Monday, 20 October 2014
Makamu wa rais mgeni rasmi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, iliyofanyika jijini Mwanza jana.
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax : 2153426
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki
au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
Aidha, kumeonekana matukio
kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare
za JWTZ. Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama
kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963
Monday, 13 October 2014
KUMBUKUMBU YA MIAKA 15 TANGU KIFO CHA MWALIMU NYERERE
WATANZANIA leo tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa muasisi na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 akiwa nchini Uingereza alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu.
Akizindua rasmi maadhimisho ya kumbukumbu hizo jana, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Kate Kamba alisema kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika mkoani Tabora
Subscribe to:
Posts (Atom)