Uongozi wa klabu ya Yanga leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu ya urushwaji wa michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha luninga cha Azam ambacho kimeingia makubaliano na kamati ya Ligi Kuu kuonyeshwa michezo yote ya ligi kwa kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea 
na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amesema 
uamuzi wa kamati ya ligi kuingia mkataba na kituo cha Azam Tv bila ya 
kuwashirikisha wahusika wenyewe ambao ni vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi kama 
klabu ya Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona taratibu za
 kupewa haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa, sisi viongozi
 wa kalbu ya Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo hivyo tukaona 
ni vema tuje kwa vyombo vya habari tuulezee umma juu ya maazimio ya 
kamati ya utendaji.
Ifuatayo ni taarifa kamili kwa vyombo vya habari: 
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi 
karibuni, Tanzania Football Federation (TFF)  iliunda Tanzania Premier 
League chini ya Bodi ya mpito Bodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo
 Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake 
kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam 
Television (ambayo ina  mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football 
Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam 
Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika
 misingi ifuatayo:
1. BODI YA TPL
1.1 Bodi
 iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi 
iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe  ……….. mwaka 
huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia
 kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA
2.1 Haijawahi
 kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu 
inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo 
zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani. 
2.2 Mfumo
 (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha 
mkataba kwa YANGA iachie  urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na 
Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya 
Tanzania.
2.3 Makubalianokati
 ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba 
Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya 
Tanzania  watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, 
ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye 
ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya 
timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.
2.4 Kamati
 ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato 
ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho
 katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa: 
2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi; 
2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama; 
2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.
3. MIGOGORO YA MASLAHI
3.1 Makamu
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa 
Makampuni ya Azam na  kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL 
na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2 Makampuni
 ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya 
utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka 
“matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira  wa miguu, kama vile Azam 
F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na 
msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya
 mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa
 YANGA.
3.3 Azam
 na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA 
alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya 
Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama 
Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.
4. KUTOKUWA NA UWAZI
4.1 Mkataba
 wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao 
badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya
 habari,  na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu
 fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za
 kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).
4.2 Ukosefu
 wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na 
TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA
 kufanya ombi hilo kwaTPL.
5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA 
5.1 Mamlaka
 ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu 
(Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. 
TPL inasingizia  kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya 
kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, 
stock and barrel."
5.2 TPL
 inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji  wa mchezo ya 
mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya 
udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu 
urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi
 ya uhusiano na hivyo 
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa mfano,
 moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya 
mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa 
michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA  Dar es
 Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila 
mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za 
YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni
 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya 
TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma 
kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau 
wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji)  walikuwa wanaafikiana 
kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya 
Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara 
yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo 
makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya 
Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo 
wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA 
linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu 
vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam 
Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo 
wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
......................
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013
 
 
  
 
 
  



 
 

