Mtoto aliyepigwa picha akidurusu
usiku nje ya mkahawa wa McDonald huko Ufilipino amevutia hisia kali ulimwenguni
kote kwa ari yake ya kupata elimu.
Mwanafunzi wa Uuguzi bi Joyce
Torrefranca, ndiye aliyeipiga picha hiyo nje ya mkahawa huo wa McDonald ulioko
katika mki wa Cebu nchini Ufilipino na akaichapisha kwenye mtandao wake wa
kijamii wa Facebook na ujumbe
Mtoto aliyekosha ulimwengu kwa ari
yake
''mtoto huyo amenikumbusha niwekee
bidii maishani''
Katika picha yake bi Torrefranca
mtoto mwenye umri wa miaka 9,Daniel Cabrera amejikunyata kwenye kibao
anachokitumia kama meza akifanya mabaki ya kazi aliyopewa shuleni.
Mtoto huyo Cabrera anatumia mwangaza
wa bango la kutangaza duka la McDonald kama taa yake akidurusu !
''kwangu mimi kama mwanafunzi
,nilipigwa na mshangao kutokana na ari ya mwanafunzi huyu mdogo aliyekuwa
amechutama akikamilisha kazi yake ya shuleni bi Torrefranca aliiambia runinga
ya ABS-CBN katika mahojiano.
''kwa hakika ilinipatia changamoto kubwa
niendeleee kufanya bidii katika kila jambo linalonikabili''
Muda mchache baada ya bi Torrefranca
kuchapisha picha hiyo kwenye Facebook maelfu ya watu waliichapisha pia wakisema
kuwa ilikuwa imewavutia sana.
''Ukitaka kitu ama ukitaka
kufanikiwa maishani sharti itie bidii katika kila jambo unalokabiliwa
nalo,hivyo utapiga umaskini teke'' alisema bi Torrefranca.
Bi Joyce Torrefranca akihojiwa
katika moja ya runinga ya taifa
Alipohojiwa kijana huyo Daniel
alisema kuwa aligundua babake mzazi alichomwa moto hadi kufa katika ajali
mbaya.
Kakake mwengine ni mgonjwa sana
alisema Daniel.
Kijana anasema kuwa yeye hulazimika
kupiga buku nje ya mkahawa huo wa McDonald kila usiku akimsubiri mamake
akamilishe wajibu wake katika mkahawa ulioko karibu.
Afisa wa serikali anayeshughulikia
maslahi ya watoto tayari ameitembelea familia ya Daniel kwa nia ya kuwapa
msaada wa kujinasua kutoka kwa minyororo ya Umaskini.
Kwa upande wake vyombo vya habari
vimekuwa vikimmiminia sifa kochokocho bi Torrefranca kwakuangazia masaibu yanayomkabili
kijana daniel.
No comments:
Post a Comment