Wednesday, 1 July 2015
Kigogo wa Bandari Afumaniwa Ndani ya Mwezi Mtukufu...Ajipiga Faini ya Mil 30..Kisa Kizima Nimekuwekea Hapa
GPL
WE acha tu! Hii ni habari ya kushangaza sana ambayo ilinaswa na paparazi wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers juzikati ambapo mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ally Mwamwanza ambaye ni afisa katika kitengo cha ‘makontena’ bandarini Dar, kudaiwa kunaswa na mke wa jirani yake, Gibson Mtinge aliyetajwa kwa jina moja la Khadija.
Licha ya wote wawili kuishi Mbezi ya Kimara, lakini kisanga hicho kilichojiri mwishoni mwa wiki iliyopita saa 12 asubuhi kilichukua nafasi maeneo ya Tegeta-Kibaoni jijini Dar es Salaam.
OFM YAKATIZA
OFM ilikuwa katika pilikapilika ya kusaka matukio ya usiku katika viwanja mbalimbali vya Jiji la Dar. Wakati inapita nje ya nyumba hiyo, kelele za ‘hoya! Hoya’ ziliifanya OFM kupiga kambi hapo kusikiliza.
OFM NDANI YA GETI
Hoya! Hoya zilipokomaa, ndipo OFM ilipoamua kusukuma geti na kuzama ndani ya mjengo huo wa maana na kukutana na kasheshe ya mwaka, wanaume wawili wakitwangana.Mwanaume aliyejitaja kuwa ni mfanyabiashara wa kusafirisafiri ambaye ndiye Gibson alidai amemfumania Ally akiwa na mkewe kitandani kwenye chumba kimoja ndani ya nyumba hiyo.
“Huyu jamaa nimemkuta na mke wangu. Huwezi kunifanyia hivi bwana Ally. Halafu wewe ni jirani yangu kabisa,” alifunguka Gibson kwa sauti yenye kuweza kufanya lolote kwa wakati huo kama si Mungu kumdhibiti shetani.
MTUHUMIWA ALITOKA KWAKE MUDA WA DAKU
Habari zaidi kutoka kwenye kinywa cha Gibson zilisema kuwa, Ally alikuwa akimtongoza mkewe kwa siku nyingi. Ikafika mahali, mke huyo akachoka na kumweleza mumewe ambapo waliweka mtego.
Siku hiyo, inadaiwa Ally alichati na mwanamke huyo akitaka waonane, mke akamwambia hayupo Mbezi wanapoishi, amelala Tegeta kwenye nyumba ya dada yake kwa vile dada huyo amekwenda Mbeya. Kwa hiyo kama anataka yeye aende Tegeta.
“Jamaa katoka kwake Mbezi saa 10 alfajiri, muda ambao watu wanakula daku kwa ajili ya mfungo. Alimuaga mkewe anakwenda kazini,” alisema Gibson huku akivuja jasho maana Ally naye ni bonge.
Ina maana taarifa hizo, Gibson alipewa na mke wake ambaye alikuwa akichati na Ally!
MAJIRANI WAINGILIA KATI
Majirani wa eneo hilo, baada ya kusikia sekeseke walizama ndani na kufanya kazi ya ziada kuwatuliza na kumtaka Gibson amwache Ally avae nguo.
MTUHUMIWA AJIPIGA FAINI
Baada ya vuta nikuvute iliyochukua muda wa saa 3, Ally alikiri kutenda kosa hilo na hivyo kuamua kujipiga faini mwenyewe kwa kusema atampa jamaa huyo mwenye mke kiasi cha shilingi milioni 30 kama fidia ya ugoni.
OFM ilimshuhudia Ally akiyaweka maelezo yake hayo kwenye karatasi na kuanguka ‘signecha’ huku akitazamwa na mashahidi wawili ambao nao walimwaga wino
Labels:
NEWS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment