Monday 27 July 2015

Upepo umegeuka, Marafiki wa Lowassa wapinga swahiba wao kwenda CHADEMA, Apson Matatani


kambi ya Lowasa kwa sasa tumbo joto kutokana na mgawanyiko mkubwa uliojitokeza. Kambii hiyo imegawanyika na kuzaa timu mbili. Timu ya kwanza inaundwa na wastaafu akiwemo Apson Mwang'onda na viongozi wa CCM wa Mikoa na wilaya. Wengi wa wanaounda kundi hili ni wachovu kifedha na wanaishi kwa kutegemea Marafiki wa Lowasa.

Timu ya Pili inaundwa na Marafiki wa Lowassa ambao ndio wenye fedha. Taarifa za uhakika kutoka kambi hiyo zinasema kuwa Marafiki wa Lowasa wakiongozwa na Rostam Aziz pamoja na Mke wa Lowasa Regina Lowasa hawataki rafiki yao aende upinzani. Hoja wanazotoa ni pamoja na hizi zifuatazo;

1. Marafiki wa Lowassa wanasisitiza kuwa Apson Mwang'onda ni mpotoshaji. Kwamba, ni Apson ndiye aliyetoa ushauri mbaya kwa Lowassa mpaka akapoteza muelekeo ndani ya CCM hali iliyosababisha jina lake kukatwa katika hatua za awali. Kwamba, Apson alikuwa anawahakikishia kuwa hakuna mwenye jeuri ya kukata jina la Lowassa na kwamba wakithubutu kufanya hivyo hapatakalika. Hata hivyo, kilichotokea ni kinyume chake.

2. Vyama vya upinzani havina dhamira ya dhati kwa Lowasa. Wao wanachokihitaji ni fedha zake na mashabiki wake ili waongeze idadi ya viti vya wabunge na kura za Rais. Kwamba, siku zote vyama hivyo vilikuwa vinamtukana
Lowassa na kumtolea kila aina ya maneno machafu. Sasa wanashangaa vyama hivyo hususan CHADEMA wanamuona Lowassa kama malaika.

3. Marafiki wa Lowasa wametumia fedha nyingi wakati wa mchakato ndani ya CCM. Lowasa aliwahakikishia kuwa atabaki ndani ya chama na kwamba hata asipoteuliwa kupeperusha bendera hatahama chama na badala yake atatafuta haki ndani ya chama hicho. Hata hivyo, wanashangaa kuona rafiki yao akiendelea kukaa kimya badala ya kuchukua hatua ndani ya chama kama alivyoahidi. Kwamba, tangu jina lake likatwe, hajachukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kupeleka malalamiko kwenye vyombo husika. Kutokana na hali hiyo marafiki hao wanaona kuwa uamuzi uliochukuliwa na chama ulikuwa ni sahihi isipokuwa rafiki yao alikuwa na agenda ya siri kwa kushirikiana na Apson Mwang'onda.

4. Wafuasi wengi waliokuwa upande wa
Lowassa wameridhika uteuzi uliofanywa na CCM ambapo wamemteua John Magufuli kuwa Mgombea Urais. Wanasema kuwa wao walichokuwa wanahitaji ni CCM kumteua mtu mwenye maamuzi na mwajibikaji. Magufuli ana sifa zote walizohitaji. Hivyo wanasema kuwa Lowasa asijidanganye kuwa wafuasi wake watamfuata upinzani.

Kutokana na hoja hizo, marafiki wa
Lowassa wamesema kuwa hawapo tayari kuendelea kupoteza fedha kumgharamia mtu ambaye hana msimamo. Hata hivyo, wanasema kuwa wapo tayari kumsaidia Lowasa kwa namna atakayotaka ikiwa atafanya maamuzi ya kuachana na siasa.

Kundi la Apson Mwang'onda kwa upande wake linasisitiza kuwa ni lazima
Lowassa aende upinzani ambako ameahidiwa kupata nafasi ya kuwa mgombea Urais. Kwamba, hata kama Lowasa hatachaguliwa kuwa Rais, atakuwa amewatuliza wafuasi wake ambao wamepoteza muda na fedha nyingi kumfikisha hapa alipo.

Mvutano huo umemuacha
Lowassa njia panda. Afuate ushauri wa marafiki zake ambao wamemsaidia kwa kila hali na kwamba wameahidi kumsaidia katika maisha yake nje ya siasa au kuendelea kushikamana na Apson ambaye siku zote amekuwa akimponza kutokana na ushauri wake.

Kutokana na hali hiyo,
Lowassa ameshindwa kukamilisha deal lake na CHADEMA kama alivyopanga na badala yake anaendelea kuwapiga danadana huku akiwaacha tumbo joto.

Ni dhahiri sasa kuwa Lowasa atafuata ushauri wa marafiki zake kuliko ushauri wa Apson. Katika hili, mchango wa Rostam unaonekana dhahiri na anaonekana kuwa ndiye rafiki wa dhati wa The White Hair. Wengine walikuwa kimaslahi zaidi.

No comments:

Post a Comment