 
  
                        Mbunge wa Kinondoni-CCM, Iddi Azan
Mbunge
 Wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania kutoka jimbo la 
Kinondoni, inasemekana ametajwa na wafungwa wa kitanzania waliofungwa 
jela huko nchini Hong Kong kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Taarifa
 hiyo iliyomhusisha Mbunge huyo na mtandao huo mkubwa wa biashara hiyo 
ya madawa ya kulevya nchini Tanzania, ilitolewa katika barua maalum 
iliyoandikwa na mmoja wa Wafungwa katika magereza ya nchini Hong Kong 
ambapo inasemekana kuna wafungwa wa kitanzania wanaofikia 200.
Kati
 ya hao wafungwa 200 waliopo magerezani na vizuizini, 130 tayari 
wameshahukumiwa na 70 bado wanasubiri kesi zao kutajwa. Kuanzia Mwezi wa
 Tano mpaka wa Sita mwaka huu wa 2013, tayari Watanzania wapatao 50 
wameshakamatwa na madawa ya kulevya wakati wakijaribu kuingia katika 
viwanja vya ndege vya nchi za China na Hong Kong.
Mbali
 na Hong Kong, pia kumekuwepo na taarifa mbalimbali za raia wa Tanzania 
ambao wamekatwa na madawa ya kulevya nchini Afrika ya Kusini na 
kwingineko duniani. Mmoja kati ya waliokamatwa na madawa hayo ni 
mwanadada mahiri wa Kitanzania ambaye alikuwa mrembo katika video 
mbalimbali za Bongo Flava anayeitwa Agnes Gerald au kama anavyojulikana 
na wengi kwa jina la Masogange.
Waraka
 huo wa mfungwa huyo wa Kitanzania pia umeorodhesha idadi kubwa ya 
wafanyabiashara wengine nchini Tanzania ambao ni wahusika wakubwa katika
 biashara hii haramu ya madawa ya kulevya.
Madawa
 hayo ya kulevya yanasemekana yanaingizwa nchini Tanzania kwa wingi kwa 
njia ya meli na boti mbalimbali yakitokea katika nchi za Pakistan, 
Afghanistan na nchi nyingine za Mashariki ya mbali.
Ni
 muhimu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha 
kampeni kubwa ya kuwakamata wahusika wote katika biashara hii na 
kuwafikisha katika vyombo vya sheria, athari za madawa hayo zimezidi 
kuonekana sehemu mbalimbali nchini Tanzania na dunia nzima.
Soma barua iliyowataja wafanyabiasha hao wakubwa wa madawa ya kulevya nchini Tanzania hapo chini.
SOURCE:Bongo celebrity




 
  
No comments:
Post a Comment