Ushindi wa kwanza Hamilton kwa Mercedes.
 
Dereva wa magari ya Timu ya Mecedes Lewis Hamilton ameweza kuishindia
 timu yake ushindi wake binafsi wa kwanza kwa Mercedes kwa kuongoza 
tangu mwanzo na kuwazidia madereva wenzake kwenye mashindano ya Hungary 
ya mbio za magari ya Langalanga au Formula 1.
Hamilton alijituliza na kutumia kasi akiwashinda
 dereva Kimi Raikkonen wa Timu ya magari ya Lotus aliyemaliza wa pili na
 Sebastien Vettel wa Red Bull aliyemaliza wa tatu.
                     
Mark Webber wa Red Bull alionyesha 
umahiri wake kwa kujikwamua kutoka nafasi ya kumi alikoanzia mashindano 
hadi kumpiku dereva moto moto wa Timu ya magari ya Ferrari, Fernando 
Alonso.
                     
Kutokana na hali hio Raikkonen sasa anapanda kwa
 pointi moja mbele ya Alonso akishika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi
 alizokusanya tangu kuanza kwa mashindano ya msimu huu wa 2013/2014 
ingawa bado yuko nyuma ya kiongozi wa mashindano na mtetezi wa taji 
Sebastien Vettel kwa pointi 38.
                     
Kwa kipindi kirefu cha mashindano haya Fernando 
Alonso alikua katika jitihada za kuzuia asipitwe na Romain Grosjean wa 
timu ya Mercedes, na katika pilikapilika Romain Grosjean, alijitia 
matatani na kuadhibiwa kwa kupita gari akizunguka nje ya uwanja.
                     
Wakati huo alimpita Felipe Massa wa Ferrari 
kwenye mzunguko wa 29 kituo cha nne, ambapo tairi zote nne zilivuka 
msitari mweupe unaobainisha uwanja na papo hapo kupewa adhabu ya 
kuuzunguka uwanja.
                     
Hapo jana baada ya Hamilton kushinda nafasi ya 
mbele ya kuongoza mbio za leo alisema kua utakua muujiza endapo 
atashinda ikizingatiwa hali ya joto kali nchini Hungary bila kusahau 
matatizo yaloikumba timu ya magari ya Mercedes kwa matairi kupasuka kila
 mara.
                     
Lakini alidhibiti mashindano kwa mda wote 
akipoteza uongozi kwa Grosjean na baadaye Mark Webber aliposimama 
kubadili tairi na mafuta lakini aliweza kurudi kileleni pale Webber 
aliposimama kubadili tairi na mafuta.
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment