Monday, 5 August 2013
PRIME MINISTER OF THAILAND, H.E YINGLUCK SHINAWATRA VISITS SERENGETI NATIONAL PARK
Hon. Ambassador, Khamisi S. Kagasheki, the Minister for Natural Resources and Tourism welcomes H.E Prime Minister of Thailand into Serengeti National Park
Prime Minister of Thailand, H.E Yingluck Shinawatra is in Serengeti National Park where by they have signed Memorandum of Understanding on National Parks and Wildlife Management and later in the afternoon game drive to witness the beauty of the park which is one of the seven wonders of the world.
Memorandum of Understanding on National Parks and Wildlife Management was signed between Minister for Natural Resources and Tourism on behalf of Tanzanian Government Hon. Ambassador, Khamisi S. Kagasheki and Deputy Prime Minister of Thailand, Hon. Plodprasop Suraswadi.
Misitu sehemu ya maisha inayotoweka
Kila sehemu ya Tanzania wakulima wanahangaika kuliko ilivyowahi kutokea,
wakishindana na mabadiliko ya hali ya hewa ili kulinda riziki zao na
usalama wa chakula, lakini huenda wasipate wasifaulu na kuidhibiti hali
hiyo.
Katika maeneo mengi ya vijijini wakulima wa Tanzania wana ufahamu wa
mabadiliko ya hali ya hewa yanavyotishia maisha yao, lakini hawana ujuzi
wa kutosha kuhifadhi mali asili ambazo ni muhimili wa shughuli zao za
kilimo.Taratibu za kienyeji ambazo zamani zilitumiwa kulinda ardhi na vyanzo vya maji, kwa mfano, wakati huu hazizingatiwi.
Viongozi wa vijiji wa siku hizi hawajali taratibu hizo wanapowaruhusu wawekezaji kufungua shughuli zao katika hifadhi za misitu. Maafisa utawala wengi katika wilaya na mikoa husema maneno matupu bila vitendo kuhusu masuala ya mazingira.
Hali inayofadhaisha zaidi, hata hivyo, ni pale ambapo maskini wanatumiwa na watu wenye tamaa ya mali kwa faida zao binafsi au wanajikuta wanalazimishwa na shinikizo la umaskini kufyeka misitu.
Misitu yafyekwa
Maeneo ya vyanzo vya maji hufyekwa kila siku na mito inakauka kutokana na miti inayokatwa kwa ajili ya mbao na uchomaji mkaa au uchimbaji wa mawe kwa shughuli za ujenzi.
Serikali za mitaa zinafahamu kabisa uporaji huu lakini mara nyingi hazina ujasiri wa kuzuia walafi ambao ndio wanasukuma uvunaji haramu wa misitu, uchimbaji mawe na biashara za mkaa ambazo hufanywa bila liseni.
Wakati ambapo viongozi wanadai kwamba taifa hili la Afrika Mashariki karibu lipate ustawi kiuchumi, hawatilii maanani athari zinazolikabili kutokana na mazingira.
“Tunao viongozi wengi wasio ona faida za mbali zitokanazo na mfumo wa ikolojia. Hawatambui kuwa chanzo asilia cha maji kikiisha haribiwa hakiwezi kuundwa upya,” alinieleza mhandisi wa maji mjini Morogoro – mji ambao miaka michache iliyopita ulisifika kutokana na mandhari yake ya mimea na majani yasiyokauka na vijito vilivyotiririka mwaka mzima.
Hata milima haiko salama
Mazingira hayo katika milima ya Uluguru ambayo iko karibu na mji wa Morogoro sasa yametoweka kutokana na kukosa uongozi wenye upeo wa kuona mbali. Na kadiri idadi ya wakazi wa mji huo inavyoongezeka, vilio vyao vya kutaka maji safi na udhibiti wa usafi pia vinaongezeka.
Wakoloni walitengeneza ramani za vyanzo vya maji na kuzuia watu wasiingilie maeneo hayo. Kwa mfano, utawala wa Kijerumani ulitengeneza ramani ya vyanzo vya maji ya mji wa Singida ulioko katikati ya nchi mwa 1910 ambapo ulikuwa haujapanuka zaidi ya kuwa kituo tu cha utawala.
Utawala wa Kiingereza ulifanya kazi hiyo hiyo kwa nchi nzima hadi miaka ya 1950.
Lakini badala ya kuimarisha utamaduni wa uwajibikaji katika jamii ili kulinda vyanzo vya maji na misitu, wenye madaraka katika Tanzania huru kwa miongo mitano iliyopita waliachia uharibifu uendelee kwa kasi isyo na kifani.
Kulingana na takwimu rasmi zilizopo, ambazo zinahitaji zitazamwe upya kwa umakini, misitu wakati fulani ilihifadhi asilimia 80 za vyanzo vya maji nchini na asilimia 60 za mabwawa ya kuzalisha umeme.
Ikolojia haipewi nafasi
Wakati hali halisi haiendi sawa na makadirio hayo, uwiano wa mifumo ya ikolojia katika sera za maendeleo haupewi msukumo wa kutosha kuondoa changamoto zinazoikabili nchi katika utoaji wa huduma za maji na nishati kwa wananchi.
Kampuni ya Umeme ya Tanzania (TANESCO) bado haina uwezo wa kufua umeme wa kutosheleza mahitaji ya watumiaji wa nishati hiyo.
Mamlaka za maji mikoani vile vile hazifanyi kazi kwa ufanisi kutokana ama na ukaukaji wa vyanzo vya maji au kukosa nishati ya kusukuma maji kwenda kwa watumiaji.
Kuni na mkaa ndicho chanzo kikubwa cha nishati inayotumiwa na watu wengi majumbani kwao mijini na vijijini.
Taarifa ya karibuni imeonesha kuwa asilimia 90 ya wakazi wa mijini nchini Tanzania hutumia mkaa zaidi ya nishati ya aina nyingine. Wauza mkaa wanayo mitandao yao ya kuupata na kuusambaza kote.
Miti inapofyekwa na kuisha eneo moja wanahamia mahali pengine na kuteketeza misitu iliyopo bila kujali kuwa misitu hiyo inastawisha mimea na viumbe wengine adimu.
Hakuna atakaye kuwajibika
Mpaka sasa hakuna mamlaka ambayo yameonesha kuwa na uwezo wa kudhibiti leseni au vibali vya ukataji miti ambapo ni dhahiri kuwa rushwa ndiyo inatawala mpaka hapo sera za kuhifadhi misitu ya Tanzania zitakapodhihirisha kuwa zina uwezo wa kutekeleza kazi hiyo.
Inashangaza kusikia kuwa TANESCO inataka bei za umeme zipandishwe kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo kila mtu angefurahi kuona matumizi ya umeme yanawafikia watu wote ili kuokoa misitu.
Uzalishaji mkaa ndio chanzo kikubwa cha kutoweka kwa misitu ya Tanzania lakini kampuni ya taifa ya umeme inajifanywa haioni tatizo hilo.
Kuongezeka kwa bei za umeme maana yake ni kwamba changamoto za mazingira zitaongezeka pia kutokana na uharibifu wa misitu, ikiwa pamoja na maporomoko ya ardhi wakati wa mvua, mabwawa yanayotumika kufua umeme yatajaa tope na mgao wa umeme utazidi mpaka hapo Tanzania itakapopata vyanzo vingine mbadala vya umeme usio na athari zozote.
Sera za Tanzania kuhusu mazingira na nishati hapana budi zilenge kuboresha na siyo kuongeza ukali katika maisha ya watu.
Mwandishi: Anaclet Rwegayura/DW Dar es Salaam
Mhariri: Mohammed Khele
SOURCE:DW.DE
TBS YAFUNGA VIWANDA VYA MIKATE MKOA WA DODOMA
Shirika la viwango Tanzania (TBS) limevifungia viwanda vitatu vya kutengeneza mikate mkoani Dodoma kutoka viwanda hivyo kutokuwa na ubora unaotakiwa kwa kanuni za kiafya. navyo ni Capital bakery. kizota bakery
World's first lab-grown burger to be tasted in London
Scientists were on Monday set to unveil the world's first lab-grown beef burger, serving it up fried to volunteers in London in what they hope is the start of a food revolution.
The 140 gramme (about five ounce) patty, which cost more than 250,000 euros ($330,000) to produce, has been made using strands of meat grown from muscle cells taken from a living cow.
Mixed with salt, egg powder and breadcrumbs to improve the taste, and coloured with red beetroot juice and saffron, researchers claim it will taste similar to a normal burger.
Professor Mark Post of Maastricht University, whose lab developed the meat, says it is safe and has the potential to replace normal meat in the diets of millions of people.
There are concerns that the growing demand for meat is putting unsustainable pressure on the planet, both through the food required for the animals and the methane gas they produce, which contributes to global warming.
"What we are going to attempt is important because I hope it will show cultured beef has the answers to major problems that the world faces," Post said ahead of Monday's event.
"Our burger is made from muscle cells taken from a cow. We haven't altered them in any way. For it to succeed it has to look, feel and hopefully taste like the real thing."
The team in the Netherlands took cells from organic cows and placed them in a nutrient solution to create muscle tissue. They then grew this into small strands of meat, 20,000 of which were required to make the burger.
In the world's first public tasting on Monday, the patty will be fried in a pan and served up to two volunteers.
Although it is very expensive, the costs of cultured beef are likely to fall as more is produced and the team claim it could be available in supermarkets within 10 to 20 years.
source:AFP
Wafuasi wa MDC wadai kushambuliwa na ZANU PF
Siku moja baada ya Rais Robert Mugabe na Zanu PF kutangazwa kushinda uchaguzi Mkuu nchini humo, baadhi ya wafuasi wa upinzani kutoka chama cha MDC wanasema wameshambuliwa na wenzao wa ZANU PF.
Baadhi ya dola za Magharibi ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, zimetilia shaka iwapo uchaguzi huo ulifanyika kwa uwazi.
Madai hayo yanakuja siku moja baada ya matokeo rasmi ya uchaguzi uliofanyika Jumatano kutolewa na kumpa ushindi rais Robert Mugabe. Chama chake Zanu-PF kilipata thuluthi tatu ya viti vya bunge.
Watu 11 mjini Harare na wengine 20 kutoka mkoa wa Mashonaland, wanasema kuwa walishambuliwa na wafuasi wa Zanu-PF wanaojulikana sana baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Chama cha MDC kimesemna uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya wizi wa kura.
Kiongozi wake Morgan Tsvangirai, ameahidi kuchukua hatua za kisheria kupinga matokeo ya uchaguzi.
Pia alisema kuwa chama chake cha MDC, hakitashirikiana na kile cha Mugabe na kuwa kitasusia kushikilia nafasi zozote katika taasisi za serikali.
Vyama hivyo viwili, vimekuwa wanachama wa serikali ya Muungano tangu mwaka 2009,baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 kusababisha ghasia.
Watu 11 waliodai kushambuliwa katika mtaa mmoja mjini Harare waliomba hifadhi katika makao makuu ya chama cha MDC mnamo Jumapili, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Brian Hungwe.
Wanadai kuwa walishambuliwa na wafuasi wa Zanu-PF waliokuwa wanakwenda nyumba hadi nyumba wakiwaamuru wafuasi wa MDC kufunga virago vyao na kuondoka.
Kiongozi wa chama cha MDC, Morgan Tsvangirai alisema uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya wizi.
Msemaji wa MDC, Douglas Mwonzora, alisema kuwa mashambulizi hayo yalipangwa. Lakini msemaji wa chama cha Zanu PF, Psychology Maziwisa, alikanusha madai kuwa wafuasi wa chama walikuwa wanawashambulia wapinzani wao.
MDC kinaonya kuwa hakitaweza kuwadhibiti wafuasi wake ikiwa madai ya wao kushambuliwa yataendelea.
Chama hicho kimeomba muungano wa nchi za Kusini mwa Afrika , Sadc, kuingilia kati na kuzuia hali kuzorota zaidi kiasi cha kutoweza jkudhibitiwa.
Baadhi ya wakuu wa chama cha MDC, wametoa wito kwa wafuasi wao kutoitii serikali na kutenga chama cha Zanu-PF.
SOURCE:BBC
Mahudhurio rasmi mkutano wa Mwigulu Nchemba jijini Dar es salaam
Mahudhurio yetu ya jana kwenye mkutano wa Mwigulu Nchemba yalikuwa hivi, tulikuwa 38 Jumla yaani watu wa iramba na waandishi wa habari na wapiga picha, viti ambavyo havikukaliwa vilikuwa 172. Nilimuuliza Meneja Ukumbi shilingi ngapi kasema Milioni 2, matangazo cloud fm pia yalitolewa hata kwenye FB, Wanafunzi wa Vyuo vikuu ndio tulikuwa wengi kama picha inavyoonekana. Nimesoma post moja watu wanalaumu gazeti la Tanzania daima, lakini lile limeonyesha jinsi tulivyokuwa wachache,
Subscribe to:
Posts (Atom)