Arsenal kumnunua Wanyama na Mitrovic
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger
anapanga kumnunua kiungo wa kati wa Southampton Mkenya Victor Wanyama na
mshambuliaji wa Anderlecht Aleksandr Mitrovic kulingana na gazeti la
the Sun nchini Uingereza.
Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni
millioni 30 kwa wachezaji hao wawili,huku Wanyama akigharimu kitita cha
pauni millioni 20 naye mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic
akigharimu pauni millioni 10.
Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka
katika kilabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na kilabu kikubwa huku
naye Mitrovic akiwa amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal katika
kipindi cha wiki chache zilizopotea.
Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier Drogba kutokana na mchezo wake.
Credits:BBC
No comments:
Post a Comment