Monday, 29 June 2015

Waangalizi wa UN Burundi wamefuatilia uchaguzi

 

Uchaguzi wa Bunge na serikali za mitaa ulifanyika jana nchini Burundi, licha ya shinikizo la jamii ya kimataifa la kutaka uahirishwe kutokana na mazingira ya kisiasa na kiusalama.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kufuatilia uchaguzi nchini Burundi, MENUB umesema waangalizi wake 36 wamefanikiwa kufuatilia uchaguzi bila kutishiwa usalama wao.
Msemaji wa MENUB Vladimir Monteiro, akihojiwa jana, alisema waangalizi wa MENUB wametembea kwenye majimbo yote ya Burundi ili kufuatilia utaratibu huo na kuandaa ripoti kwa ajili ya Katibu Mkuu na Baraza la Usalama.

Serikali ya Burundi ilishikilia msimamo wake wa kufanya uchaguzi jana tarehe 29 Juni, kinyume na mapendekezo ya timu ya uhamasishaji iliyohusisha Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda, ya kuhairisha uchaguzi hadi Julai, tarehe 30.

Monteiro ameeleza msimamo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuhusu uamuzi huo.Ameongeza kuwa Katibu Mkuu amesikitishwa kwamba mapendekezo ya timu ya uhamasishaji kuhusu kuhairishwa kwa uchaguzi hayakusikilizwa, lakini kwamba anaendelea kuwaomba wadau wa Burundi waendelee kufanya kazi ili kupata suluhu kupitia mazungumzo, bila ghasia.

Polisi wampiga vibaya Mwandishi wa Habari Zanzibar





Mwandishi wa Habari kwa jina Omar Ali mzaliwa wa Mkoani Kangani kisiwani Pemba, jana mida ya asubuhi ameshambuliwa na kupigwa vibaya sana na jeshi la Polisi Zanzibar na kutupwa maeneo ya Maisara mjini Zanzibar.

Mwandishi huyu alikuwa anachukua habari kutoka kituo cha uandikishaji dafatari la kudumu maeneo ya Migombani Zanzibar na polisi hao inasadikiwa walisema ni mwandishi wa Chama cha Wananchi CUF na ndipo walipomshika na kuanza kumpiga vibaya sana na kumvunja miguu kama anavyoonekana kwenye picha akiwa hospital mahutui miguu ikiwa imevujika.

Ikumbukwe:
Matukio haya yanakuja baada ya wananchi wa Zanzibar kuhakikisha kila kituo hawezi kuandikishwa mtu ambaye hahusiki kama ambavyo tumeona na kuskia kupitia vyanzo mbali mbali mpango wa CCM kupeleka mamluki visiwani Zanzibar kujiandikisha kwaajili ya kukiokoa Chama cha Mapinduzi hasa Zanzibar ambako kuna kila dalili kungoka madarakani Oktoba mwaka huu.

Wema Sepetu: Siwezi kumsapoti Diamond kwenye MTV Awards, nitaonekana ninajipendekeza



Katika Kipindi cha TV cha Wema Sepetu Kiitwacho In My Shoes Wema Usiku huu wa Leo Amedai kuwa hawezi Kumsapoti Mwanamuziki Diamond kwenye Tuzo za Mtv Awards kwa vile Kufanya Hivyo ataonekana anajipendekeza kwa vile Diamond hajawahi kumuomba kufanya hivyo...

Pia amedai kuwa yeye na Diamond walishayamaliza hivyo hataki kujihusisha na Diamond kwa njia yoyote ile kama ni kosa alishalifanya kipindi cha nyuma na hawezi rudia kosa..

Katika hatua nyingine Wema Sepetu amedai kuwa Kitendo cha yeye kumsapoti Ali Kiba katika tuzo za Kill Music kilikuja baada ya Ali Kiba yeye Mwenyewe Kumuomba Wema Kufanya Hivyo na kumtumia picha ambazo alizipost kwenye Account yake ya Instagram.

Taharuki Kampala eti Mbabazi anarejea leo

Taharuki imetanda mjini Kampala Uganda baada ya habari kuenea kuwa mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni ,aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi anarejea leo.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa polisi wametumwa katika barabara ya kutoka Kampala hadi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.
Bwana Mbabazi anasemekana kuwa anarejea kutoka kwa ziara ya kimataifa iliyompeleka Uingereza na Marekani.
Wafuasi wake wamepanga kumkaribisha kwa shangwe na vigelegele.
Yamkini wamepanga kuwa na msafara wa magari yaliyojaa wafuasi wake kumkaribisha.
Amama Mbabazi alitangaza majuma mawili nia ya kushindana na rais Muuseveni kuwania uwenyekiti wa chama cha National Resistance Movement na hatimaye kuwania kiti cha urais.
Wawili hao walikuwa washirika wa karibu kwa zaidi ya miaka 40 .

Rais Museveni ametawala Uganda tangu mwaka wa 1986 na anatarajiwa kuwania urais kwa muhula wake wa nne.
Museveni alimfuta kazi bwana Mbabazi mwaka uliopita katika hatua iliyotafsiriwa na wachanganuzi wa kisiasa nchini humo kuwa mbinu ya kukandamiza mpinzani wake mkuu.
Bwana Mbabazi anakabiliwa na changamoto kubwa ya kushinda uteuzi katika chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).
Rais Museveni tayari ameidhinishwa na kamati kuu ya chama japo anahitaji kupokea ithibati ya wanachama katika mkutano mkuu wa wajumbe.
Iwapo atakonga nyoyo za wajumbe wa NRM sasa Mbabazi sasa atawania urais dhifi ya Museveni
Mwandishi wa BBC Rachael Akidi anasema kuwa hii ndiyo itakayokuwa mtihani mkubwa zaidi kuwahi kumkabili rais Museveni ndani ya chama cha NRM.

Makamu wa Pili wa Rais Burundi akimbia nchi



Makamu wa Pili wa Rais wa Burundi, amemshambulia vikali Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo na kukimbia nchini akimlaumu Nkurunziza kwa kutaka kuendelea kubakia madarakani kinyume cha katiba. Inaaminiwa kwamba hivi sasa Gervais Rufyikiri amekimbilia nchini Ubelgiji kuomba hifadhi ya kisiasa. Ofisi ya Rais wa Burundi imeviambia vyombo vya habari kuwa Rufyikiri alitumwa kwa kazi maalumu huko Ubelgiji siku chache zilizopita kabla ya kurejea nyumbani na baadaye kutoroka nchini humo. Jana Jumatano Rufyikiri aliiambia kanali ya televisheni ya France 24 kwamba anapinga kile alichokiita jaribio la rais la kuwania urais kwa mara ya tatu "kinyume cha sheria." Burundi imetumbukia kwenye machafuko ya kisiasa tangu mapema mwaka huu baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kugombea urais kwa kipindi cha tatu. Jambo hilo limezusha machafuko nchini Burundi hususan jijini Bujumbura yaliyoambatana na jaribio lililoshindwa la mapinduzi. Tarehe 13 Mei mwaka huu, baadhi ya maafisa wa kijeshi wa Burundi walifanya jaribio la mapinduzi, lakini walishindwa nguvu na maafisa watiifu kwa Rais Nkurunziza.

UK’s Prince Harry to work in Tanzania

Dar es Salaam. Prince Harry of UK is to embark on a three-month assignment in Africa, working in the area of conservation in Tanzania, South Africa, Namibia and Botswana.

Harry’s father Prince Charles and elder brother Prince William organised a major conference, in London, on the illegal wildlife trade in February 2014, aimed at saving endangered species like rhinos, tigers and elephants from poachers.

President Jakaya Kikwete attended the conference during which support was galvanized to boost Dar’s own war with poachers who are now thought to have decimated up to 60 per cent of the country’s elephant population.

Prince Harry’s itinerary in Tanzania is yet to be made public but it is believed that he will join one of the several ongoing campaigns under the government and private organisations toPROTECT elephants in the Selous National Park from poachers.

The BBCREPORTED on Friday that in southern Africa, the Prince will be involved in “front-line conservation projects,” having developed a programme with conservation experts, including those from the Zoological Society of London (ZSL). The same organisation works in Tanzania.

He will learn about environmental education programmes as well as working “at the sharp end of wildlifePROTECTION,” joining rangers who respond to reports of poaching attacks on elephants and rhino, and spending time with vets who try to save animals after attacks, BBC reported.

Jonathan Baillie, director of conservation programmes at ZSL, said: “After this period, Prince Harry will be one of the best-informed ambassadors for the conservation community on what is really happening on the ground in Africa. His experience will be of great value.”

Harry who is fifth-in-line to the throne is understood to be leaving for Africa next week.

His trip to the continent comes on the backdrop of his ending of a decade-longCAREER with the Army, according to Kensington Palace.


CITIZEN

Faiza:Sugu Amedanganya Bunge Kuhusu Matunzo ya Mtoto





Mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi, Faiza Ally jana amesema 'Sugu' alidanganya Bunge alipodai hutoa sh.500,000 kila mwezi za matunzo ya mtoto.

Na ingawa Sugu alidai bungeni pia kuwa hulipa ada ya sh. milioni tatu kwa mwaka kwa ajili ya elimu ya mtoto huyo, Faiza amedai ni kwa nusu ya pili tu ya kipindi cha miaka miwili ambayo amekuwa akisoma.

Aidha, mwanamitindo Faiza amesema hayupo tayari kumaliza kifamilia mvutano wa malezi ya mtoto na 'Sugu', kama Mbunge huyo alivyoeleza bungeni juzi.

Akizungumza katika chumba cha habari cha Nipashe jijini jana, Faiza alisema 'Sugu', mwanamuziki wa hip hop pia, hutoa sh.500,000 za matumizi ya mtoto lakini si kila mwezi.

"Bahati nzuri fedha hizi huwa anazituma kwa njia ya simu, kuna rekodi ya miamala (itathibitisha)... hatumi kila tarehe moja kwa mfano," alisema.
"Katika miezi sita iliyopita? Katika miezi sita iliyopita ametuma si zaidi ya mara nne."

Faiza alisema Mbunge wa Mbeya Mjini huyo alianza kulipa ada ya shule hivi karibuni, lakini mtoto huyo wa miaka miwili na miezi nane alianza kusoma akiwa na mwaka mmoja na miezi saba.

Kuhusu nia ya Sugu ya maridhino, Faiza alisema "haya mambo hayataisha kifamilia.

"Kama angekuwa anataka suluhu ya kifamilia kama alivyodai bungeni, wazazi wangu anawajua. Wazazi wake na ndugu zake wote nawajua, hakuwahusisha akakimbilia mahakamani.

"Siwezi. Acha haya mambo tukaamuliwe na mahakama (ili) haki itendeke."
Faiza anakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo Manzese kumpa 'Sugu' haki ya kuishi na mtoto.

Mahakama ilimpa 'Sugu' haki hiyo baada ya Mbunge huyo kuonyesha hofu ya mtoto kukosa malezi mema kutoka kwa mama yake kutokana na mapenzi ya Faiza katika mavazi mafupi, ikiwemo pedi za wagonjwa au wazee, na nguo ziachazo wazi sehemu kubwa ya mwili.

Faiza amesema ingawa Sugu anamtuhumu kukosa maadili kwa sababu ya mavazi mbunge huyo amewahi kutolewa kwa nguvu bungeni na kurekodi CD zenye matusi za 'Anti Virus', vitendo ambavyo ni picha mbaya kwa mtoto siku za usoni.

Faiza alikutana na Sugu kupitia mtandao wa kijamii wa 'facebook' 2011 na aliondoka nyumbani kwa Mbunge huyo "baada ya kushindwa"; Januari mwaka jana, alisema.

Nipashe,28/06/2015