Sunday, 12 July 2015

Msako mkali Mexico wa muuza mihadarati


Mamlaka ya nchini Mexico limeanza msako mkali wa kumtafuta Joaguin Guzman gwiji la biashara ya madawa ya kulevya duniani, kufuatia kutoroka kwake katika gereza lenye ulinzi mkali mwishoni mwa wiki.
Helikopta za Blackhawk ambazo zimeonekana kuruka juu gerezani Altiplano magharibi ya Mexico City mahali alipokuwa ameshikiliwa huku ndege zote zikiwa zimezuiwa kuruka karibu na Uwanja wa ndege.
Wafanyakazi wa magereza wanahojiwa baada kubainika kuwa Joaguin alitoroka kupitia njia ya nchini ya ardhi yenye urefu wa kilomita moja na hii ni mara ya pili kutoroka.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Marekani, Loretta Lynch, ametoa msaada wa kumkamata Guzman ambae pia hujulikana kama ' El Chapo ' .

No comments:

Post a Comment