waliyotarajia.

Walichokifanya hawa Wazee wa CCM ni kile kinasemwa, demokrasia isiyo na mipaka ni vurugu kwa maana kwamba waliwapa wajumbe wa NEC na Mkutano Mkuu demokrasia lakini wakawapa mtu wao wanayetaka wamchague.

Aliyekuwa anapiga kelele barabarani akidai hakatwi mtu alijikuta akiwa yeye ndiyo wa kwanza kukatwa.

Ama kweli, CCM ina wenyewe!

No comments:

Post a Comment