Friday, 2 August 2013
Duru ya pili ya uchaguzi Mali
Uchaguzi wa Mali ambao umekuja kufuatia mapinduzi ya kijeshi pamoja na waasi kuteka sehemu ya Kaskazini mwa nchi, utakuwa na duru ya pili, kwa mujibu wa tangazo la serikali.
Hakuna mgombea aliyepata zaidi ya silimia hamsini ya kura zilizopigwa kudai ushindi.
Waziri mkuu wa zamani, Ibrahim Boubacar Keita na aliyekuwa waziri wa fedha, Soumaila Cisse watatoana kijasho katika duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika tarehe 11 Agosti.
Uchaguzi unanuia kurejesha demokrasia baada ya zaidi ya mwaka mmoja ya mgogoro wa kisiasa
KCB BANK WAFUTURISHA JIJINI DAR
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba (kulia), akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara (CCM) Philiph Mangula muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni mwenyekiti wa bodi ya KCB Benki Docta Edmund Mndolwa.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya KCB Moezz Mir akiteta jambo bna Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB jijini Dar es Salaam…
Tsvangirai is a cry baby: Mugabe
BULAWAYO — President Robert Mugabe yesterday mocked rival Prime Minister Morgan Tsvangirai, labelling him a cry baby and accused him of usurping the responsibility of Zimbabwe Electoral Commission (ZEC) by threatening to announce elections results.
BY NQOBILE BHEBHE
Addressing his campaign rally at White City Stadium, Mugabe said Tsvangirai planned to discredit the electoral process.
On Friday Tsvangirai lashed out at African Union (AU) Commission chairperson, Nkosazana Dlamini-Zuma for claiming that he had not raised any complaints over the alleged vote rigging by Zanu PF.
Zuma had said all the candidates she had met since arriving in Harare on Wednesday never mentioned any attempts by Zanu PF to steal the election.
Mugabe said Tsvangirai was opposed to elections.
“Listen to what the MDC-T leader says, he is opposed to everything, he is crying every day. Just now, Madam Zuma came from the AU, she is the chairperson of the commission, she listened to what other observers were saying and made a statement to say things are going on well,” said Mugabe.
“No, things are not going well says Tsvangirai, crying all the time. He did not want elections. Parliament expired on June 29 but he says no no no, let us continue, there are other outstanding issues so we cannot have an election. We can’t have an election, yet the constitution says we must have elections every five years. What sort of a leader are you?”
Mugabe said Tsvangirai does not obey the rules of the country.
“He said I am the one who will announce the election results. Have you ever heard any leader saying that? You will announce the election results as who?
“The law says election results will be announced by the Zimbabwe Electoral Commission. We as Zanu PF obey that. We must obey the law,” said Mugabe.
Mugabe said he was aware that one group within MDC-T had been assigned to work on tactics of undermining the election, create violence or raise objections and cry afterwards saying the process was not free and fair.
Mugabe refuted allegations that the electoral process hadbeen militarised.
Mugabe pledged to urgently look into the water crisis in Bulawayo saying the Mtshabezi pipe line would be “officially commissioned soon”.
However, the Mtshabezi pipe line was commissioned by Water Resources Development and Management minister Samuel Sipepa Nkomo last week.
Mugabe also lashed out at insensitive local authorities who are auctioning off houses for residents who owe money.
“What cruelty is that, we can’t have it? People owe yes, but give them a chance to pay. MDC-T says they don’t care, in fact that’s what they want,” said Mugabe.
Mugabe admitted that some people were starving and food relief was not reaching the rural areas.
source: http://www.thestandard.co.zw
Tanzania National Parks is 2013 SAG Award Winner
Environmental Sciences Research Institute (ESRI) recognized more than 170 organizations
during the Special Achievement in GIS (SAG) Awards ceremony at the Esri International User
Conference (Esri UC) in San Diego, California. The SAG Awards acknowledge vision,
leadership, hard work, and innovative use of Esri's Geographic Information Systems (GIS)
technology."The SAG Award identifies people and organizations that are using the power of
geography to improve our world and drive change," said Esri president Jack Dangermond. "At
Esri, we are deeply inspired by the passion and innovation of our users. They deserve recognition
for solving challenges and for their invaluable contributions to the continued evolution of
geographic science."
Various organizations worldwide were honored at the Esri UC which includes; Environmental
Management, agriculture, cartography, climate change, defense and intelligence, economic
development, education, government, health and human services, telecommunications, and
utilities industries. The SAG Awards ceremony was held at the San Diego Convention Center on
July 10, 2013.
Tanzania National Parks (TANAPA) was one of the organizations that received the 2013 SAG
award.SAG awards recognized the exemplary work performed by different users of Esri
technology, thus acknowledge the innovative and intelligent applications of GIS technology.
TANAPA has embarked on the implementation of an enterprise GIS making timely and relevant
geo-information available to a wide range of users. TANAPA established a GIS Unit and
invested in ArcGIS for Server, ArcGIS for Desktop and Trimble GPS technology to support the
integration of data from many sources and devices into a timely operational view of events and
activities in and around the parks. TANAPA will soon be able to collect, upload and synchronize
geo-information between all its parks and its headquarters in Arusha. The information collected
using this process will be helpful in delivering timely management decisions and thus effectively
improve park management on a daily basis.
By embracing Geographic Information Systems (GIS) technology, our organization have used
GIS to improve our world—and set new precedents throughout the GIS community. The SAG
Award ceremony presided over by Jack Dangermond, the President and founder of Esri. During
the reception, winners were invited to take pictures with Jack. Special Achievement in GIS
award are submitted by Esri staff from thousands of organizations worldwide, then personally
reviewed and selected by the Esri President.
DIAMOND! MWAMBIE ZITTO KABWE AFANYE SIASA AACHANE NA BONGO FLAVA"NEY WA MITEGO

Mfalme wa kudiss Tanzania, Nay wa Mitego amerejea tena kuchafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake mpya, Salam Zao.
Kwenye Salam Zao, Nay ameendeela kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.
Awamu hii list ya aliowadiss imeongezeka zaidi na kuingia pia kwenye siasa huku akiendelea kuwapa madongo wana hip hop wenzie.
Ameanza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay.
Nay wa Mitego ameendelea kuwadiss wana hip hip huku akiijita kuwa yeye ndio gangster rapper na anatengeneza hela huku wengine wakinuka vikwapa. Hakusita pia kuwarushia bombshell Weusi. “Yo Mchomvu wape salam ‘Kubumkubum’ waimbie watakufa njaa muziki umebadilika,” anarap Nay.
Nay pia amemdiss Zitto Kabwe kwa kurap:
“Word up Diamond, mwanangu wewe si mtoto wa Kigoma, mpe salama Zitto Kabwe mwambie afanye siasa aachane na Bongo Flava huku hatumtaki kabisa, maneno mengi, propaganda hajui kutekeleza, Kigoma Allstars tayari kawatelekeza.”
Rapper huyo pia amerap kuwa wapo watu waliojipatia utajiri kutokana na misiba ya Mangwea na Kanumba.
“Wanamiliki gari, wameota na vitambi kwa hela za rambirambi, mkizingua nawataja,”anasisitiza. Anasema tangu kifo cha Kanumba Bongo Movies imekufa na haiuzi tena.
Pia hajamuacha mwanzilishi wa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen kwa kudai kuwa licha ya kuwapa zawadi kubwa washindi, wameendelea kupigika mtaani.
“Hizi Salam ziende kwa madam Rita na Bongo Star Search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?! Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani, Haji Ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani.”
Source:Mpekuzi
Thursday, 1 August 2013
KAMPENI YA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo, burudani pamoja na michezo. Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.
Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.
Leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazindua kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 ni makosa.
Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania. Katika uzinduzi huu, Mamlaka imewaalika baadhi ya watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania walio wengi wanafaidika na mawasiliano. Miongoni mwao wako wamiliki wa blog mbalimbali, wasimamizi wa makundi mbalimbali katika mtandao wa FB na mengineyo.
Nia ya Mamlaka ni kuomba ushirikiano kwao ili waweze kushiriki katika kampeni hii na kuwahamasisha mashabiki wao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kunufaisha Taifa letu kwa matumizi mazuri. Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Tunawasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania
31 Julai 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)