Thursday, 9 July 2015

Nassari Afunguka.......Asema Ajali ya Helikopta Aliyopata ni ya Kishirikina, Ndesamburo Asema Atanunua Nyingine


Wakati Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akisema anashindwa kuamini kilichotokea na kunusurika katika ajali ya helikopta juzi, mmiliki wa chopa hiyo, Philemon Ndesamburo amesema atanunua nyingine haraka kabla ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu. 

Kauli hizo zilitolewa jana ikiwa ni siku moja baada ya helikopta hiyo inayomilikiwa na Ndesamburo kupitia kampuni yake ya Keys Aviation kupata ajali wakati ikitumiwa na Nassari na baadhi ya viongozi wa Chadema.
 
Wakati ikipata ajali, ilikuwa imekodishwa na Kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd inayomilikiwa na Kapteni William Slaa.
 
Katibu wa Ndesamburo, Basil Lema alisema ilipata ajali baada ya kupigwa na kimbunga wakati anga likiwa limefunikiwa na wingu zito.
 
“Mheshimiwa Ndesamburo amemshukuru Mungu kwa kuwanusuru watu waliokuwa kwenye ndege hiyo ambao ni pamoja na Mbunge Joshua Nassari.
 
“Ameweka wazi kwamba atalazimika kununua nyingine mapema kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu,” alisema Lema akimnukuu Ndesamburo.
 
Lema alisema rubani aliyekuwa akiendesha helikopta hiyo alifanikiwa kuielekeza juu ya miti alioutumia kupunguza kasi ya kushuka chini na kusaidia abiria kutoka salama.
 
“Imeharibika lakini abiria wote ni wazima. Walikuwamo wanne,” alisema na kuongeza kuwa helikopta hiyo ndiyo iliyotumiwa na Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana na chama hicho kilitegemea kuitumia katika Uchaguzi Mkuu ujao.
 
Pia, imewahi kutumiwa na makada mbalimbali wa CCM akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba na kada maarufu wa Moshi mjini, Buni Ramole.
 
Kauli ya Nassari
Akizungumza na waandishi wa habari katika wodi alikolazwa kwenye Hospitali ya Seliani – Arusha, Nassari alisema waliporuka kutoka Leguruki, hakukuwa na dalili zozote za kuchafuka kwa hali ya hewa, lakini dakika chache baada ya kuruka angani wingu zito lililoambatana na upepo mkali liliwafunika ghafla.
 
“Wingu lile na upepo ule sijawahi kuona katika maisha yangu yote zaidi ya kusoma kwenye vitabu vya simulizi vya mambo ya ushirikina. Namshukuru Mungu wote tuko salama kwani hatukuwa na matumaini ya kupona ajali ile,” alisema Nassari.
Mbunge huyo aliyekuwa katika ziara ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura, alimwagia sifa rubani Slaa kwa uwezo na ustadi aliouonyesha hadi wakanusurika.
 
“Kama siyo ustadi wake, naamini watu wangeokota vipande vya nyama tu kwenye eneo la ajali, ila Mungu ni mkuu leo tuko hai wote licha ya madhara madogo,” alisema.
 
Nassari alisema muda mfupi kabla ya kuruka saa kumi na moja jioni, wakati akihutubia mkutano huko Leguruki, alipokea simu kutoka kwa mchungaji mmoja akimtaarifu kupata maono kuwa anakabiliwa na hatari ya kukutwa na jambo kubwa na baya akimtaka adumu katika sala.
 
“Dakika 15 baadaye nikaruka na kupata ajali. Naamini kilichotuokoa ni nguvu ya sala niliyosali baada ya kupokea ujumbe wa mchungaji na maombi ya wachungaji wangu wanaoniombea kila siku,” alidai Nassari.
 
Rubani Slaa alisema alishangaa lilipotokea wingu na upepo uliosababisha ndege kuanguka ikiwa njiani kuelekea Ndoombo na Ngureserosambu.
 
“Kabla ya kurusha ndege nilijiridhisha na hali ya hewa. Hakukuwa na kiashiria chochote cha hali ya hatari kama maeneo mengine ambako tulishindwa kutua kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha."
 
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Seliani, Dk Paul Kisanga alisema hali za majeruhi si mbaya, isipokuwa Eva Kayaha aliyevunjika mbavu mbili.

Friday, 3 July 2015

Msekwa Amjibu kauli ya Nape

Haiwezekeni mchezaji makini aliejindaa kwa mechi afunge bao kwa mkono. Goli kama hilo litafutwa na refa. Naomba wananchi wapuuzie maneno ya upuuzi kama hayo.

Kufunga goli la mkono ni faul na moja kwa moja litakataliwa na refa ambayo ni Tume ya Uchaguzi. Kauli mbaya kama hizo zinaweza kufanya Wananchi kukosa imani na Serikali na kuleta machafuko na ninaamini haya ninayoyasema ndio msimamo wa chama changu.

Pius Msekwa.2.07.2015 (ITV, kipindi cha Mzelendo).

Wednesday, 1 July 2015

Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Tarehe 2 July 2015


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru Kada wa CCM Rajabu Maranda na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na kesi wizi wa Sh milioni 207 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Jopo la mahakimu watatu likiongozwa na Hakimu John Utamwa, Ignas Kitusi na Eva Nkya liliwaachia washitakiwa hao baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa hao.

Mbali na Maranda washitakiwa wengine walioachiwa huru ni Farijala Hussein na waliokuwa wafanyakazi wa BoT, Ester Komu, Bosco Kimera na Imani Mwakosya.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Utamwa alisema washitakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka manne kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo BoT na wiziwa Sh milioni 207.2 wako huru kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka hayo bila kuacha shaka kama inavyotakiwa kisheria.

Alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuithibitishia mahakama jinsi Maranda na Farijala walighushi makubaliano ya kukusanya deni kati ya Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ya Tanzania.


Katika hukumu hiyo iliyosomwa bila Mwakosya kuwepo mahakamani, Hakimu Utamwa alisema upande wa Jamhuri wameshindwa kumleta mpelelezi wa kesi hiyo ili aweze kuithibitishia Mahakama saini ambazo zinadaiwa kuwepo katika makubaliano hayo hivyo udhaifu huo hauwezi kuwatia washitakiwa hatiani.

Aliongeza kuwa, upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha shitaka la kughushi, kwa hiyo shitaka la kuwasilisha nyaraka za uongo litakuwa limekufa,kwa sababu wameshindwa kuonesha kweli nyaraka ni za kughushi.

Aidha alisemwa wameshindwa kuonesha ni jinsi gani fedha hizo zilihamishwa kama wanavyodai kuwa mchakato huo ulifanikiwa kwa sababu Maranda na Farijala walitumia nyaraka za kughushi.

“Hakuna shahidi aliyeweza kutoa ushahidi ukaenda sawa na hati ya mashitaka iliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya washitakiwa,” alisema Hakimu Utamwa.

Nyaraka zinazodaiwa kughushiwa ni hati za makubaliano ya kuhamishiwa deni kutoka Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ya nchini Tanzania, ambazo walizutumia na kuiba fedha hizo.

Baada ya Hukumu hiyo, Farijala alirudishwa rumande kwa sababu anatumikia kifungo cha miaka miwili jela alichohukumiwa katika kesi nyingine na Maranda aliachiwa lakini bado ataendelea kwenda mahakamani kwa kuwa anakabiliwa na kesi nyingine.

Ndugu na marafiki waliokuwepo katika eneo hilo la mahakama walishukuru mahakama kutoa uamuzi wa haki na kusema kweli Mungu ametenda miujiza.

Membe Arudisha Fomu Ya Urais......Akana Kuhusika Na Ufisadi Wa Mabilioni Ya Libya.

MAKADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamerejesha fomu na kufafanua mambo kadhaa ambayo yamekuwa yanazungumzwa juu yao kama njia ya kujiweka sawa kabla ya uteuzi kufanywa na vikao vikuu vya chama hicho.

Mmoja wa waliorudisha fomu ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye wakati akirudisha fomu za kuomba kuteuliwa na kusema kuwa wanaochukulia suala la urais ni la kufa au kupona wana matatizo kwani anayejua Rais wa Tanzania ajaye ni Mungu.

Alisema safari yake ya kutafuta wadhamini ilikuwa na misukosuko mingi ikiwemo kutokea ajali tatu lakini hakuna ambaye alikuwa ameumia sana.

Akiwa ameongozana na mke wake, Tunu Pinda alisema mwana CCM mkomavu ni yule ambaye yuko tayari kukubali matokeo.

Alisema mpaka sasa ni wanachama wa CCM 42 waliojitokeza kugombea lakini katika hatua ya kwanza ni majina matano tu yatakayoteuliwa na kundi kubwa litaondolewa.

“Mimi sitegemei kwenye mchujo wa watu watano watokee watu wa kunung’unika kwani kila mtu aliyefika kuchukua fomu alikuwa anafahamu kuwa kutakuwa na mchujo kama tuko wengi wako watano kisha unakwenda ngazi ya pili, hakuna sababu ya kunung’unika,” alisema.

Alisema baadaye kuna kwenda kwenye Mkutano Mkuu atabaki mmoja. “Utanung’unikia nini? Kuna kushinda na kushindwa na kuna kupata na kukosa na ukisema suala la Urais ni kufa au kupona basi una matatizo, ifike mahali wana CCM wapate mtu ambaye wanadhani anaweza kusaidia kuongoza,” alisema.

Pia alisema waliojitokeza mwaka huu kuchukua fomu ni wengi. “Tuliojitokeza tusinuniane, kwa nini haniungi mimi mkono, na wewe usione jambo hili ni nongwa na usijione mapenzi ya Mungu yako kwako tu,” alisema.

Pia aliwataka viongozi wenzake washirikiane kumuunga mkono mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM. “Anayejua rais wa Tanzania atakuwa nani ni Mungu peke yake,” alisema.

Mwakyembe arudisha fomu
Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe jana alirudisha fomu na kusema CCM itapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu kutokana na kutekeleza ilani yake vizuri na wananchi kuwa na imani kubwa na chama hicho.

Mwakyembe ambaye alirudisha fomu jana mchana alisema katika safari yake ya kutafuta wadhamini mkoani ameweza kuwaona wanachama wengi wa CCM ambao wanaonesha imani kubwa na chama chao.

Alisema kila alipokutana na wana CCM waliojitokeza kumdhamini kwa tathmini aliyofanya tangu kuanza kwa siasa ya vyama vingi nchini CCM, itashinda ushindi wa kimbunga kwani mtaji upo kutokana na kazi kubwa iliyofanya serikali ya awamu ya nne katika utekelezaji wa ilani.

“Tumejipanga kuhakikisha wanaingia kwenye uchaguzi kifua mbele kutokana na kutekeleza ilani,” alisema.

Pia alisema kwa upande wa pili wana kazi ya kuhakikisha yote mazuri yaliyofanywa na CCM yanasemwa.

 “Tuna kazi ya kuhakikisha kuwakumbusha wananchi barabara za lami na mafanikio mengi yamepatikana na serikali ya awamu ya nne ya CCM,” alisema.

Alisema kazi kubwa ni kuhakikisha umma unatambua CCM imefanya mambo mengi kutokana na upotoshaji unaofanywa na wapinzani kuwa CCM haijafanya lolote.

Pia alisema CCM kuwa na wagombea wengi waliojitokeza mwaka huu ni dalili njema za CCM kutoa fursa za kupatikana mmoja ambaye kila moja atamuunga mkono ili kuweza kukivusha chama.

Dk Mwakyembe alisema yuko tayari kumuunga mkono mgombea atakayeteuliwa na chama. Awali alisema amezunguka katika mikoa 15 katika kutafuta wadhamini.

Dk Mwele Malecela
Mwanachama mwingine wa CCM aliyerudisha fomu jana ni Dk Mwele Malecela ambaye alisema pamoja na kazi kubwa iliyofanywa katika uongozi wa awamu nne bado kuna watu wanaoishi kwenye umasikini uliokithiri.

Alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari. Alisema alifanikiwa kupata wadhamini katika mikoa 20 ikiwemo 17 ya Tanzania bara na mitatu ya Zanzibar.

Alisema wananchi wameonekana kufarijika kuona wanafuatwa kwenye maeneo ya kata walipo. Alisema ameweza kuzunguka mikoa tisa kwa siku nne hali inayoonesha kuwa kazi kubwa imefanyika katika ujenzi wa barabara za lami kuunganisha mikoa.

‘Pamoja na maendeleo na kazi kubwa ya awamu zote bado kuna umasikini uliokithiri lazima kuliangalia suala hilo kama kiongozi na kulitafutia ufumbuzi,” alisema.

Alisema aliguswa sana na wanawake waliojitokeza wakiwemo wazee ambao walikuwa wakitaka kumuona ni mwanamke wa aina gani ambaye anataka kugombea Urais.

“Wanawake wamefurahi sana kuona wanawake tunajitokeza hii ni fursa nzuri ya kuwapa moyo akinamama kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi,” alisema.

Membe Ayakana  Mabilioni  ya  Libya
Membe kwa upande wake wakati anarudisha fomu akijibu swali aliloulizwa kuhusu madai ya kuwa anahusika na ufisadi wa fedha za Libya na kama inavyosambazwa na wapinzani wake, alisema akigundulika kuwa alikula hata dola moja yuko tayari kujiuzulu.

“Uvumi kuwa nahusika na mabilioni ya Libya hauna mashiko kabisa baadhi ya wanasiasa wenzangu wanajua ukweli wote huu lakini kwa makusudi wameamua kuniunganisha na kampuni hiyo na kuwaaminisha watu ni yangu au nina hisa maneno hayo ni ya uongo,” alisema.

Alifafanua kuwa Libya ni moja kati ya nchi wafadhili wa Tanzania ambapo, kama ilivyo wafadhili wengine imekuwa ikiipa Tanzania misaada na mikopo yenye masharti nafuu.

Alisema katika utaratibu huo, Tanzania na Libya zilitia sahihi mkataba wa kubadili madeni na kuyaingiza katika miradi ambao uliweka utaratibu wa matumizi na urejeshaji wa fedha za deni la Libya.

Alisema kumbukumbu alizonazo zinabainisha kuwa kabla ya Serikali ya Libya kuweka saini katika mkataba wa nyongeza iliyotaka fedha hizo zikopeshwe kwa kampuni ya Meis, upembuzi yakinifu wa mradi husika ulifanywa kupitia vyombo vyake, na wao wenyewe kujiridhisha juu ya ubora wa mradi huo.

Sumaye na mahakama ya rushwa
 Naye Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye naye alirejesha fomu alisema akichagulia kuwa Rais wa nchi ataanzisha mahakama maalumu ya wala rushwa.

Mbali na rushwa pia vipaumbele vyake ni pamoja na ufisadi, uhujumu uchumi na kwamba ataunda chombo cha uchunguzi katika masuala hayo.

Pia alisema wakati akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania alifanya mambo makubwa na atahakikisha anaunda serikali inayofahamu kutimiza wajibu wake.

‘Uchumi ninaouzungumzia si wa takwimu ni wa hali halisi, nitaangalia pia maeneo kama viwanda vikubwa na vidogo ili watu wengi waweze kujiajiri na kulinda viwanda vya ndani,” alisema.

Alisema atahakikisha uzalishaji wa viwanda vya ndani unaongezeka na kunakuwa na ongezeko la mauzo ya nje ya nchi. Pia alisema ataimarisha huduma za jamii, ikiwemo elimu, afya upatikanaji wa maji na huduma nyingine muhimu.

Alipohojiwa kama maeneo aliyokwenda kutafuta wadhamini aliombwa rushwa, Sumaye alisema, tangu aanze kazi ya siasa hajawahi kutoa rushwa.

“Hata maeneo ambayo nimekwenda kutafuta wadhamini sijatoa fedha hata zilizodaiwa kwa lugha laini nilikataa kwani nilitaka nidhaminiwe na wale walio na imani na mimi,” alisema.

Alisema wakati akiwa Waziri Mkuu alipambana na wala rushwa ambapo aliweza kuwafukuza kazi watu 3,360 huku wengine 400 walipelekwa mahakamani.

Balozi Mahiga
Balozi Mahiga naye wakati anarejesha fomu alisema ameenda mikoa 15 kwa gari na akawashukuru wana CCM kumlaki na kwamba wamehamasika na wanasubiri kwa hamu uchaguzi.

Alisema kama CCM ikimpitisha kuwa mgombea atahakikisha kuwa anajenga maadili ya uongozi ili kuondokana na vitendo vya rushwa na ufisadi.

Alisema uongozi mzuri ni ule unaojengwa katika misingi ya maadili na atapambana na rushwa ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikirudisha nyuma wananchi wengi.

“Nitahakikisha ninaimarisha misingi ya umoja na mshikamano katika nchi ikiwa ni pamoja na kudumisha muungano wa Tanzania na Zanzibar,” alisema.

Joseph Chaggama
Mwanachama mwingine wa CCM aliyerudisha fomu jana ni Joseph Chaggama ambaye alisema amezunguka katika mikoa 17 wakati wa kutafuta wadhamini. Alisema anaijua CCM vizuri na jinsi Serikali inavyoendeshwa.

Alisema yeye ni mmoja wa watu wasiofahamika na sababu ya kuchukua fomu ni nia ya dhati kutoka moyoni kuwa anaweza kuongoza nchi.

Pia alisema uwezekano wa yeye kuchaguliwa lazima kutokee muujiza. Alisema yuko tayari kuwatumikia Watanzania ikiwa atapewa ridhaa ya kuwa mgombea wa CCM na akashinda uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Pia alisema yuko tayari kumuunga mkono mgombea ambaye atateuliwa na chama.

Monica Mbega
Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Monica Mbega naye alirudisha fomu na kusema kuwa chama kiliweka utaratibu mzuri wakati wakienda mkoani kupata wadhamini katika mikoa 15 ikiwemo mitatu ya Zanzibar.

Alisema amekamilisha kazi yake kwa ukamilifu bila matatizo na kuwashukuru wanawake wengi waliojitokeza kumuunga mkono.

Alisema suala la rushwa linategemea jinsi mtu alivyokwenda wakati akitafuta wadhamini.

Amos akemea matumizi makubwa ya fedha
Mwingine aliyerudisha fomu hizo jana ni Amosi Siyantemi ambaye ni mtumishi wa CCM wakati ambaye alisema kuwa kwenye mchakato wa kutafuta wadhamini baadhi ya wagombea wameonesha matumizi makubwa ya fedha.

“Ni jambo la kujiuliza fedha hizo wamepata wapi na ni kiasi gani ni lazima wachunguzwe na kuchukuliwa hatua,” alisema Siyantemi.

Pia alisema rushwa ni ugonjwa mbaya unaoiangamiza jamii ni lazima zichukuliwe hatua za haraka na makusudi ili kuweza kukomesha suala hilo kabla nchi haijatumbukia kwenye shimo la machafuko.

Alisema CCM ya sasa si kama ile ya Mwalimu Nyerere. “Tunahitaji kurejesha haraka heshima ya CCM machoni mwa Watanzania na kwenye macho ya Jumuiya ya Kimataifa,” alisema.

Alisema akichaguliwa kuwa Rais atahakikisha kunakuwa na huduma bora za matibabu sanjari na bima ya afya kwa kila Mtanzania, kufanya mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa elimu kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kupunguza idadi ya masomo.

Pia alisema atapiga marufuku mauzo na manunuzi yanayofanyika nchini kwa malipo ya dola ambapo malipo ya dola yatafanyika kwa kibali maalumu.

Pia alisema atakuwa na jukumu la kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya sanaa, michezo na burudani yatakayolenga kuwanufaisha kiuchumi wananchi.

Escrow Yaendelea Kumtesa Tibaijuka..Amshambulia Halima Mdee, Adai Anatumiwa na Wabaya Wake Kumchafua


Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amemshambulia Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kwamba vinatumiwa na wabaya wake kumkashifu katika utendaji wake.

Profesa Tibaijuka alitoa shutuma hizo wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Bureza. Alisema alikumbwa na kashfa ya Escrow, kutokana na kupata fedha kutoka kwa kaka yake Rugemalila (James) alizompa kusaidia shule anayoisimamia.

Alikanusha tuhuma zilizotolewa na Mdee bungeni dhidi yake kwamba alipokuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kabla ya kuvuliwa wadhifa huo, alikuwa mporaji wa mali za wananchi hasa kumiliki ardhi kubwa.

Alidai kuwa katika kashfa hiyo, kitendo cha kusema fedha aliyoipata ni ya mboga kwa maana ni ndogo imetafsiriwa na kutumiwa na vyombo vya habari, hasa magazeti kumchafua zaidi ndani na nje ya Tanzania.

“Nasema hapa mbele yenu na waandishi wa habari wapo hapa, magazeti yanafanya biashara kupitia kwangu kwani wanapoandika habari zangu magazeti yananunulika kwa haraka siku husika,” alisema Profesa Tibaijuka.

Alilitaja Mwananchi na magazeti mengine pamoja na baadhi yaliyaitwa kuwa ni ya uchwara ambayo alidai kuwa yamenunuliwa na wabaya wake.

Alidai kuwa Mdee alidanganya bungeni kuwa Profesa Tibaijuka ni mporaji ardhi za wananchi kuanzia jimboni na kama isingekuwa ni kinga ya mbunge kutoshtakiwa, angemfungulia mashtaka mahakamani.

Alisema waandishi wa habari wa magazeti hawaandiki mambo mema aliyofanya jimboni badala yake wamesimama kwenye kashfa ya Escrow lakini yeye hafanyi maendeleo yake kwa fedha hizo, bali ana pensheni ya Umoja wa Mataifa (UN).

“Fedha nilizopata Umoja wa Mataifa bado ninazo na Halima Mdee tutakuja kukutana mbele ya safari kama ni pesa ya kula bado ninayo na ile ya Escrow ya Rugemalila ni kuhemea mboga acheni kudanganyika,” alisema Profesa Tibaijuka.

Aliwaomba wananchi wa kata hiyo kumuunga mkono kwani licha ya kudaiwa kuwa ana umri mkubwa hivyo awaachie vijana, bado yumo na atagombea tena kuwaongoza wananchi akiwa mbunge.

Mdee ajibu mapigo

Akijibu shutuma dhidi yake Mdee alisema alichokisema ni cha kweli na kwamba anao ushahidi kuthibitisha madai yake hayo.

“Asiweweseke kwa kuwa hilo suala la uporaji wa ardhi ni la kweli na wala sikumuonea.”

Kigogo wa Bandari Afumaniwa Ndani ya Mwezi Mtukufu...Ajipiga Faini ya Mil 30..Kisa Kizima Nimekuwekea Hapa



GPL
WE acha tu! Hii ni habari ya kushangaza sana ambayo ilinaswa na paparazi wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers juzikati ambapo mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ally Mwamwanza ambaye ni afisa katika kitengo cha ‘makontena’ bandarini Dar, kudaiwa kunaswa na mke wa jirani yake, Gibson Mtinge aliyetajwa kwa jina moja la Khadija.


Licha ya wote wawili kuishi Mbezi ya Kimara, lakini kisanga hicho kilichojiri mwishoni mwa wiki iliyopita saa 12 asubuhi kilichukua nafasi maeneo ya Tegeta-Kibaoni jijini Dar es Salaam.

OFM YAKATIZA
OFM ilikuwa katika pilikapilika ya kusaka matukio ya usiku katika viwanja mbalimbali vya Jiji la Dar. Wakati inapita nje ya nyumba hiyo, kelele za ‘hoya! Hoya’ ziliifanya OFM kupiga kambi hapo kusikiliza.

OFM NDANI YA GETI
Hoya! Hoya zilipokomaa, ndipo OFM ilipoamua kusukuma geti na kuzama ndani ya mjengo huo wa maana na kukutana na kasheshe ya mwaka, wanaume wawili wakitwangana.Mwanaume aliyejitaja kuwa ni mfanyabiashara wa kusafirisafiri ambaye ndiye Gibson alidai amemfumania Ally akiwa na mkewe kitandani kwenye chumba kimoja ndani ya nyumba hiyo.


“Huyu jamaa nimemkuta na mke wangu. Huwezi kunifanyia hivi bwana Ally. Halafu wewe ni jirani yangu kabisa,” alifunguka Gibson kwa sauti yenye kuweza kufanya lolote kwa wakati huo kama si Mungu kumdhibiti shetani.

MTUHUMIWA ALITOKA KWAKE MUDA WA DAKU
Habari zaidi kutoka kwenye kinywa cha Gibson zilisema kuwa, Ally alikuwa akimtongoza mkewe kwa siku nyingi. Ikafika mahali, mke huyo akachoka na kumweleza mumewe ambapo waliweka mtego.

Siku hiyo, inadaiwa Ally alichati na mwanamke huyo akitaka waonane, mke akamwambia hayupo Mbezi wanapoishi, amelala Tegeta kwenye nyumba ya dada yake kwa vile dada huyo amekwenda Mbeya. Kwa hiyo kama  anataka yeye aende Tegeta.


“Jamaa katoka kwake Mbezi saa 10 alfajiri,  muda ambao watu wanakula daku kwa ajili ya mfungo. Alimuaga mkewe anakwenda kazini,” alisema Gibson huku akivuja jasho maana Ally naye ni bonge.
Ina maana taarifa hizo, Gibson alipewa na mke wake ambaye alikuwa akichati na Ally!

MAJIRANI WAINGILIA KATI
Majirani wa eneo hilo, baada ya kusikia sekeseke walizama ndani na kufanya kazi ya ziada kuwatuliza na kumtaka Gibson amwache Ally avae nguo.


MTUHUMIWA AJIPIGA FAINI
Baada ya vuta nikuvute iliyochukua muda wa saa 3, Ally alikiri kutenda kosa hilo na hivyo kuamua kujipiga faini mwenyewe kwa kusema atampa jamaa huyo mwenye mke kiasi cha shilingi milioni 30 kama fidia ya ugoni.
OFM ilimshuhudia Ally akiyaweka maelezo yake hayo kwenye karatasi na kuanguka ‘signecha’ huku  akitazamwa na mashahidi wawili ambao nao walimwaga wino

A Man Who Lived Close To LUPITA NYONG’O For 3 yrs Reveals Her Ugly Side.

 

After word got out that celebrated actress Lupita Nyong’o was charging Kenyans Ksh 10,000 to dine with her at Villa Rosa Kempinski, many people took it to social media and criticized her for that move.

They felt that the Hollywood based actress had let fame get into her head and she was now feeling like a small god.

Otuma Ongalo, who is a former Senior Editor at the Standard Newspaper, has come out to reveal how the once humble Lupita has become too proud after gaining international fame.
Otuma claims that he once shared a tiny office with Lupita’s mum for three years and she was a humble lady. However, the internationally recognized actress now feels too big and she can no longer shake the hands with “raiyaa” (common mwananchi).

Here’s what the former Standard Newspaper Senior Editor had to say on Lupita’s current behaviour.

Is it true that Lupita Nyong'o is now asking people to cough out 10k just to dine with her? I can't believe that this humble girl is now so overpriced. For almost three years I shared a tiny office with her mum and she was always there doing one or two errands for us though those were the days she was Miss Malaika. I have watched her grow as a high school leaver but she was also a good actor with local outfit. What I can't believe is that she is now too big to even shake my hand.