Kocha wa kilabu ya Manchester United
Louis Van Gaal amethibitisha kuwa beki wa kilabu ya Torino Matteo
Darmian atafanyiwa ukaguzi wa matibabu kabla ya kuhamia kilabu hiyo kwa
pauni milioni 12.9.
Mshambuliaji wa Manchester united Robin Van
Persie tayari anaendelea na mazungumzo na kilabu ya Fenerbahce na Van
Gaal anasema:Iwapo tutahisi anaendelea vyema tutasema,lakini kufikia
sasa hatuna hisia hiyo.Kuhusu uhamisho,aliongezea:''Nilisema mwishoni mwa msimu uliopita kwamba ununuzi wa wachezaji na uuzaji ni hatua.Hatua hiyo huendelea hadi mwezi Septemba.''Naona kama uhamisho huo unachukua mda mrefu.Nimesema hivyo mara nyingi.hatahivyo tunaendelea vyema''.
No comments:
Post a Comment