Sunday, 12 July 2015
Msako mkali Mexico wa muuza mihadarati
Mamlaka ya nchini Mexico limeanza msako mkali wa kumtafuta Joaguin Guzman gwiji la biashara ya madawa ya kulevya duniani, kufuatia kutoroka kwake katika gereza lenye ulinzi mkali mwishoni mwa wiki.
Helikopta za Blackhawk ambazo zimeonekana kuruka juu gerezani Altiplano magharibi ya Mexico City mahali alipokuwa ameshikiliwa huku ndege zote zikiwa zimezuiwa kuruka karibu na Uwanja wa ndege.
Wafanyakazi wa magereza wanahojiwa baada kubainika kuwa Joaguin alitoroka kupitia njia ya nchini ya ardhi yenye urefu wa kilomita moja na hii ni mara ya pili kutoroka.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Marekani, Loretta Lynch, ametoa msaada wa kumkamata Guzman ambae pia hujulikana kama ' El Chapo ' .
Van Persie atua Uturuki
Mashabiki wa manchester United wengi
walijua kuwa Van Persie anaondoka kuelekea Fenabashe lakini kwa mtoto
mdogo mwingereza wa miaka minne Louis Diamond hakufahamu kuwa kipenzi
chake Robin Van Persie anaondoka mpaka pale alipoambiwa na wazazi wake
kwamba mpachika magoli Robin alikuwa tayari kuelekea uturuki. Hivi sasa
waturuki wameanzisha kampeni ya kuchangishana pesa ili mtoto huyo ambaye
video yake imesambaa mitandaoni na kutizamwa na watu wengi aletwe
Uturuki kumshuhudia mchezaji huyo.
Shabiki huyo mdogo wa miaka
minne alipoambiwa na wazazi wake kuwa Van Persie alirekodiwa na baba
yake akilia sana na video yake imesambaa mitandaoni duniani kote."hatujamwambia kama video yake imesambaa duniani, tumemwambia tu kuwa tumewaonyesha marafiki zake tu hapa mtaani tu hajui kama ni dunia nzima, mimi na mke wangu tuna hamu ya kumwona atakavyocheka tukimwonyesha video hii miaka kumi baadaye" Alisema baba wa mtoto huyo.
Kuna uwezekano pesa iliyopangwa kuchangwa mashabiki wa uturuki ikazidi kiwango cha pauni 1200 za uingereza kilichokusudiwa kumsafirisha mtoto huyo na baba yake ili kuja kushuhudia mechi ya kwanza ya Van Persie nchini uturuki.
Ni vema pia mtoto akapozwa kwa kuambiwa kuwa kinakuja chuma kipya kutoka southampton, Morgan Shineidelini ambaye atafanya vipimo Man U.
Kwa upande mwingine Liverpool inachukua kitita cha pauni milioni 49 kumuuza Raheem Sterlin kuelekea Man City na kumfanya kijana huyo mdogo wa miaka 20 kuwa mchezaji wa ghali zaidi katika england.
Saturday, 11 July 2015
Maneno 36 ya Waziri Membe Kuhusu Mtu Aliyekamatwa na Mabilioni ya Wajumbe Dodoma..
Kuna stori zimeenea mitandaoni kwamba kuna mtu ambae amekamatwa na mabilioni ya pesa Dodoma, kingine ni kwamba amekamatwa na simu ikiwa na maelekezo kwamba pesa hizo ni za kuwapatia Wajumbe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameandika ujumbe @Twitter kukanusha kuhusika na mtu huyo
- “Kuna taarifa za uongo zinazoenezwa kwamba kuna “Mtu wa Membe” amekamatwa na pesa Dodoma“
Kwenye Tweet nyingine Waziri Membe ameandika hivi
- ”siasa hizi ni za hovyo kwani hazitajenga Taifa letu. Naomba msihadaike na watu wanaotaka kututia doa baada ya kukosa uchafu dhidi yetu” @BernardMembe
Mtoto aliyekosha ulimwengu kwa ari yake
Mtoto aliyepigwa picha akidurusu
usiku nje ya mkahawa wa McDonald huko Ufilipino amevutia hisia kali ulimwenguni
kote kwa ari yake ya kupata elimu.
Mwanafunzi wa Uuguzi bi Joyce
Torrefranca, ndiye aliyeipiga picha hiyo nje ya mkahawa huo wa McDonald ulioko
katika mki wa Cebu nchini Ufilipino na akaichapisha kwenye mtandao wake wa
kijamii wa Facebook na ujumbe
Mtoto aliyekosha ulimwengu kwa ari
yake
''mtoto huyo amenikumbusha niwekee
bidii maishani''
Katika picha yake bi Torrefranca
mtoto mwenye umri wa miaka 9,Daniel Cabrera amejikunyata kwenye kibao
anachokitumia kama meza akifanya mabaki ya kazi aliyopewa shuleni.
Mtoto huyo Cabrera anatumia mwangaza
wa bango la kutangaza duka la McDonald kama taa yake akidurusu !
''kwangu mimi kama mwanafunzi
,nilipigwa na mshangao kutokana na ari ya mwanafunzi huyu mdogo aliyekuwa
amechutama akikamilisha kazi yake ya shuleni bi Torrefranca aliiambia runinga
ya ABS-CBN katika mahojiano.
''kwa hakika ilinipatia changamoto kubwa
niendeleee kufanya bidii katika kila jambo linalonikabili''
Muda mchache baada ya bi Torrefranca
kuchapisha picha hiyo kwenye Facebook maelfu ya watu waliichapisha pia wakisema
kuwa ilikuwa imewavutia sana.
''Ukitaka kitu ama ukitaka
kufanikiwa maishani sharti itie bidii katika kila jambo unalokabiliwa
nalo,hivyo utapiga umaskini teke'' alisema bi Torrefranca.
Bi Joyce Torrefranca akihojiwa
katika moja ya runinga ya taifa
Alipohojiwa kijana huyo Daniel
alisema kuwa aligundua babake mzazi alichomwa moto hadi kufa katika ajali
mbaya.
Kakake mwengine ni mgonjwa sana
alisema Daniel.
Kijana anasema kuwa yeye hulazimika
kupiga buku nje ya mkahawa huo wa McDonald kila usiku akimsubiri mamake
akamilishe wajibu wake katika mkahawa ulioko karibu.
Afisa wa serikali anayeshughulikia
maslahi ya watoto tayari ameitembelea familia ya Daniel kwa nia ya kuwapa
msaada wa kujinasua kutoka kwa minyororo ya Umaskini.
Kwa upande wake vyombo vya habari
vimekuwa vikimmiminia sifa kochokocho bi Torrefranca kwakuangazia masaibu yanayomkabili
kijana daniel.
Man United kumsajili Matteo Darmian
Kocha wa kilabu ya Manchester United
Louis Van Gaal amethibitisha kuwa beki wa kilabu ya Torino Matteo
Darmian atafanyiwa ukaguzi wa matibabu kabla ya kuhamia kilabu hiyo kwa
pauni milioni 12.9.
Mshambuliaji wa Manchester united Robin Van
Persie tayari anaendelea na mazungumzo na kilabu ya Fenerbahce na Van
Gaal anasema:Iwapo tutahisi anaendelea vyema tutasema,lakini kufikia
sasa hatuna hisia hiyo.Kuhusu uhamisho,aliongezea:''Nilisema mwishoni mwa msimu uliopita kwamba ununuzi wa wachezaji na uuzaji ni hatua.Hatua hiyo huendelea hadi mwezi Septemba.''Naona kama uhamisho huo unachukua mda mrefu.Nimesema hivyo mara nyingi.hatahivyo tunaendelea vyema''.
Friday, 10 July 2015
Mugabe: “Even satan wasn’t Gay, he chose to approach naked Eve instead of naked Adam.”
“Even satan wasn’t Gay, he chose to approach naked Eve instead of naked Adam.” – President, Mugabe on homo sexuality.
Following the legalization of gay marriage across America by the Supreme Court last week, Zimbabwean president Robert Mugabe, who is known for his extreme anti-gay views has been making headlines.
Earlier this week was a marriage proposal to president Obama and yesterday, he allegedly said what you see below during another interview;
Subscribe to:
Posts (Atom)






